Dereva na 'Anko' wabaka mtoto wa miaka 6 Dar

Dereva na 'Anko' wabaka mtoto wa miaka 6 Dar

Bongo fleva, Singeli inachangia ubajaji, ushoga?


  • Total voters
    47
  • Poll closed .
Watoto mlionao majumbani pamoja na kuwawekea ratiba ngumu za masomo ya kidunia muwape muda pia wa kumjua Mola wao..Ajabu unakomenti apa kwa uchungu kumbe nawe ktk nyumba Yako unatengeneza “Ma Anko" wa baadae.
 
Hii nchi vitu vingi havina controlling matokeo yake kila kitu kiko Auto mode.

Hizi shule nyingi hazina controlling kwa watoto kila mahala na mamlaka husika ziko kimyaaa kabisa kama hazipo.
 
Nimesoma comments za wanaume humu nimesikitika sana. What a shame! Baadhi yenu mnaonekana kutupa lawama kwa mama wa mtoto. So mnahalalisha huyo mtoto kubakwa? Mungu awaepushie yasiwafike mabinti zenu. Hamtopata nguvu ya kuandika ujinga
 
MTOTO mwenye umri wa miaka sita[6 YEARS] anayesoma darasa la kwanza katika Shule ya Starlight Pre and Primary iliyopo Tegeta Wazo mkoani Dar es Salaam (jina kapuni) amebakwa na wanaume wawili watu wazima kwenye gari la shule, ‘school bus.’

Wanaume hao ni dereva wa basi la Shule ya Starlight Pre and Primary na kondakta wake ambaye anafahamika zaidi na watoto kwa jina la ‘anko’ na kwamba mtoto huyo amekuwa akifanyiwa ukatili huo kwa muda mrefu bila kuwaambia wazazi wake kwa sababu wabakaji hao walikuwa wakimtisha kuwa akisema watamuua.
Akizungumza na Tanzania PANORAMA Blog, mzazi wa mtoto huyo (jina limehifadhiwa) amesema alibaini mtoto wake kufanyiwa kitendo hicho cha kikatili baada ya kulalamika mfululizo kuumwa na tumbo ndipo alipoanza kumdadisi jinsi anavyoumwa huku akimfanyia uchunguzi wa mwili.

“Siamini kwa sababu sikuwahi kufikiria wale watu wazima tena wa shule tunayoiamini kuwafuata watoto wetu nyumbani kuwapeleka shule na kuwarudisha wanaweza kufanya kitendo cha kikatili hivyo. Mtoto alikuwa haishi kulalamika kuumwa tumbo, nimempeleka Kitengule Hospitali zaidi ya mara tano, tunapewa dawa lakini malalamiko ya kuumwa tumbo hayaishi.
“Majuzi akaanza kulia tena tumbo linamuuma, nikachanganyikiwa kabisa maana kila nikienda hospitali hawaoni tatizo, nikaamua kukaa naye chini kumbembeleza huku nikimuuliza tumbo linaumaje, akawa anasita kusema, hapo akili ikashtuka.

“Nikazidisha utulivu huku nikimbembeleza asilie bali aseme linaumaje akasema anaogopa kwa sababu watamuua, nikamuuliza akina nani, hakusema. Nikamwambia hakuna wa kumuua mimi nipo na baada ya kumbembeleza sana ndiyo akaanza kusema dereva na ‘anko’ wa gari lao la shule yaani ‘school bus’ huwa wanambaka, wanambaka kwa zamu.

“Alieleza kila kitu, alisema wanavyomshika mpaka wanavyomvua nguo na wao wanavyovua. Alisema wakati wanarudishwa nyumbani kutoka shuleni watoto wote huwa wanapelekwa kwanza anabaki yeye peke yake kwenye gari, kisha gari linapelekwa eneo la ukimya, wanafunga vioo na mapazia ya kwenye vioo vya gari ndiyo wanamtendea huo unyama, wakimaliza ndiyo wanamrudisha nyumbani huku wakimtisha kuwa akisema watamuua,” alisema mzazi wa mtoto huyo na kuongeza.

“Usiku ule ule tulimpeleka hospitali akapata matibabu ya awali na wakatuambia ni kweli kaishaharibiwa kabisa. Tuliwasiliana na polisi usiku huo huo wakawahi nyumbani asubuhi asubuhi ile gari ya shule ilipofika tu yule dereva akatiwa nguvuni ila huyo mwenzake alikamatwa baadaye wakapelekwa kituo cha polisi cha Madale, kesi namba iliyofunguliwa ni MDL/RB/3889/2022, KUBAKA.

Hivi sasa tunaendelea na matibabu ya mtoto katika Hospitali ya Mwananyamala.

Tanzania PANORAMA Blog jana ilifika Shule ya Starlight Pre & Primary na kukutana na mwalimu mkuu wa shule hiyo ambaye hakuwa tayari kujitambulisha jina na baada ya kuulizwa kuhusu tukio la kukamatwa kwa wafanyakazi wa shule yake, alisema hawezi kuliongea kwa sababu anajiandaa kwenda kuswali hivyo aulizwe meneja wa shule na kumuongoza mwandishi ofisi kwa meneja.

Alipoulizwa meneja wa shule ambaye naye hakujitambulisha jina lake alisema hana taarifa kuhusu tukio hilo na kuomba muda wa kuwasiliana na mkurugenzi wa shule ambaye aliomba kuongea na Tanzania PANORAMA Blog na kukanusha katakata wafanyakazi wa shule yake kubaka mtoto mwenye umri wa miaka sita huku akisisitiza wafanyakazi wake wote wapo kazini kama kawaida.

Baadhi ya wafanyakazi wa shule hiyo waliozungumza na Tanzania PANORAMA Blog wamethibitisha kukamatwa kwa wenzao wawili wanaotuhumiwa kumbaka mtoto huyo na kueleza kuwa uongozi wa shule unafanya kila jitihada kuficha ukweli.

Wakati uongozi wa Shule ya Starlight Pre and Primary ukikanusha kwa nguvu kubwa wafanyakazi wake kukamatwa kwa tuhuma za kumbaka mtoto mdogo wa miaka sita, RPC Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mtatiro Kitinkwi amethibitisha kutokea tukio hilo na kueleza kuwa upelelezi umeishakamilika na jalada la kesi hiyo litapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.​

Credit: PANORAMA Blog.
MY TAKE: Kesi hii watafungwa na mahakama ya wilaya miaka 30 au maisha, mahakama ya Rufaa itawaachia maana ushahidi haukujitosheleza au walipigwa wakihojiwa, au daktari hakuitwa kutoa ushahidi.
View attachment 2430744
~ Watu wakiwatenda vibaya Majahili kama hawa mnawaita Wanyama eti?
Wanatimiza sunna ya mtume Muhamad maana alilala na mtoto wa miaka sita
 
Nimesoma comments za wanaume humu nimesikitika sana. What a shame! Baadhi yenu mnaonekana kutupa lawama kwa mama wa mtoto. So mnahalalisha huyo mtoto kubakwa? Mungu awaepushie yasiwafike mabinti zenu. Hamtopata nguvu ya kuandika ujinga
Nafikiri kuna kitu umeshindwa kuelewa,kama ungeelewa usingekuja na hiki ulichoandika.

Mama wa mtoto analaumiwa hapa(mimi pia nimemlaumu) kwa uzembe, mtoto hawezi kubakwa na wanaume wawili tena kwa kipindi kirefu halafu wewe unajiita mama wa mtoto na hujui. Unakuja kujua baada ya mtoto kuharibika. Huo ni uzembe na hali ya kutokujali.

Mtoto wa miaka sita ni mdogo sana kufanyiwa ukatili tena na wanaume wawili halafu mzazi makini ashindwe hata kushtukia mabadiliko.

Sijui huu uelewa wako wa mama akilaumiwa basi ni kahalalisha mtoto kubakwa umeutoa wapi.

Na kama wewe ni mzazi, jitahidi kumuangalia mtoto wako kwa ukaribu, hakuna majukumu yanayoweza kumfanya mtu asiwe Mzazi. Watu waache uzembe. Ogesheni watoto na wakagueni vizuri acheni kufuga makucha.
 
Wakati mwingine inategemea na mwenekano wa mtoto!unakuta litoto lina miaka 8 au kumi lakini kulingana na mivyakula anayokula anaonekana kama mtu mzima wa miaka 35,hii nayo nadhani inachangia matamanio kimaunekano
🤣🤣🤣 kweli ni wewe kwenye hiyo avatar yako.
 
Wazazi bwana...mnapanuliana huko kwenye starehe zenu halafu mnazalishana bila uelewa....matokeo yake mnamuona mtoto kama kaja kuwaharibia maisha.... mnakuwa wakoloni, hata hao wana nafuu, ni kumfokea mtoto na kumpiga kila unapopata nafasi... mwishowe mtoto wako mwenyewe anakuja kukuogopa hata wakati anapotakiwa kutafuta msaada kwako. Yani ujinga tupu
 
Wakati mwingine inategemea na mwenekano wa mtoto!unakuta litoto lina miaka 8 au kumi lakini kulingana na mivyakula anayokula anaonekana kama mtu mzima wa miaka 35,hii nayo nadhani inachangia matamanio kimaunekano
lukesam njoo usome hii af uje na maelezo yako marefu hivyo. We kwa akili yako unaona ni sawa?
 
Wakati mwingine inategemea na mwenekano wa mtoto!unakuta litoto lina miaka 8 au kumi lakini kulingana na mivyakula anayokula anaonekana kama mtu mzima wa miaka 35,hii nayo nadhani inachangia matamanio kimaunekano
Lione Hilo lichizi hebu peleka ujinga huko
 
kama kubakwa atabakwa na mtu mmoja lakini wawili huo ni uongo maana asingeweza kutembea haki itendeke
 
We jamaa acha ujinga ukiwa mzazi inatakiwa uwe makini sasa yani wanaume wawili tena wa kibongo wambake mtoto h mtoto wa miaka sita afu akaendelea kutembea vizuri tena akilalamika tumbo basi mbuzi nyie huu ni uongo mkubwa sana
Soma vzuri uzi,alafu urudi
 
Huu ni uhaini kabisa, kuharibu nguvu kazi ya taifa, kuua utu wa mtoto...Hawa watu inabidi wawe wananyongwa tu.....
Mimi kama ni mzazi watu kama hawa hata wakipewa miaka 30.ni kufanya figisu kuwatafuta huko waliko...watu kama hawa hawapaswi kuishi kwa amani..ni mtafutano na kisasi mpaka watamani kufa...shenzi kabisa
 
lukesam njoo usome hii af uje na maelezo yako marefu hivyo. We kwa akili yako unaona ni sawa?
Huyo ana matatizo ya akili, ni mgonjwa wa akili ndio anaweza kumtamani mtoto eti kisa ana maumbile makubwa.

Niliona ujumbe wake nikampuuzia.

Mimi nilikuwa natilia shaka umakini wa wazazi wa kileo, mtoto anaingiliwa hadi anaharibika na wao kama wazazi wala hawashtukii.

Huu ukatili kwa watoto umetamalaki sana nchini sasa hivi. Na ukipitia habari zote hata wewe utajikuta umehoji ni wapi nafasi ya mama kwa mtoto? Wengi watoto wanalawitiwa au kubakwa mpaka wanaanza kutoa harufu ndio mzazi anakuja kujua, ni uzembe.
 
kama kubakwa atabakwa na mtu mmoja lakini wawili huo ni uongo maana asingeweza kutembea haki itendeke
Endelea kuamini hivyo mpaka siku yafike nyumbani kwako ndio utajua kuwa kumbe inawezekana.

Hoja yako ni dhaifu sana,kwani hawawezi kuwa wanapokezana, leo anamfanyia dereva, kesho anapumzishwa halafu keshokutwa zamu ya konda?
 
Back
Top Bottom