Dereva mzuri ni yupi?

Dereva mzuri ni yupi?

Yeah me poa tu, we ndo unaadimika sana sijui majukumu ya kumlea vivi
Na kwambia,
sasa hivi muda mwng nakua mwsho wa upepo,network mpk niende kijiji cha pili
 
Hili swali ukiwauliza wengi watakupa majibu yasiyo sahihi na kati yao tena wasomi kabisa watakwambia dereva mzuri ni yule asiyesikiliza abiria wake wanasemaje sahihi kabisa lakini ni makosa makubwa kujiaminisha kwenye dhana hii ama kudhani ndio jibu sahihi

Dereva naye ni binadamu kama binadamu mwingine yoyote sio mkamilifu ana mapungufu yake ....udereva ni fani ni ujuzi wa kusomea darasani kwa kufundishwa na wataalamu ambao nao ni binadamu vile vile

Dereva ni mmoja tu na hapaswi kuwasikiliza abiria ila hiki si kigezo cha dereva bora

Dereva bora ni yule ambaye pamoja na kufuata sheria za udereva na barabarani lakini ana tafakuri ya kuweza kuepusha ajali na kuhakikisha abiria wake wanafika safari yao salama salimini

Dereva mzuri ni yule anayehakikisha chombo chake ni kizima na hakina kasoro yoyote

Kuwa dereva mzuri kuna hitaji zaidi ya kutokuwa na misimamo isiyozingatia hekima weledi na tafakuri
Uendeshaji tahadharishi, huyo ndiye dereva mzuri. Usipite speed kwenye makutano ya feeder roads kisa eti uko kwenye main road. Punguza mwendo maana anaweza akawa nakuja dereva tokea feeder road bila kusimama akaingia main road!
 
Yeah me poa tu, we ndo unaadimika sana sijui majukumu ya kumlea vivi
Nikatika harakati za kumtafutia vivian mkate wa kila siku
Bob marley:Is this love
 
Hahaha unajua kuna wakati ukimsikiliza kiongozi tena wajuu unatamani uzibe masikio maana unakuta hukutarajia kusikia maneno fulani kutoka kwa mtu huyo na hasa ukizingatie level yake ya elimu inahitaji analysis ya mambo kwa hali ya juu.

Hivi kumbe zile namba za simu za makamanda wa polisi wanazoweka kwenye mabasi ili dereva kama hawasikilizi abiria wawapigia ni upuuzi mtupu??Barabara ina alama za kuzizingatia, ina sheria na kanuni za kufuata..... lakini nashangaa dereva anasema hapaswi kusikiliza abiria ikumbukwe Mr. dereva hii si gari binafsi

Kulikuwa na madereva wengi wakiwania kuendesha hili gari. Dereva huyu aliyeko kwenye steering alikuja kwetu kwa unyenyekevu mkubwa kwamba tumpe kazi na kwamba yeye atakuwa dereva wa wote na atamsikiliza kila abiria na atahakikisha ustawi wa kila abiria so tukampa kazi. Safari imeanza tunashuka Kitonga dereva hataki kusikiliza abiria utadhani si yeye aliyeomba kazi kwa unyenyekevu mkubwa. Inasikitisha dereva anaendesha gari kama kabeba matofali na si binadamu wenye ubongo kama yeye. Sijajua vizuri hii safari mwisho wake utakuwa nini kwa kweli maana tunafukia mashimo kwa kwenda mbele, tyres hazina upepo konda anamweleza dereva tusimame gari ichekiwe dereva hataki kusikia chochote anaongeza mwendo tu.
 
Hahaha unajua kuna wakati ukimsikiliza kiongozi tena wajuu unatamani uzibe masikio maana unakuta hukutarajia kusikia maneno fulani kutoka kwa mtu huyo na hasa ukizingatie level yake ya elimu inahitaji analysis ya mambo kwa hali ya juu.

Hivi kumbe zile namba za simu za makamanda wa polisi wanazoweka kwenye mabasi ili dereva kama hawasikilizi abiria wawapigia ni upuuzi mtupu??Barabara ina alama za kuzizingatia, ina sheria na kanuni za kufuata..... lakini nashangaa dereva anasema hapaswi kusikiliza abiria ikumbukwe Mr. dereva hii si gari binafsi
hii si gari binafsi dereva kumbuka hilo
 
Napenda sana unavyotumia fasihi kaka, tunavyoendeshwa hata sielewi dereva anaelekea wapi maana mbele kuna giza nene
 
Dreva gari imepata pancha taa haziwaki giza limeingia yeye anakanyaga tu halafu anadai ati yeye ni dreva mzuri!
 
Me lori sipandi afu kama mkulu ni dereva wa roli basi anaendesha mchanga ila sio watanzania
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom