Dereva mzuri ni yupi?

Dereva mzuri ni yupi?

Hili swali ukiwauliza wengi watakupa majibu yasiyo sahihi na kati yao tena wasomi kabisa watakwambia dereva mzuri ni yule asiyesikiliza abiria wake wanasemaje sahihi kabisa lakini ni makosa makubwa kujiaminisha kwenye dhana hii ama kudhani ndio jibu sahihi

Dereva naye ni binadamu kama binadamu mwingine yoyote sio mkamilifu ana mapungufu yake ....udereva ni fani ni ujuzi wa kusomea darasani kwa kufundishwa na wataalamu ambao nao ni binadamu vile vile

Dereva ni mmoja tu na hapaswi kuwasikiliza abiria ila hiki si kigezo cha dereva bora

Dereva bora ni yule ambaye pamoja na kufuata sheria za udereva na barabarani lakini ana tafakuri ya kuweza kuepusha ajali na kuhakikisha abiria wake wanafika safari yao salama salimini

Dereva mzuri ni yule anayehakikisha chombo chake ni kizima na hakina kasoro yoyote

Kuwa dereva mzuri kuna hitaji zaidi ya kutokuwa na misimamo isiyozingatia hekima weledi na tafakuri


Kwa maana hiyo unakiri kuwa Magufuli ni dereva mzuri maana anatafakuri sahihi na anatetea wanyonge ambao ndio wengi hapa Tanzania.
 
Dereva mzuri ni huyu
tapatalk_1492061866227.jpeg
 
mtu mwenyewe anakwambia kabeba abiria kwenye lori, tangu lini lori likabeba abiria,
 
Kusema kwamba dereva mzuri ni yule asiyesikiliza abiria wake sidhani kama ni sahihi.
Yaani dereva we ukae tu macho mbele hata kama mizigo inaanguka usikilizi we mwendo "mbere"
Basi sawa, kuna mtu anataka kuchimba dawa, ukimwambia atachimba 2020 atachafua hali ya hewa kwenye lori tulilopanda.
 
Lori ni gari la kubeba mizigo. Lakini hutokea mara chache likabeba watu hasa nyakati za misiba wakati wa kwenda kuzika au kubeba wafuasi wa Chama Cha Mashinani kwenda kwenye mikutano ya kampeni.

Sasa la ajabu dereva wa lori aliyepakia mizigo unaomba ushauri kwa watu ambao hawapo ndani ya gari kwa kuandika maandishi haya nyuma ya roli lake HOW AM I DRIVING? au NAENDESHAJE? na kuweka namba ya simu ili apigiwe kuelezwa juu ya uendeshaji wake, inakuwaje huyu wa kwetu hataki kutusikiliza sisi abiria wake tuliomo ndani ya lori lake? Kama anayumba hovyo barabarani, anaturusha kwa spidi kwenye matuta na wemgine ni wajawazito tusimwambie? Kuna wengine wamezidiwa wanataka kuchimba dawa na dereva hataki kusikiliza abiria je wajisaidie humo humo? Je tukisema anaendesha kidikteta tutakuwa tunakosea? Na je tukisema hakupitia mafunzo ya udereva na ana leseni ya mtaani tutakuwa tumekosea. Maana dereva mzuri ni yule anayepokea maoni na ushauri wa abiria wake na walio nje. Sasa mfano abiria anakwambia amepigiwa simu kuwa huko mbele kuna roli jingine limeanguka barabarani au daraja limebomoka sasa anakwambia dereva uchukue tahadhali na wewe hutaki si mwisho utaenda kuwa bwaga na wewe mwenyewe kufa. Tafadhali dereva wetu wa lori nenda NIT ukasome!
 
Back
Top Bottom