Depo mpya

Depo mpya

CIA mgumu

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2022
Posts
961
Reaction score
1,961
Habari za mda huu ndugu zangu, mchana huu nipo njiani kwenda Njombe kuangalia parachichi zangu, sasa nimepanda bus kutoka chuo cha police moshi na kuna vijana ndio wanaenda kuanza kazi.

Ajabu ni kwamba vijana hawa wameanza majigambo hata kabla hawajafika kituo cha kazi , tumepita pale geti la mtera afisa uhamiaji akaingia ndani kutukagua sie ngumbaru akasalimia vizuri kawatania kidogo madogo wakati anatoka nje ya basi ndio madogo wanaishia kurusha madongo na dharau.

Je, Hii ni heshima na nidhamu waliofundishwa huko?
 
Bado hawajazoea vazi huwa kuna kaulimbukeni fulani tu ka muda sasa wangekuwa wametoka kuutafuta mshati si ndo ingekuwa balaa, wasamehe tu watazoea.
Ndio hivyo mkuu nimeshawasamehe maana hata mimi waliniona boya ila baada ya mda kupita wakajua huyu ni mlima parachichi wakanyea coz kuna mkuda akawasanua
 
Matani gani embu tuambie ukute amewadharau halafu WEWE unategemea wanyamaze
Hapana mkuu hajawadharau kawasalimia salamu ya poleni na safari na hongereni kwa mafunzo na nendeni mkatimize wajibu wenu, sasa madogo baadae yakaanza unatukaguaje sisi wewe ni uhamiaji tu duuuh nilinyamaza kimya
 
Wanakuwaga na kiherehere kinoma hawa.. Afu muda wote hujihisi kama Raia zinawadharau, so hupenda kulazimisha uwatambue. Mbaya zaidi uwe Janki kama wao.

Bora kukutana na Askari Mtu mzima kuliko hivi vidude..
Wakubwa zao wanaowaongoza kuwagawa vituo tunafahamiana sasa shida kwenda kukaa nao siti moja huko na miili yetu hii ndio ikawa madharau full
 
Hao bado wana moto wa mafunzo,ni kawaida hiyo hali,wakitulia mtaani wenye common sense watarudi kukaa sawa,wengine watakuwa na sumu za kudumu.
 
Ukweli mkuu, kama mmoja hivi namuona hadi macho ni shidaa
Hao bado wana moto wa mafunzo,ni kawaida hiyo hali,wakitulia mtaani wenye common sense watarudi kukaa sawa,wengine watakuwa na sumu za kudumu.
I
 
Bado hawajazoea vazi huwa kuna kaulimbukeni fulani tu ka muda sasa wangekuwa wametoka kuutafuta mshati si ndo ingekuwa balaa, wasamehe tu watazoea.
Weee weee balaa la askari mpya ni hatari hasa hawa wa uu mshati mshatii mara full mayoko hata akitembea anawaza hivi hawa wanajua mimi mbaka baka wakienda pass ya kwanza baada ya mafunzo ya awali salaleeee ila wakishakaa mwaka naa kitu hivi basi hivyo muwasamehee bure jameeni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom