Wakubwa baada ya gazeti la JAMHURI kuchapisha habari nyingi za uchunguzi, mwaka huu kwa mara nyingine tena limenyakua tuzo ya mwandishi bora.
Deodatus Balile, Mhariri Mtendaji wa Gazeti la JAMHURI ameibuka mshindi kwa kupata tuzo ya uandishi bora kwa Mwaka 2014.
Habari yake iliyoshinda ni ile iliyosaidia kuvunja mtandao wa dawa za kulevya nchini, ambapo Serikali baada ya habari hiyo imerekebisha sheria na sasa anayesafirisha dawa za kulevya ni kufungwa tu, hakuna faini.
Huu ni ushindi wa pili kwa gazeti la JAMHURI baada ya mwaka jana, Naibu Mhariri Mtendaji, Manyerere Jackton kushinda habari za uchunguzi katika eneo la Maliasili na Utalii.
Shukrani za pekee ziwaendee waandaaji wa tuzo na wafanyakazi wenzangu kwa ushirikiano mkubwa na kwa mara nyingine gazeti la JAMHURI limethibitisha kuwa TUNAANZIA WANAPOISHIA WENGINE.
Tafadhali endeleeni kutuunga mkono kwa kusoma gazeti LA JAMHURI.
Balile, D.
Mhariri Mtendaji,
Jamhuri Media Ltd