Deo Fulikunjombe aomba mwongozo kukomesha tabia ya kufuja muda

Hata mimi hili suala la kutaja majina huwa linanitatiza sana.Mimi nafikiri waziri akisema hiyo list iingie kwenye hansard kama ilivyo itaingia tu, si lazima ataje majina ya watu wote waliochangia kwa kusema na kwa maandishi. Namuunga mkono.

My take: Mimi akija Deo Kugombea jimboni kwetu kwa tiketi ya CCM simpi kura ng'o! tumechoshwa na mfumo wa utawala wa CCM, umeshindwa ku-deliver.

Kwahiyo nyie wenye uelewa msiendelee kuchelewesha ukombozi kwa falsafa zenu zilizoshindwa. Mimi nachagua CHADEMA from now, mtu akija na kichama chake napiga chini tu siangalii.
Bosi hata Shibuda kisa Chadema!! No way akatafute jimbo la ujira wa mwiha na siyo jimboni kwangu mimi na nafamilia yangu tutampa kura mgombea Ccm kana anatosha.
 
Nachomsifu Deo Philikunjombe anajua kusoma majira na nyakati...amejitenga na siasa za chama chake, na amesimama kama yeye binafsi, na hili litamasaidia sana, maana ukitaka kuonekana mavi mbele ya watanzania wenye akili kwasasa, jaribu kujifungamanisha na siasa za CCM...tazama watu kama Lusinde, Mwigulu nk wanaonekana wapuuzi kwasababu ya kujifungamanisha na siasa uchwara za CCM.
 
Wana Jf sasa ni dhahiri Deo Fulikunjombe anaingia rasmi kwenye vitabu vya kihistoria, kwa kuwa natumia simu ngoja niwe short and clear.

Ni hivi, kumekuwa na tabia ya Mawaziri kupewa dakika 40 kujibu hoja za Wabunge, lakini cha kustaajabisha waziri anatumia dakika 20 kutaja majina ya wabunge waliochangia bajeti badala ya kujibu hoja.

Sasa Deo ameomba muongozo wa Spika kama jambo hili ni sahihi au kiti kitamke kulikomesha mara moja.

Speaker atatowa mwongozo baadaye kabla ya kusitisha shughuli za Bunge za asubuhi.

My Take: Wanaodhani sisi hasa mimi Matola nina ugomvi na CCM wanajidanganya, nahitaji kuwa na mbunge wa aina hii bila kujali chama chake, hata kama leo Deo Filikunjombe akigombea jimboni kwangu kwa tiketi ya CCM nitampigia kura yangu bila tabu yoyote. Mimi msimamo wangu huwa nachaguwa mtu na siyo chama.

Spika amejibu nini kuhusu mwongozo huu Matola
 
Last edited by a moderator:
Siku nikimsikia Mnyika anawashukuru vimada nitamlima memo mara moja mimi kama mpiga kura wake. Tumemtuma kutuwakilisha na sio kutoa shukrani na blah blah zingine.
 
Update:Naibu spika Job Ndugai amemkatisha Waziri wa fedha kusoma majina ya waliochangia baada ya kuanza kusoma msululu wa majina katika majumuisho yake jioni hii, amesema wazi ni kupoteza muda. Hongera sana Fulikunjombe dozi imewaingia na imeanza kufanyiwa kazi kwa vitendo.
 
kutoa shukrani.
kutaja wachangiaji kwa majina.
kutambulisha wageni.
kutambulisha vilabu.
kutoa rambirambi.
kulalamika sana then mwishoni kuunga mkono hoja.
kuunga mkono hoja mwanzo wa kuchangia halafu tena kuongea kwa kirefu.
 
kutoa shukrani
kutaja wachangiaji kwa majina
kutambulisha wageni
kutambulisha vilabu
kutoa rambirambi
kulalamika saaana then mwishoni kuunga mkono hoja
kuunga mkono hoja mwanzo wa kuchangia halafu tena kuongea kwa kirefu
ujira wa mhiha!
 
kutoa shukrani
kutaja wachangiaji kwa majina
kutambulisha wageni
kutambulisha vilabu
kutoa rambirambi
kulalamika saaana then mwishoni kuunga mkono hoja
kuunga mkono hoja mwanzo wa kuchangia halafu tena kuongea kwa kirefu
Madam Speaker naye kwenye hili hayuko nyuma, kwenye kipindi cha maswali na majibu Waziri akiulizwa swali yeye anamwambia Waziri naomba ujibu kwa kifupi sana! Mwe!!
 
Mwigulu nchemba juzi ameingiza wachungaji kama wageni wake bungeni .... leo tena amewaalika mashehe kama wageni wake bungeni kutoka katika jimbo lake

Teh the the .... anahaha kweli kweli ... Dr. Kitila Mkumbo ameshawasha taa za kijani anapita
 
ni sawa na mwanafunzi asiyrjua jibu la swali basi anaanza kiandika andika anachokifiria ilimradi aomekane alijaribu
 
Mbunge anaweza kuwa mzuri wa fikra lakini kama hayupo chama chenye sera nzuri ni kazi bure.
Ni ukweli kwamba Filikunjombe anamtizamo mzuri kisiasa lakini jukwaa alilosimama tayari limeshaoza na mbaya zaidia liosimama nao hapo juu wanacheza sindimba au kupiga kwata. Hivyo pindi litapoanguka wote wataanguka nalo.


[/QUOTE]Kuchagua mbunge au rais sababu ya sera ni kuzidi kudandanyana na kuingizana kwenye mashimo ambayo vigumu kutokamo. Sera vyama vyote vina sera nzuri sana kuanzia na CCM yenyewe.

Angalia sera za CCM ambazo tumeziimba miaka yote ni nzuri mno lakini je, watendaje wake ni wazuri kama sera zenyewe? CCM inafuata sera za awali kabisa za kujenga msingi wa taifa linalojitegemea.

Sasa angalia Mwenyekiti wa CCM ambaye ni rais anavyopitisha bakuli la kuomba huku na huko kana kwamba hatuna rasilimali hapa nchini? Nchi yetu ina rasilimali kuzidi mataifa makubwa yaliyoendelea na sera za CCM zililenga huko lakini nothing is done.


CHADEMA inaweza kuwa na sera nzuri za kuwajali wanyonge lakini si kila kiongozi ana uwezo wa kuongoza na kuelekeza utekelezaji wa sera na kodi za wananchi. Angalia Mwanza kabla ya miaka miwili meya ameachishwa kwa sababu ya kushindwa kuongozi na kufuata miongozo, hiki ni kipimo tosha kuhusu hoja yako ya sera.

Wenye elimu na akili pevu huchagua mtu anayefaa badala ya kuchagua wa kutoka chama fulani, huchagua uwezo wa mtu badala ya kuchagua mradi tu anatoka chama fulani hayo ndiyo yaliyotufikisha hapa.
 
Wana Jf sasa ni dhahiri Deo Fulikunjombe anaingia rasmi kwenye vitabu vya kihistoria, kwa kuwa natumia simu ngoja niwe short and clear.

Ni hivi, kumekuwa na tabia ya Mawaziri kupewa dakika 40 kujibu hoja za Wabunge, lakini cha kustaajabisha waziri anatumia dakika 20 kutaja majina ya wabunge waliochangia bajeti badala ya kujibu hoja.


Matola, nilishaanza kuweka mada nyingi tu hapa siku za nyuma kuhusu huyo Mbunge Filikunjombe, nilivyoandamwa hapa na kutukanwa, na wengine kufikiria ni yeye mwenyewe Filikunjombe ndiye anayeweka mada hizo. Na wengine kuniambia natumiwa au nalipwa naye, yote ni sababu ya tofauti za uwezo wa kusoma jambo na mtu na kujenga ufahamu mathubuti.

Nilishaona sana mambo yake ambavyo haonyeshi wote, anajali wapiga kura wake, mtetezi wa wanyonge, haoni haya kujichanganya na kushirikiana na wabunge wengine wa vyama vingine kwa masilahi ya taifa. Ingwa sijawahi hata mtia machoni mwangu Mbunge huyu, ila tu nimefurahishwa na mazuri ambayo wengi sasa mnyayaona.

Tunahitaji watu kama hawa bila kujali itikadi zao kwani sote malengo ni kuleta maendeleo kwa taifa letu. Sijapendezwa na kila moyo ukipenda ndiyo yanayodidimiza maendeleo kwani hatuangalii mambo kiakili bali rangi ya chama kwani ni mtazamo finyu mno.

Great thinkers wako makini kuangalia ubora wa mtu bila kujali anatoka wapi au chama gani.
 
Ni hoja ya msingi aliyoileta!
Deo mbona anajulikana Way back kuwa ni mwanamageuzi ndani ya ccm!
Na hata hizo dakika 20 zilizobaki zinamegwamegwa kwa kumshukuru mkewe kipenzi na watoto wake wazuri walioko St. Feza!
jamani mnataka wasitushukuru? ngoja na wewe siku ukiwa waziri utamshukuru hata jirani yako.
Umesahau, namshukuru na mchungaji kwa Maombi ya kila siku na kuniweka kwenye ulinzi wa Mungu............... wakati ni mtuhumiwa wa ubadhilifu wa mali ya Umma, sasa sijui Mchungaji huwa anaombea nini!
 
jamani mnataka wasitushukuru? ngoja na wewe siku ukiwa waziri utamshukuru hata jirani yako.
Umesahau, namshukuru na mchungaji kwa Maombi ya kila siku na kuniweka kwenye ulinzi wa Mungu............... wakati ni mtuhumiwa wa ubadhilifu wa mali ya Umma, sasa sijui Mchungaji huwa anaombea nini!

Mkuu najua mchango wangu hauhusiani na siasa. msinishambulie
Huyo dada wa kwenye avatar yako huwa namzimia sana. usiibadilishe ili niendelee kusuuzika moyo
 
Mkuu timbilimu, mi mwenyewe nilimsikia kama sio Spika alikua Naibu wake, Kuna waziri alikua anataka kuacha kutaja majina ya wachangiaji kwa akili ya muda, akaambiwa awataje tu kwa kua huo muda hauhesabiwi. Hapa tunazungumzia Bunge la Makinda, sio la wakati wa Sita

Ndugu Zanta natumaini umepata majibu ya hoja yetu. Naibu Spika ktk kikao cha jioni amemzuia Waziri kusoma majina ya wachangiaji kwamba ni kupoteza muda. Ametakiwa aanze kujibu hoja za Wabunge!
 
Muda wa kutaja majina hauhesabiwi kwenye ule muda anaopewa Waziri kujibu hoja.

Nadhani umefanya tathmini kinyume. Muda wa kutaja majina ni muda wa 'kikao' cha bunge hata kama hauhesabiwi lakini bado unapunguza muda wa bunge. Mawaziri wanashindwa kujibu hoja nyingi sana za wabunge kwa sababu muda wa bunge 'hautoshi'. Pitia hansard utaona wabunge wengi wanakosa hata muda wa kuchangia kwa sababu 'muda hautoshi' (maneno ya spika). Lakini wakati huo huo wanatumia hata huo muda mchache kushukuru wake zao, kutaja majina ya wabunge, na kutambulisha wageni wao!

Bunge la Tanzania ni kichefuchefu. Uchaguzi mkuu ulifanyika mwaka 2010, lakini leo hii 2012 mbunge anasimama na kushukuru wapiga kura wake kwa kumchagua! Hivi kwenye campaign alisema ataenda bungeni kuwashukuru?
 
Back
Top Bottom