Deo Fulikunjombe aomba mwongozo kukomesha tabia ya kufuja muda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Deo Fulikunjombe aomba mwongozo kukomesha tabia ya kufuja muda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Matola, Aug 15, 2012.

 1. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Wana Jf sasa ni dhahiri Deo Fulikunjombe anaingia rasmi kwenye vitabu vya kihistoria, kwa kuwa natumia simu ngoja niwe short and clear.

  Ni hivi, kumekuwa na tabia ya Mawaziri kupewa dakika 40 kujibu hoja za Wabunge, lakini cha kustaajabisha waziri anatumia dakika 20 kutaja majina ya wabunge waliochangia bajeti badala ya kujibu hoja.

  Sasa Deo ameomba muongozo wa Spika kama jambo hili ni sahihi au kiti kitamke kulikomesha mara moja.

  Speaker atatowa mwongozo baadaye kabla ya kusitisha shughuli za Bunge za asubuhi.

  My Take: Wanaodhani sisi hasa mimi Matola nina ugomvi na CCM wanajidanganya, nahitaji kuwa na mbunge wa aina hii bila kujali chama chake, hata kama leo Deo Filikunjombe akigombea jimboni kwangu kwa tiketi ya CCM nitampigia kura yangu bila tabu yoyote. Mimi msimamo wangu huwa nachaguwa mtu na siyo chama.
   
 2. Mromboo

  Mromboo JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 726
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Ni vizuri namimi pia nakuunga mkono. ila uwe makini na spellings zako usije leta maana tofauti na wazo lako. nice time.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ni hoja ya msingi aliyoileta!
  Deo mbona anajulikana Way back kuwa ni mwanamageuzi ndani ya ccm!
  Na hata hizo dakika 20 zilizobaki zinamegwamegwa kwa kumshukuru mkewe kipenzi na watoto wake wazuri walioko St. Feza!
   
 4. d

  decruca JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mimi naona huwa hawana majibu ya kueleweka, sasa wanaona watumie muda huo kuuza chai, then nusu uliobaki ndio wapige blabla, inakera.
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  CCM wanamchukia Deo kuliko hata ya Tundu Lissu!!!! Mfano halisi wa bingwa wa kutaja watu ni yule Naibu waziri aliyeibiwa zile silaha zake za maangamizi kule morogoro pamoja ni milaptop minne na Simu zinazo jaa kiroba huwa akitaja wake zake huwa nachoka kwasababu anawataja mpaka mademu wake wa Moro waliomliza
   
 6. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,334
  Likes Received: 2,648
  Trophy Points: 280
  Mkuu hata kama unasema unachagua mtu, lakini kumbuka sera na ilani ya chama kilichopo madarakani ndivyo vinavyoongoza nchi.
  Mbunge anaweza kuwa mzuri wa fikra lakini kama hayupo chama chenye sera nzuri ni kazi bure.
  Ni ukweli kwamba Filikunjombe anamtizamo mzuri kisiasa lakini jukwaa alilosimama tayari limeshaoza na mbaya zaidia liosimama nao hapo juu wanacheza sindimba au kupiga kwata. Hivyo pindi litapoanguka wote wataanguka nalo.
   
 7. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Na kama umeangalia vizuri,nyuma ya Deo amekaa Mama Zakia Megdji(?)...wakati Deo akieleza Mama alikuwa anatikisa kichwa kuashria hakubaliani na mtazamo wa Deo...Na Utashangaa kuna sehemu ya hotuba huwa hawaisomi lakn wanasema hansard iandike!sasa kwanin na majina wasiache na waseme Hansard iandike?
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Spika na uongozi mzima wa bunge wana mapungufu makubwa. Wanatumia muda mwingi sana kutambulisha wageni badala ya kufanya kazi waliyotumwa na watanzania. Hakuna mbunge aliyetumwa kupeleka wageni Dodoma, kama watu wanatembelea bunge kuna sababu zipi za kuwatambulisha? Ni Tanzania tu ambapo Spika anaweza kutumia (kwa wastani) dakika 10 kila siku ya kikao kutambulisha wageni binafsi wa wabunge! Huku ni kuhujumu haki za watanzania. Bunge ni mahali pa kujadili kero za wananchi, wageni wanaokuja wafanye hivyi kimya kimya unless ni mtu mashahuri anayealikwa kwa niaba ya nchi (sio mbunge mmoja mmoja).

  Kuhusu mawaziri kutaja majina, hii ni fedheha kubwa sana. Dr Mgimwa alitumia dakika 29 kutaja majina ya wachangiaji, naibu wake akatumia dakika 10! Na ujue ni jinsi gani tatizo la kukariri linavyotafuna nchi hii, kila waziri utasikia akitaja jina la mchangiaji na kumalizia kusema 'mbunge'! Hivi kuna mtu anaweza kuchangia mjadala bungeni kama sio mbunge?

  Tatu, bunge linatakiwa sasa likae chini na kuweka utaratibu wa kutoa shukrani, au salamu za rambirambi. Sio kila mtu anasimama kusema kitu kile kile. Wanaweza kuamua chief whip toka chama tawala na kambi ya upinzania wakishatoa salamu za pongezi au rambirambi basi inatosha. Pia bunge sasa liweke utaratibu maalum wa ku-respond mara kunapotokea janga la kitaifa au msiba unaogusa taifa.

  Kwa mfano, ni wakati gani au ni mtu wa aina gani akifa bunge litasimama kwa dakika moja? Huu mtindo wa kufanya mambo kwa kunusa 'umaarufu' na kutafuta photo opportunities unaleta mtafaruku.
   
 9. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  kwa kweli hata mimi huwa nachukia unakuta waziri anasoma majina zaidi ya hamsini,majina yenyewe ya kibantu tuliyonayo ni marefu kutaja jina kamili,ukiongeza na neno mheshimiwa ni nusu dakika!matokeo yake wanaoteza muda sana,unakuta atamaliza kutaja majina yote lakini hatamaliza kujibu hoja za wabunge,sasa majina au majibu ya hoja!its high time huu utaratibu uangaliwe!
   
 10. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,659
  Likes Received: 21,878
  Trophy Points: 280
  Bunge la blabla. Waziri anapoteza muda kumshukuru mama yake kwa kumzaa na kumtunza hadi kupewa uwaziri huo si ujinga?
   
 11. Utanijua

  Utanijua JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 211
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 60
  Ni kweli jamaa kasema jambo la maana,wanatajwa mpaka watu ambao hawana mchango wowote wanatupotezea muda tu mara nawashukuru watoto wangu, mke wangu, dereva kwa uvumilivu,uvumilivu wao sisi unatuhusu nini wakaambiane warudipo majumbani
   
 12. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #12
  Aug 15, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  "nyimbo nzima wanatajataja majina..
  (Tenaa)
  Kwa mistari isio na vina"

  By...D
   
 13. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kwa mfano

  Wizara ya Ulinzi:

  UTANGULIZI
  1. Mheshimiwa Spika, baada ya Bunge lako Tukufu kupokea taarifa iliyowasilishwa..

  2. Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu,
  aliyenijalia afya njema na kuniwezesha kuwasilisha hotuba yangu ya bajeti kwa
  mwaka 2012/2013. Pili namshukuru kwa dhati Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuniteua kuwa
  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Nawathibitishia Waheshimiwa Wabunge
  wenzangu na wananchi wote wa Tanzania kwamba nitatekeleza majukumu niliyokabidhiwa
  kwa umakini na uaminifu mkubwa.

  3. Mheshimiwa Spika, tatu napenda kutumia fursa hii kuwapongeza Mawaziri na Manaibu
  Mawaziri walioteuliwa kushika nyadhifa hizi hivi karibuni.

  Vile vile nampongeza Mhe. James Mbatia (Mb.) kwa kuteuliwa na Mhe. Rais kuwa Mbunge.
  Nampongeza pia Mhe. Mussa Azan Zungu (Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge.
  Vile vile napenda kuwapongeza Watanzania waliochaguliwa na Bunge letu Tukufu kuwa Wabunge
  wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

  4. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2011/2012
  Wabunge wenzetu watatu waliiaga dunia. Wabunge hao ni Marehemu Jeremia Sumari,
  Marehemu Mussa Silima na Marehemu Regia Mtema. Napenda kutoa pole za dhati kwako
  Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge, ndugu, marafiki na Watanzania wote kwa ujumla
  kwa msiba huo mkubwa uliotupata. Namuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho zao Peponi. Amin.

  5. Mheshimiwa Spika, halikadhalika, napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Kamati ya Bunge
  ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Edward Lowassa
  ,
  Mbunge wa Monduli kwa kutupa ushauri na mapendekezo mazuri sana wakati wakichambua
  mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yangu. Kamati hii imekuwa
  ikiishauri vyema Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kuhusu njia mbalimbali za
  kuimarisha utendaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Jeshi la Kujenga Taifa ili liweze
  kutekeleza majukumu yake ya Ulinzi wa nchi yetu.

  6. Mheshimiwa Spika, kabla sijatoa maelezo yangu kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2012/2013
  napenda kuungana na Waheshimiwa Wabunge kuwapongeza Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda (Mb),
  Waziri Mkuu, Waziri wa Fedha, Mhe. Dk. William Mgimwa (Mb), na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu),
  Mheshimiwa Steven Wasira (Mb) kwa hotuba zao ambazo zimetoa mwelekeo katika masuala ya Mipango, Uchumi,
  Mapato na matumizi ya Serikali kwa kipindi cha mwaka 2012/2013.
  ===============================
  ?????
   
 14. peri

  peri JF-Expert Member

  #14
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  sio tu kwenye kutaja majina, hata kutambulisha wageni sidhani kama kuna umuhimu kusema leo tuna mtoto wa mh fulani, mara wanafunzi wa shule fulani, mara madiwani nk.
  Ni kupoteza muda kusiko na msingi.
  Kuna vitu vingi muhimu vya kujadiliwa na bunge.
   
 15. N

  Newvision JF-Expert Member

  #15
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tumetoka mbali lakini hii tabia ya Wabunge has wa CCM kupoteza muda wa thamani ambao sisi wapiga kura tumeulipia haitabadilika mpaka Wana CCM wenyewe wakubali kuwa sasa hatuna muda wa kupoteza na tunataka hoja zenye nguvu za kuleta maendeleo. Hii imejikita pia hata katika lugha nyingi ndani ya Bunge za kuongea mambo ya utani eti "namshukuru ndugu yangu au mtani wangu......" lugha za namna hii zinamfanya hata yule waziri/muhusika unayemuaddress kufanya utani na hoja pia.Ni lazima tubadilike na tuache kuwafanya wapiga kura wa Tanzania ya leo ni mbumbu. Deo anajua hivyo
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Niko jimbo la Mnyika, siwezi changua Kenge yeyote hata awe na rangi gani kutoka chama cha Magwepande!
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Mkuu kama umenisoma vizuri hapo juu nimesema natumia simu, tangu niwe Member hapa Jf ni jana tu ndio nimeanza kutumia simu na nauona ugumu wanaokumbana nao Members wenzetu wanaotumia simu.
   
 18. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #18
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  1.hiyo kutaja mlolongo wa wachangiaji ni kufuja muda
  2.kutoa shukrani kwa mke, mume watoto vimada, wajomba , bibi babu, shangazi ni kufuja muda
  3.kutaja mlolongo wa wageni waliofika bungeni ni kupoteza muda
  4. Kupigana vijembe na taarabu bungeni na kupiga meza muda mrefu ni kufuja muda

  Kifupi bunge letu halina discpline ya muda hata kidogo na ni kutokana na udhaifu wa kiti cha speaker ambacho nachelea kusema kipo wazi tangu alipoondolewa mzee wa speed na viwango
   
 19. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #19
  Aug 15, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Ndugu Mwenyekiti napenda kuchukuwa fursa hii kumshukuru Rais kwa kunichagua kuwa Naibu waziri.
  Napenda kuwashukuru familia yangu mme na watoto kwa kunivumilia maana muda mwingi siko nao.
  Ndugu mwenyekiti naomba kuwashukuru wananchi wa jimbo langu kwa kunichagua.
  Ningependa kumshukuru driver wangu kwa kazi nzuri.
  Ndugu mwenyekiti hoja ni nyingi nitajibu zingine kwa maandisha.
  Nashukuru sana
   
 20. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #20
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Muda wa kutaja majina hauhesabiwi kwenye ule muda anaopewa Waziri kujibu hoja.
   
Loading...