Denti 'KIGAGULA' asimamishwa Shule!

Denti 'KIGAGULA' asimamishwa Shule!

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,519
Reaction score
167,188
Yule denti 'KIGAGULA' asimamishwa Shule!

Uongozi wa Shule ya Msingi Liwiti, Tabata, jijini Dar es Salaam umemsimamisha masomo denti wa kike Rehema Maneno, wa darasa la tano anayedaiwa kuwaroga madenti na mateacher wake.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa teacher mkuu wa skonga hiyo,aliyemtaja teacher anayeumwa kwasasa baada ya kudaiwa kurogwa na denti huyo kuwa ni Julius Mjwahusu, ambaye hali yake kiafya si nzuri.

Kadhalika Head Teacher huyo anakiri kuwepo kwa hofu ya madenti wa shule hiyo dhidi ya Rehema, ambaye baada ya kuhojiwa alikiri kumroga Mwalimu Julius na wanafunzi wengine shuleni hapo.

Anasema uongozi wa shule hiyo umemsimamisha masomo kwa muda wakati kamati ya shule na bibi mlezi wa mwanafunzi huyo aitwaye Rehema Abdallah wakihojiwa.

“Kwa sasa tumemsimamisha masomo Rehema ili tuchunguze tuhuma dhidi yake... ni vigumu kuthibitisha uchawi, hivyo tutapokea vipimo vya hospitali vya mwalimu na huyu mwanafunzi pia tutampima akili zake.

Kwa maneno yake denti huyo kigagula, anakiri kuwa ni mchawi aliyefundishwa na bibi yake mzaa baba, aliyemtaja kwa jina la ‘Nywele Zangu’, mkazi wa Tabata Kimanga akishirikiana na rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Jeniffer.
 
Here we go again!

Wapi Rama mla Watu? Kesi yake iliishia wapi? Last time nilmwona pale Mahakama ya Kisutu na Msalaba Mkubwa!
 
Kuna tetesi kuwa huyo mwalimu anayedaiwa kulogwa ana 'drums' na habari yote ni kutafuta jinsi ya kumlaumu huyu mwanafunzi. Pia inadaiwa kuwa ni unyanyapaa wa hali ya juu kwa huyu mwanafunzi
 
Nasikitika sana kwani siku hizi hata tukiumwa ukimwi tunasingizia kurogwa na kutisha watoto wakiri hata wasichokijua... sina imani sana na hii tabia ya kupromote uchawi hovyo...

tuwroge akina Rostam basi
 
yule denti 'kigagula' asimamishwa shule!

uongozi wa shule ya msingi liwiti, tabata, jijini dar es salaam umemsimamisha masomo denti wa kike rehema maneno, wa darasa la tano anayedaiwa kuwaroga madenti na mateacher wake.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa teacher mkuu wa skonga hiyo,aliyemtaja teacher anayeumwa kwasasa baada ya kudaiwa kurogwa na denti huyo kuwa ni julius mjwahusu, ambaye hali yake kiafya si nzuri.

Kadhalika head teacher huyo anakiri kuwepo kwa hofu ya madenti wa shule hiyo dhidi ya rehema, ambaye baada ya kuhojiwa alikiri kumroga mwalimu julius na wanafunzi wengine shuleni hapo.

Anasema uongozi wa shule hiyo umemsimamisha masomo kwa muda wakati kamati ya shule na bibi mlezi wa mwanafunzi huyo aitwaye rehema abdallah wakihojiwa.

"kwa sasa tumemsimamisha masomo rehema ili tuchunguze tuhuma dhidi yake... Ni vigumu kuthibitisha uchawi, hivyo tutapokea vipimo vya hospitali vya mwalimu na huyu mwanafunzi pia tutampima akili zake.

Kwa maneno yake denti huyo kigagula, anakiri kuwa ni mchawi aliyefundishwa na bibi yake mzaa baba, aliyemtaja kwa jina la ‘nywele zangu', mkazi wa tabata kimanga akishirikiana na rafiki yake aliyemtaja kwa jina la jeniffer.

jamani si akaroge wale mawakili waliopeleka kesi ya dowans kule mahakama kuu!!natamani kuhudhuria msiba wao
 
Mbona huyo mtotoamemtaja bibiye kuwa ndio mwalimu wake wa uchawi?
Mi nadhani kuna haja ya kumuuliza huyo mtoto amemrogaje huyo mwalimu
 
Back
Top Bottom