2007-11-13 17:00:25
Na Sharon Sauwa, Kinondoni
Mwanafunzi mmoja wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu Dar es Salaam amejikuta akiumia vibaya na kulazwa wodini akiwa hoi baada ya kujirusha toka kwenye ghorofa ya pili ya jengo mojawapo la chuo hicho, kampasi ya Mlimani.
Taarifa za Kipolisi zinasema mwanafunzi huyo wa Shahada ya Uhandisi aliyetambulika kwa jina la Geofrey Gustafu, 26, amejirusha kutoka ghorofa ya pili na kuumia vibaya ikiwa ni pamoja na kuvunjika mguu wa kulia baada ya kubambwa na polisi wakati akiwa mbioni kukomba kompyuta mojawapo ya chuo chake hicho.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jamal Rwambow, amesema tukio hilo limetokea jana, mishale ya saa 9:00 alasiri, katika Jengo la Uchanganyaji Kemikali (Chemical Processing) chuoni hapo.
Akasema Kamanda Rwambow kuwa wakati askari polisi wa chuo hicho wakiwa lindoni katika jengo hilo, wakamuona mwanafunzi huyo akifungua ofisi zilizopo katika jengo hilo na kuchukua kompyuta tatu.
Akasema kufuatia tukio hilo, polisi hao walifyatua risasi hewani ambazo zilimtia hofu Geofrey na kumfanya ajirushe kutoka katika ghorofa alilokuwa.
Kamanda Rwambow akasema kitendo cha kujirusha lwa mwanafunzi huyo ndicho kilichomfanya aumie na kuuvunjika mguu wa kulia.
Akasema hivi sasa, mwanafunzi huyo amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Hata hivyo, akasema Kamanda Rwambow kuwa Polisi bado wanaendelea na upelelezi zaidi wa tukio hilo kufuatia kuripotiwa kwa matukio kadhaa ya wizi wa kompyuta na vifaa vyake katika chuo hicho.
SOURCE: Alasiri
Du! We kijana unajifunza wizi badala ya uhandisi? Kitu gani ulikosa hadi uamue kufanya uliyofanya?
Mbona habari inajichanganya(angalia Bold)?
Alikuwa mbioni kuchukua au alishazichukua hizo komputa?
Alizibebaje hizo pc tatu kutoka ghorofani?
Nchi hii sasa noma, na hao askari nao!
Walifyatua risasi akiwa anakimbia?
Siku hizi bwana Polisi kwa risasi.