Denti Chuo Kikuu Dar ajirusha toka ghorofani

Hume

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
340
108
2007-11-13 17:00:25
Na Sharon Sauwa, Kinondoni


Mwanafunzi mmoja wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu Dar es Salaam amejikuta akiumia vibaya na kulazwa wodini akiwa hoi baada ya kujirusha toka kwenye ghorofa ya pili ya jengo mojawapo la chuo hicho, kampasi ya Mlimani.

Taarifa za Kipolisi zinasema mwanafunzi huyo wa Shahada ya Uhandisi aliyetambulika kwa jina la Geofrey Gustafu, 26, amejirusha kutoka ghorofa ya pili na kuumia vibaya ikiwa ni pamoja na kuvunjika mguu wa kulia baada ya kubambwa na polisi wakati akiwa mbioni kukomba kompyuta mojawapo ya chuo chake hicho.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jamal Rwambow, amesema tukio hilo limetokea jana, mishale ya saa 9:00 alasiri, katika Jengo la Uchanganyaji Kemikali (Chemical Processing) chuoni hapo.

Akasema Kamanda Rwambow kuwa wakati askari polisi wa chuo hicho wakiwa lindoni katika jengo hilo, wakamuona mwanafunzi huyo akifungua ofisi zilizopo katika jengo hilo na kuchukua kompyuta tatu.
Akasema kufuatia tukio hilo, polisi hao walifyatua risasi hewani ambazo zilimtia hofu Geofrey na kumfanya ajirushe kutoka katika ghorofa alilokuwa.

Kamanda Rwambow akasema kitendo cha kujirusha lwa mwanafunzi huyo ndicho kilichomfanya aumie na kuuvunjika mguu wa kulia.

Akasema hivi sasa, mwanafunzi huyo amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Hata hivyo, akasema Kamanda Rwambow kuwa Polisi bado wanaendelea na upelelezi zaidi wa tukio hilo kufuatia kuripotiwa kwa matukio kadhaa ya wizi wa kompyuta na vifaa vyake katika chuo hicho.

SOURCE: Alasiri

Du! We kijana unajifunza wizi badala ya uhandisi? Kitu gani ulikosa hadi uamue kufanya uliyofanya?

Mbona habari inajichanganya(angalia Bold)?
Alikuwa mbioni kuchukua au alishazichukua hizo komputa?
Alizibebaje hizo pc tatu kutoka ghorofani?


Nchi hii sasa noma, na hao askari nao!
Walifyatua risasi akiwa anakimbia?
Siku hizi bwana Polisi kwa risasi.
 
Maisha magumu Dar- wanafunzi wanaanza kujifunza wizi mapema!
Sasa unadhani huyu binti akikabithiwa- mali ya uma- ataionea huruma kweli!
 
Maisha magumu Dar- wanafunzi wanaanza kujifunza wizi mapema!
Sasa unadhani huyu binti akikabithiwa- mali ya uma- ataionea huruma kweli!

Mzalendo, huyo dogo ni mwizi na siamini kama ndiyo mara yake ya kwanza inawezekana ni mwizi hata huko nyumbani kwao anapotoka. Ina kuona wasomi wetu wanajiingiza katika vitendo vya wizi wakiwa chuoni je wakikabidhiwa madaraka makubwa itakuwaje?
 
Ni aibu tupu kwa wasomi tunaodhani kesho tutawapa nchi kusimamia mabarabara na majengo mengine ya serikali.

Du! kumbe akina karamagi tunao wengi sana. when will the beautiful ones get born in these african countries? that question worries me much.
 
Aisee wizi ni kitu kibaya sana- kwa wote- ila kwa mwanake inashtua zaidi!

Sasa kama hajaolewa- atakayemwoa atakuwa amapata bom!
 
Bwana wezi wanaanzia kuanzia kwenye familia. Nakumbuka chuo kikuu pale ukianika Jeans hapo nnje inabidi uchunge hadi ikauke otherwise wataikomba wenzio. Mademu kule Hall III na Hall VII ndio usisema walikuwa wanaibiana Chupi kama hawana akili nzuri.
 
Mtoto wa Mkulima,
Kuibiana chupi wanawake vyouni ni kawaida- ni tabia ya mtu. Ila wizi wa Computer Chuo Kikuu- hii sii kawaida!
 
Mtoto wa Mkulima,
Kuibiana chupi wanawake vyouni ni kawaida- ni tabia ya mtu. Ila wizi wa Computer Chuo Kikuu- hii sii kawaida!

Mzalendo, mwizi ni mwizi tuu mkuu. Kama mtu anapata nafasi ya kuiba chupi akafanikiwa akipata nafasi ya kuiba kitu kikubwa ataiba tuu. Kwanini asiibe komputer akauze ili anunue chupi nyingi?
 
mwizi ni mwizi tuu mkuu. Kama mtu anapata nafasi ya kuiba chupi akafanikiwa akipata nafasi ya kuiba kitu kikubwa ataiba tuu. Kwanini asiibe komputer akauze ili anunue chupi nyingi?[/QUOTE said:
That is logical enough!
 
Ila miye huu wizi ulivyoripotiwa unanichanganya, kwani walianza kusema alikuwa mbioni kukomba komputa, mara wakaendelea kusema walinzi walimuona akichukua komputa tatu.

Swali, Aliwezaje kubeba komputa tatu?
Na hao askari walimfyatulia risasi wakati gani?
Na je kulikuwa na ulazima wa kufyatua risasi?
 
Jamani mbona mi sioni mahali popote walipotaja jinsia yake? whai i see is the name GEOFREY unless linamaanisha ni mwanamke ntendelea kuamini ni mwanaume. After all experience inaonyesha wanawake vyouni hawawezi kufanya wizi wa aina hiyo direct. Hata hivyo sishangai coz wezi UDSM ni wengi tu na kitu cha kawaida pale na what are we expecting kama wakubwa wenyewe ni wezi wa raslimali za nchi na pia wanawanyima mikopo? sitetei wizi coz hata mi nishaibiwa cm hostel ndani ya chumba usiku wa manane tukiwa tumelala bila kushtuka hadi asubuhi tulipokuta dirisha liko wazi. Hiyo ndo Udsm watu wanaiba hata kwenye ATM pale
 
Jamani mbona mi sioni mahali popote walipotaja jinsia yake? whai i see is the name GEOFREY unless linamaanisha ni mwanamke ntendelea kuamini ni mwanaume. After all experience inaonyesha wanawake vyouni hawawezi kufanya wizi wa aina hiyo direct. Hata hivyo sishangai coz wezi UDSM ni wengi tu na kitu cha kawaida pale na what are we expecting kama wakubwa wenyewe ni wezi wa raslimali za nchi na pia wanawanyima mikopo? sitetei wizi coz hata mi nishaibiwa cm hostel ndani ya chumba usiku wa manane tukiwa tumelala bila kushtuka hadi asubuhi tulipokuta dirisha liko wazi. Hiyo ndo Udsm watu wanaiba hata kwenye ATM pale

Kwa Suala la jinsia, hata miye najua ni mwanaume, hilo la binti sijui limepatikana wapi. Labda wahabarishaji wawe walikosea jina!

Aliiba CPU tupu nini, manake ukichanganya na monitor sina uhakika kama mtu aweza kubeba tatu, labda kama ana nyenzo!
 
Mpaka naondoka MUCHS, wezi walikuwa wakikamatwa(toka mtaani) walikuwa hawapewi nafasi ya kurudi kwao kuhadithia experience hiyo...ilikuwa ni one way ticket kuzimu. Wanafunzi tulikuwa hatuibiani wala kuiba mali za chuo. Bongo watu wamezidi tamaa, ndio maana wakina sisi tunaona 'maadili' ni halali kujumuishwa ktk mapambano haya ya kifkra. Watu inabidi mmoja mmoja kwa wakati wake wabadilike ili mambo yaende sawa hapo bongo!!!. Personal responsibility ni nyeti mno.......wakati nipo high school kuna jamaa aliiba viatu vya mtu, akashikwa kavi ficha ndani ya cover la godoro lake, jamaa akapata aibu kubwa sana na wakati wa likizo akanywa sumu kujiua kwasababu ya aibu hiyo!!. Huyu mwizi maisha yake hayatakuwa sawa again, ataishi na hii aibu for the rest of his life!!!!
 
Maisha magumu Dar- wanafunzi wanaanza kujifunza wizi mapema!
Sasa unadhani huyu binti akikabithiwa- mali ya uma- ataionea huruma kweli!

Mzalendo, nadhani huyu mwizi ni mwanaume, maana jina lake ni GEOFREY. Sasa kama jina hili linatumika hata kwa kina dada basi leo nitakuwa nimechemsha.
 
Mie nashauri Polisi wachunguze wizi Huu. maana hapa habari inaleta utata. Hasa ukiangalia kila kona UDSM kuna geti la Polisi na wanachunguza kila kinachotoka. na ukitoka na kitu lazima uwe na copy ya karatasi inayoonesha umetoka nayo wapi na sababu kibao. Unless iwe LAPTOP, maana hio hawa-iangalii. Wizi wa vitu vidogo nguo, chupi huwa havina udhibiti na jambo la kawaida UDSM, Mabibo na kwingineko.
Inawezekana kijana ni mwizi kweli lkn pia inawezekana kijana alikuwa akipiga msuli, aliposikia RISASI ktk hali ya kutaka SALAMA yake akajorusha.
Pia naungana na wenzangu juu ya kuukomesha wizi wa kila NAMNA. uwe wa KALAMU au Nguvu. Kila mtu achukie wizi ktk NAFSI yake, lkn pia TUACHE TAMAA na STAREHE MBWA. wengi tunahitaji utajiri wa haraka, TUACHE, TUACHE...jana alikuwa kijana wa Ki-SUDAN ya KUSINI age below 15..ameomba watu waache VITA na WAACHE ULEVI...
 
Mzalendo, nadhani huyu mwizi ni mwanaume, maana jina lake ni GEOFREY. Sasa kama jina hili linatumika hata kwa kina dada basi leo nitakuwa nimechemsha.

Mhhhhhhhhh Mzalendohalisi kwa kweli umetuchanganya tangu lini Geofrey akawa mwanamke. Majina ambayo tunaweza kuchanganyikiwa kuhusu jinsia ni haya ya Kizaramo, kama vile Ajuaye, Siwawezi nk
Lakini hili la Geofrey sikubali kama ni mwanamke labda uniambie ulikuwepo ukamuona kwamba aliyehusika ni mwanamke tujue lilikosewa jina likawa ni la mwanaume wakati mwizi ni mwanamke.
 
Heading aliyopost Hume ndo imenifanya kudhani ni binti- kumradhi!
Denti Chuo Kikuu Dar ajirusha toka ghorofani
 
This student has lost the plot. Hivi hii ni tabia au ni ugumu wa maisha chuoni?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom