Tanga: Afisa wa TRA ajirusha ghorofani na kufariki

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Arusha, Richard Walalaze (35) amekutwa amefariki baada ya kujirusha kutoka ghorofani jijini Tanga.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Henry Mwaibambe amesema kuwa mfanyakazi huyo amejirusha kutoka ghorofa ya pili ya Hoteli ya Ocean Breez jijini Tanga alikokuwa amepanga chumba tangu Julai 16 mwaka huu.

Mwananchi imefahamishwa kuwa Richard alikuwa miongoni mwa watumishi wa TRA waliokuwa jijini Tanga kwa kazi maalumu ya kuandaa taarifa ya Mamlaka hiyo ya mwaka.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma
- Mapya yaibuka ofisa TRA anayedaiwa kujiua hotelini
 
Back
Top Bottom