Denis Msaky atoka Mwananchi atimkia Mtanzania

Denis Msaky atoka Mwananchi atimkia Mtanzania

Mkuu, mbona unaweka post mfululizo kabla hata haujajibiwa? Sasa si ungeunganisha maneno yote katika post moja?



We hujui kama hawa misukule wa LB 7 FC wanalipwa kwa idadi ya post!
Mwenzako yupo kibaruani hapo yaani anaingiza 7000.
 
msacky kaamua kuingia rasmi kwenye timu ya ushindi 2015!, sisi wasoma trend, tunasema kaamua kuchukua uamuzi wa busara!. Sio unakuwa tuu mwandishi wa habari siku zote za maisha yako, lazima ujiandae for changes!,

hakuna ubishi kuwa mwananchi ndilo gazeti makini kuliko yote na top in town, ila kuendelea kuajiriwa na mcl ni kukubali kuwa mwandishi wa habari maisha yako yote na utazeekea newsroom!. Kwa lugha nyingine pale msacky alipofikia akiwa mwananchi ndio palikuwa mwisho wake akisubiri kuzeeka, hivyo amefanya uamuzi wa busara sana kwenda mahali ambapo atapanda juu zaidi na zaidi kufuatia trend ya mtanzania!.

Angalieni alianza salva, mwangalie alipo sasa!, akafuatia muhingo, mwangalie alipo sasa!, akaja kibanda ambaye niliamini ndie angekuja kumpokea salva mikoba, come 2015!, sasa msaky nae kaenda, duu na mimi najiuliza sijui niamue kurejea newsroom?!, yaani nijirudishe mwenyewe utumwani kukubali kuwa mtumwa for 2015!.

Any way, hakuna ubishi kuwa msaky ni jembe, ili ikubukwe siku zote mafanikio ya mfugaji bora, ni watoa pasi wazuri, its a team work that matters!, unaweza kukuta msaky aliweza kungara mwananchi kutokana na timu iliyokuwepo mwananchi, msishangae kama ata flop mtanzania!.

Sakina datoo ilikuwa hivyo hivyo, aling'ara sana na sunday citizen kulifanya ni gazeti la never miss!, alipohama na kuhamia guardian on sunday aliishia ku flop!.

Ila pia hii concentration ya mafahali katika hili hili zizi moja la mgombea wetu wa 2015, linaniogopesha!, huku bashe, kule kibanda, sasa msaky! Who's next?!.

Pasco.

uzuri nyie mnajuana bwana,sisi yetu macho na masikio
 
Pasco unazeeka, yaani uandishi wako unaji contradict kichizi. :A S 13:
Hawa kina pasco wameshakuwa kama kina liyongo ni watu wa kusubiri fadhila za ukuu wa wilaya tu!!! mimi simshangai
 
Pasco,

Mkuu huna uhakika kama Lowasa atakuchukua akishinda?
 
Mkuu Alex, pole!, hebu nisome tena na tena huku umetulia, hakuna contadiction yoyote!. La kuzeeka nalikubali, ila ukijiona umeipitia te na na tena bado hunielewi, then I'm sorry for you, bado unahitaji level fulani ya uelewa kuweza kunielewa!. Can't help it!.
Pasco

Pasco,
Contradictions zako ziko hapa!BTW uliweza kuipata ile movie ya Pascali's Island?

Angalieni alianza Salva, mwangalie alipo sasa!, akafuatia Muhingo, mwangalie alipo sasa!, akaja Kibanda ambaye niliamini ndie angekuja kumpokea Salva mikoba, come 2015!, sasa Msaky nae kaenda, duu na mimi najiuliza sijui niamue kurejea newsroom?!, yaani nijirudishe mwenyewe utumwani kukubali kuwa mtumwa for 2015!.
 
Kaingia CCM rasmi,sijui MoU yake na Zitto ime-expire au terminated kwa hiyo kakimbilia kwa Lowasa??!!

Zitto yuko CCM na inawezekana ni kambi ya Lowassa!!! Kwa hiyo anakwenda pale kwa maandalizi!!! Hadi uchaguzi 2015 tutaona kila rangi.
 
New Habari Corporation wameamua kujiimarisha hasa katika kipindi kinachokaribia kampeni za uchaguzi mkuu kupitia magazeti kwakuwa wanamchukua na Sholei aliyerithiwa na Tido pale Mwananchi
 
Pasco

Kama kwa mhariri kama Muhingo kuwa Mkuu wa Wilaya unaona kuwa hayo ni mafanikio , basi wewe ni wa kusikitikiwa tu
 
Msacky asidanganye umma ukweli wenyewe ni huu.
1/Msacky amekuwa akionywa mara kadhaa na waajiri wake kuwa aache kuandika habari kwa kutumiwa na wanasiasa fulani lakini akawa mkahidi.

2/Tayari mkataba wake na mwananchi ulikuwa unaenda kufutwa kwa kuwa Msacky alishindwa kuufuata vyema.

3/Amekuwa na mahusiano mabaya na waandishi wengine wa Mwananchi na hivyo mara kadhaa wamiliki wake walishinikizwa kumfukuza.

4/Mapato ya Gazeti la Mwananchi yalishuka sana toka Msacky akiwa anaandika habari za kizushi dhidi ya CHADEMA.

*Kifupi Denis Msacky sio Mwandishi mzuri kimaadili na kitaaluma zaidi ya ujanja ujanja wa kutumia Pesa na kununuliwa kirahisi sana na wanasiasa husuasani watawala, tabia ambazo wamiliki wa Gazeti la Mwananchi wanazichukia sana.
 
Mwandishi Denis Msaky alikuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi na swahiba mkubwa wa Zito Kabwe. Hatimaye sasa jamaa kaamua kuondoka Mwananchi (amefukuzwa?) na kuhamia gazeti la Mtanzania ambalo linamilikiwa na Rostam Aziz. Huko Bwana Msaky anakwenda kuungana na Absalom Kibanda ambaye ndie Mhariri Mtendaji wa New Habari.

Msaky ndie ambaye inasemekana (kwa mujibu wa mwendesha mashtaka) kuwa alipangiwa njama za kutekwa na Wilfred Lwakatare ambaye ni mkurugenzi wa usalama wa Chadema. Ndie mhariri ambaye amekuwa akitumiwa sana na Zitto katika maswala yake ndani ya Mwananchi kwa muda mrefu hali ambayo ilisababisha hata gazeti hilo kuanza kupoteza umaarufu wake.

Pia inadaiwa kuwa Msaky alikuwa akitumiwa na Edward Lowassa kama kiungo kikuu kwenye Mwananchi maana EL ana mtu katika payroll yake (hasa wahariri) katika karibu kila gazeti kubwa na chombo kikubwa cha habari hapa Tanzania.

Tutarajie ufufuo mpya wa Gazeti la Mtanzania baada ya kupata mhariri mpya? Au tutarajie kurejea kwa ubora wa Mwananchi kama zamani baada ya kibaraka wa Zitto na Lowassa kuondoka huko? Tusubiri
 
Aiseee, 2015 imekaribia!!! Sema sasa hawataandikwa sana maana wamekatazwa kampeni za wazi kwa miezi 12. Ila Denis ni opportunistic sana!!!!! Achunge sana siasa na weledi wa kazi yake!!!! Best wa ZZK!!
 
Mtanzania kwani lipo? Mwananchi nitalirejea sasa kama kaondoka..lilishapotea.
 
maybe, ila huyu kijana Msaky si mwema katika kuleta mabadiliko nchini kwani ana link na Ikulu, na hii yote imetokea baada ya Mh. tido Mhando kuona muelekeo wa huyu kijana juu ya MCL si mwema, Enzi za Shollei kama MD wa MCL kijana alikuwa anajiona sana na alimkamata sana Shollei na kwa vile alikuwa na link na Ikulu hivyo kumfanya Shollei asitimize malengo mazuri ya MCL, na hata shollei alipotaka kuwa muwazi juu ya nchi hii kupitia gazeti la Mwananchi alikiona cha moto, muda wake ulipoisha wa kukaa TZ hakuongezewa mda na hivyo kumfanya arudi kwao Kenya na kumkabidhi Tido.Msaky si mwema katika tasinia ya Habari.
 
SIRI NZITO YA MSACKY NA LOWASSA HII HAPA
Huu ni mkakati MAHUSUSI wa
kuzuia rasimu ya Katiba. Unasukwa
na Makongoro Mahanga na Denis
Msacky, kupitia kinachoitwa, "Mradi
wa kumfikisha Lowassa Ikulu."
Hii imepatikana huku Denis Msacky
akiwa amejiunga na Rostam Aziz –
Habari Corporation – kutokea gazeti
la MWANANCHI katika kuhakikisha
Edward Lowassa anaingia
madarakani kwa jua au mvua
mwaka 2015.
Anakwenda Ikulu kufanya nini? Jibu
lake ni rahisi sana. Kuiba na
kumlipizia kisasi Jakaya Kikwete,
ikibidi hata kumfunga gerezani.
Basi!
Huko ndiko walikopanga kumtumia
mwandishi huyu wa habari
kufanikisha vizuri malengo yao.
Hapa wamedhihirisha ule mtandao
wao uliowahi kuanikwa na gazeti la
----------- wakati fulani, Zitto -
Msacky - Rostam.
Kabla ya hata uchaguzi wa
mwenyekiti wa Bunge la Katiba
haujafanyika, gazeti tayari
limefanya mahojiano na Mahanga.
Soma mwenyewe.
Katika mkakati huu, Msacky na
kundi lake, wameapa kufa kupona
kuhakikisha rasimu ya Katiba ya
serikali tatu haipiti. Ni kwa sababu
ya hofu ya kutibua move za urais za
mzee wa Monduli.

CHANGAMOTO KWA MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM
SAMWEL SITTA.pdf
 
Imetulia ila imwage yote na madata ful nataka nika iprint ni wasambazie wabunge wa bunge la katiba hapa dodoma wajue mambo hy
 
wapambe nuksi. lowassa na kikwete hawajakutana barabarani, lowassa =chenge= sitta=kikwete=tanzania imara. mtahangaika sana
 
Back
Top Bottom