Denis Msaky atoka Mwananchi atimkia Mtanzania

Denis Msaky atoka Mwananchi atimkia Mtanzania

Mongoiwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Posts
524
Reaction score
271

Kuna Habari kwamba Mhariri Mkuu Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi Denis Msacky, ameacha kazi rasmi huko na kwamba sasa atajiunga rasmi New Habari na kuwa Mhariri Mkuu Mtendaji wa Gazeti la Mtanzania kuanzia sasa.
 
huyu jamaa ni mtu makini mno. hapana chezea yeye. chadema wamejaribu sana kumuua lakini wameshindwa.
 
Mkuu wa Usalama Chadema akamatwa

rwakatare.jpg

Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Chadema,Wilfred Lwakatare

Na Bakari Kiango na Fidelis Butahe, Mwananchi
Posted Jumatano,Marchi13 2013 saa 21:9 PM
Kwa ufupi

Siku nzima ya jana mitandao ilikuwa imetawaliwa na habari ya picha ya video ikimwonyesha Lwakatare akidaiwa kupanga mikakati ya kumteka Mhariri Mtendaji wa Mwananchi, Dennis Msacky. Lwakatare alionekana akitoa maelekezo kwa watu, ambao sura zao hazikuonekana, akiwataka kufuatilia nyendo za Msacky.
 
Lwakatare Alionyeshwa akiwataka watu hao kumkamata na kumdhuru Msacky, kisha wamtupe mbali kama njia ya kumnyamazisha. Alikuwa anamtuhumu Msacky kama alikuwa anashirikiana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ili kukihujumu chama chao.
 
lwakatare kwenye video anasema
"Inabidi mfahamu nyendo za mtu huyu, kama anapenda vitu kama kutembea usiku au kinywaji anachokunywa," alinukuliwa kwenye mtandao huo.

Pia anaonekana kwenye video hiyo akitoa mbinu mbalimbali za namna ya kufanya utekaji nyara.
 
watanzania tunaendelea kuilaani chadema na lwakatare kwa uovu uhalifu na tabia yao ya kupenda kula nyama za watu
 
Msacky kaamua kuingia rasmi kwenye timu ya ushindi 2015!, sisi wasoma trend, tunasema kaamua kuchukua uamuzi wa busara!. Sio unakuwa tuu mwandishi wa habari siku zote za maisha yako, lazima ujiandae for changes!,

Hakuna ubishi kuwa Mwananchi ndilo gazeti makini kuliko yote na top in town, ila kuendelea kuajiriwa na MCL ni kukubali kuwa mwandishi wa habari maisha yako yote na utazeekea newsroom!. Kwa lugha nyingine pale Msacky alipofikia akiwa Mwananchi ndio palikuwa mwisho wake akisubiri kuzeeka, hivyo amefanya uamuzi wa busara sana kwenda mahali ambapo atapanda juu zaidi na zaidi kufuatia trend ya Mtanzania!.

Angalieni alianza Salva, mwangalie alipo sasa!, akafuatia Muhingo, mwangalie alipo sasa!, akaja Kibanda ambaye niliamini ndie angekuja kumpokea Salva mikoba, come 2015!, sasa Msaky nae kaenda, duu na mimi najiuliza sijui niamue kurejea newsroom?!, yaani nijirudishe mwenyewe utumwani kukubali kuwa mtumwa for 2015!.

Any way, hakuna ubishi kuwa Msaky ni jembe, ili ikubukwe siku zote mafanikio ya mfugaji bora, ni watoa pasi wazuri, its a team work that matters!, unaweza kukuta Msaky aliweza kungara Mwananchi kutokana na timu iliyokuwepo Mwananchi, msishangae kama ata flop Mtanzania!.

Sakina Datoo ilikuwa hivyo hivyo, aling'ara sana na Sunday Citizen kulifanya ni gazeti la never miss!, alipohama na kuhamia Guardian on Sunday aliishia ku flop!.

Ila pia hii concentration ya mafahali katika hili hili zizi moja la mgombea wetu wa 2015, linaniogopesha!, huku Bashe, kule Kibanda, sasa Msaky! who's next?!.

Pasco.
 
Yote maisha kikubwa ni kazi msack anafanya kazi kitaluma siyo kishamba kama mhariri wa tanzania daima.
 
Mkuu wa Usalama Chadema akamatwa

rwakatare.jpg
Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Chadema,Wilfred Lwakatare
Na Bakari Kiango na Fidelis Butahe, Mwananchi

Posted Jumatano,Marchi13 2013 saa 21:9 PM
Kwa ufupi

Siku nzima ya jana mitandao ilikuwa imetawaliwa na habari ya picha ya video ikimwonyesha Lwakatare akidaiwa kupanga mikakati ya kumteka Mhariri Mtendaji wa Mwananchi, Dennis Msacky. Lwakatare alionekana akitoa maelekezo kwa watu, ambao sura zao hazikuonekana, akiwataka kufuatilia nyendo za Msacky.
Haya tuone kama lwakatare atamfuata na huko tena mwisho wa siku ukweli wote bayana.
 
Kila la kheri na maandalizii ya 2015! Ila kwa mwandishi makini kuondoka MCL kwa nafasi ile kwa ajili ya tamaa ya fursa za 2015 ni jambo la kifikirishaa pia.
 
watanzania tunaendelea kuilaani chadema na lwakatare kwa uovu uhalifu na tabia yao ya kupenda kula nyama za watu
Mkuu, mbona unaweka post mfululizo kabla hata haujajibiwa? Sasa si ungeunganisha maneno yote katika post moja?
 
Pasco unazeeka, yaani uandishi wako unaji contradict kichizi. :A S 13:
 
Mawazo mengine, Pasco unamuita jembe mtu unayesema kafuata fursa za Urais 2015?
 
Kaingia CCM rasmi,sijui MoU yake na Zitto ime-expire au terminated kwa hiyo kakimbilia kwa Lowasa??!!
 
Pasco unazeeka, yaani uandishi wako unaji contradict kichizi. :A S 13:
Mkuu Alex, pole!, hebu nisome tena na tena huku umetulia, hakuna contadiction yoyote!. La kuzeeka nalikubali, ila ukijiona umeipitia te na na tena bado hunielewi, then I'm sorry for you, bado unahitaji level fulani ya uelewa kuweza kunielewa!. Can't help it!.
Pasco
 
Mawazo mengine, Pasco unamuita jembe mtu unayesema kafuata fursa za Urais 2015?
Mongo, mtu kama ni jembe ni jembe!, ujembe ni ability, ila ili hilo jembe liweze kulima, inategemea terrain, hata jembe liwe vipi, kwenye kichuguu utahitaji sururu, na kwenye swamps utahitaji rato!.

By the way, him ni Off topic, vipi ulifanikiwa kufuata ushauri wangu huu,
Wosia wa Ask. Moses Kulola kwa Watanzania: Tuchague Rais kwa ...

nilikushauri kwenda kumuomba msamaha Askofu Kulola kabla hajazikwa, kuhusu ule uzushi uliomzushia humu!.
Pasco.
 
Kuna Habari kwamba Mhariri Mkuu Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi Denis Msacky, ameacha kazi rasmi huko na kwamba sasa atajiunga rasmi New Habari na kuwa Mhariri Mkuu Mtendaji wa Gazeti la Mtanzania kuanzia sasa.
Mission accomplished!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom