Denis Magesa na fursa za kazi Ulaya na Marekani ni kweli?

GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
4,134
5,244
Habari Wana Jf.

Twende kwenye mada moja kwa moja, huyu jamaa wa kuitwa Denis Magesa anapatikana kwenye Mtandao wa YouTube,Ana dai kuwatafutia watu kazi za mashambani, kazi za udereva na kuosha vyombo katika nchi za Ulaya na marekani ambapo hizo kampuni zinakulipia kila kitu visa, nauli, makazi na chakula endapo utafanikiwa kuitwa kwenda kufanya kazi huko ughaibuni.

Nimewahi kuwasiliana nae kwenye whatsapp akanieleza gharama za kukuombea kazi,kukutengenezea cover latter, pamoja na kukuhudumia binafsi gharama ni sh elfu 95 za kitanzania na anakuombea kazi sehemu tano tofauti.

Nimeandika hapa kupata ukweli wa hili swala maana Nina mashaka kwa Sababu vijana wengi wanahangaika kupata njia rahisi yenye gharama nafuu ya kwenda ulaya na marekeni kupiga kazi.


Naomba kujua Kama Kuna mwana jf aliyewahi kusaidiwa na huyu jamaa na akaweza kwenda sehemu tajwa kufanya kazi Kama nilivyo elezea.

Nimesoma nyuzi nyingi humu toka mwaka 2016 nilipojiunga na jf Mara ya pili zinazohusiana na kujiripua ughaibuni kutafuta maisha. Kama hii fursa ya jamaa itakuwa kweli Basi Naamini vijana wengi tutatimba ulaya na marekani japo kwa muda mfupi maana jamaa anadai anakufanyia maombi kabla hata ya kupata pasi ya kusafiria.

Nawasilisha mjitokeze kwa wingi kuchangia mada hii.
 
Huyo anakusanya registration fee akikusanya maokoto ya kutosha anawaachia manyonya, wakati mpo kwenye waiting list mnasubiri viza, tena usipoangaliwa unapigwa na viza fee na ya medical examination.

Ulaya hawaendi kwa style hizo na hata Agency wa kazi za udereva ni Uarabuni zaidi.
 
Mbona kama umetapeliwa mkuu. Hiv unaweza kupata kaz bila kuwa na vibali vyakuishi kwanza ulaya? Mi nataman sana wabongo watoke nje ya nchi kwaajili ya exposure lakin warud kufanya kaz hapa nyumban. Nakuhakikishia hakuna sehem rahc kupata hela kama hapa Tanzania. Usiande kupoteza muda bure mkuu komaa hapa utatoboa
 
Vipi hatafutii watu ajira zakuchunga ng'ombe Estonia?

Wewe jamaa unasema umejiunga JF 2016 lakini akili yako imelala.

Unaona kabisa hapo unaibiwa wewe unaleta story "unamfahamu huyu jamaa"

Nani akupatie kazi yakuosha vyomba Amerikkka? Una akili kweli?

Usipoteze muda bora ushike jembe ukalime au kapige kazi ya saidia fundi.
 
Back
Top Bottom