DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 409
- 343
Wanabodi,
Suala la serikali mbalimbali kukopa fedha kwenye taasisi za fedha kama vile benki ya dunia au IMF halijaanza leo na wala halitaisha hivi karibuni. Katika dunia ya sasa, inaaminika kwamba mikopo ni njia mojawapo inayoweza kutumiwa na serikali yoyote katika kuendeleza miradi yake na hatimaye kujikwamua kiuchumi.
Jaribu kufikiria Tanzania iliyopata uhuru mwaka 1961. Huenda Tanzania hii haikuwa na mahusiano ya kutosha na nchi zingine. Mifumo ambayo ingeiwezesha nchi kujiingizia kipato kwa njia ya kodi au kuwezesha matumizi ya rasilimali ili kujikwamua kiuchumi ingehitaji muda ili iwe imara.
Labda mazingira hayo ya kipindi hicho yana ashiria kwamba kujitosa kwenye mikopo ndio njia pekee kwa serikali ambayo haina vitendea kazi vya kutosha kuwa hudumia wananchi wake.
Miaka mingi baadaye, mwaka 2025, Tanzania Imejikuta na deni la trilioni 97 ambalo limethibitishwa na serikali kuwa himilivu. Kauli hii inatokana na wachumi wengi duniani kupendekeza deni la taifa lolote linaloendelea kuwa angalau asilimia 40 ya mapato ya nchi hiyo (GDP). Ingawa deni la taifa linasemekana kuwa himilivu, bado limeongezeka. Kwasababu hiyo ni vyema kujiuliza kama mikopo ya hivi karibuni imetumika zaidi katika shughuli za uwekezaji au imetumika katika kulipia shughuli za kila siku za serikali.
Mifano nitakoyo eleza kuhusu mikopo ambayo serikali imechukua inaweza isitoe picha kamili ila ni mifano inayo onyesha matumizi ambayo labda sio sahihi.
Samia bond (Dola za kimarekani milioni mia tatu) ambayo imelenga kuwezesha ujenzi na ukarabati wa barabara ni mfano wa mkopo uliochukuliwa na serikali kutoka kwa wananchi kwa matumizi ambayo haya imarishi ufanisi wa kazi ya serikali.
Ujenzi wa barabara hizi unaweza kuonekana kama kitu kizuri ila mafanikio haya ni ya muda mfupi tu na kwa kiasi kikubwa haya justify ukopaji wa fedha wa namna hii. Ingawa ingechukua muda mrefu zaidi, uwekezaji kwenye miundombinu unaweza kufanywa na serikali huku ikizingatia umuhimu wa kuishi ndani ya uwezo wake.
Mfano mwingine ni mkopo ambao serikali ilichukua mwaka 2007 kutoka NSSF wa shilingi bilioni 15.9 kwa ajili ya ujenzi wa machinga complex. Miradi huu haukuweza kutatua changamoto za wamachinga na kwasababu hiyo serikali imeshindwa kulipa deni.
Kwa haraka haraka, sidhani kama huu ndio uwekezaji unaoweza kuchochea maendeleo ya kudumu ya kama miaka 20. Kukopa kwa ajili ya shughuli za kawaida za serikali kama vile kulipa mishahara, kufanya shughuli za ujenzi za hapa na pale, na expenditure za kawaida kuna ashiria kukosa mikakati thabiti ya kulipa madeni hayo
Utagundua kwamba mabadiliko yanayoweza kuleta mageuzi makubwa na ya muda mrefu mara nyingi, hayaji na political mileage.