Deni kwa baba mkwe linanisumbua kiasi

Deni kwa baba mkwe linanisumbua kiasi

Mkuu, naomba nikuulize swali la kizushi; mahali ya binti yake uliisha maliza? Sijui unafanya kazi gani but kwa mtu mwenye uwezo wa kununua kifurushi cha internet kudai 80k kwa baba mkwe hiyo ni aibu sana na hapa nahisi kama inatudhalilisha wanaume bwn. Kwanza mkeo kaenda kujifungulia kwao (hiyo ni njia mojawapo ya wewe kukwepa majukumu yako kama baba wa mtoto mpya) halafu still unadai vikosi 8 vya wana msimbazi!? Hapana bwn.
 
Nani ana muhudumia mkeo huko kwao?
Ulipo mpeleka mkeo kwao akajifungue, ulimbebesha na chakula atakacho kuwa anakula?
Alafu mbona hauna msimamo, mara umasamehe hilo Deni mara utake kumdai.
Alafu mbona pesa yenyewe mdogo sana kuliko udhalilishaji ulio mfanyia humu uyo baba mkwe kwa kumtangaza? Angekuwa ni baba yako mzazi ungekuja tueleza hapa ?
 
Huna adabu,baba mkwe ni babako. Mkeo akijua Haya mambo atakuona hudhamini kwao.sahau na tafuta zingine.
 
Nafikiri Wengi Wamekwambia, Ila Kudai Noti Nane, Tena Kwa Ba' Mkwe,. Mwanae Unamgaragaza Kila Siku Mpaka Umemvimbisha Tumbo, Then Unadai (Misimbazi 8) Mwanaume Umetisha...!
 
Hata kama ni laki na themanini, hutakiwi kuidai bwana kwa mkweo wala hata kuigusia. Wewe wa wapi wewe!? Yaani hiyo itoe kabisa kwenye hesabu zako za msingi
 
yalishasemwa humu sana tu eti ukitaka kujua ugumu wa kudai deni kopesha ukweni
 
Mm nategemea id iendane na mtu, kumbee njaa tu ivi kwe elfu 80 si ilibidi umpe ata bila kukuomba? Ndo maana lowasa anachukia umaskini loh
 
Hahahaha walimwengu hawaishi vituko......umempeleka mkeo kwao kula uzazi ulifikiri pale ni kituo cha kulelea wazazi......babamkwe alikosa hela ya mboga akaona aombe kwa dizini ya kukopa
 
hizo samehe baba !
kiendacho kwa baba mkwe ni mahari
lol
 
Back
Top Bottom