Baba mkwe amekopa kwenye kurudisha mkwanja anajisahaulisha. Hii siyo sawa ndugu zanguni

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,510
23,722
Wadau kuna siku nipo nafanya service garage fulani mara na baba mkwe naye akatia team amekuja fanya garage hapo hapo. Wametengeneza mara kuna spare inahitajika na amepungukiwa 190,000.

Akanambia nimwazime 250,000. Nikamwazima. Miezi miwili imekata. Naona amejisahaulisha kabisa. Kila mara namkumbusha kidizaini kwa salamu tu. Naona anajibu kama vile shwari tu. Hagusii kabisa deni.

Sasa mimi nahitaji mkwanja wangu nimeshapeleka watoto shule nahitaji balance hapa home. Nakumbuka hakuomba alisema nimkopeshe. Sasa anajisahaulisha kitu ambacho mi kinanikwaza.

Mimi mtoto wake nililipa mahari cash na sikutaka hata punguzo. So hapa yasije mambo ya baba mkwe ni kama mzee wako. Ndiyo ni kama mzee wangu nami namtreat kama mzee wangu ndo maana nataka kumdai. Mimi hata mdingi huwa tunadaiana vizuri tu Maana alinifundisha dawa la deni ni kulipa tu.

Sasa jana kidogo nimzukie home kwao maana nlikuwa majalala sana but bahati nzuri nikapata ugeni. Ila nawazia leo hii nimfuate ofisini kwake au home. Anipe tu changu.hiyo itanisukuma mpaka tarehe 25.

Nlikuwa naongea na jamaa yangu ananambia eti baba mkwe ni kama mzazi wako hadaiwi. Nikamwambia mi mzazi wangu tunadaiana vizuri tu. Akabadili tena kuwa baba mkwe usimdai. Hapo nikashangaa. Hadi nchi inadaiwa itakuwa baba mkwe?

Sasa nikaona niulize why baba mkwe hatakiwi kudaiwa ikiwa alikopa? Shida ni nini?
 
Mpe muda Mkuu japo watu kama hao kuwapa pesa inabidi uwe na asilimia 50 kwa 50 kwani kuna kulipwa na kutokulipwa pia.

Na pia ndo jifunze kutokumpa mtu kiasi chote anachohitaji yaani hapo ungempa hata nusu yake au hata chini ya hapo nyingine angejua mwenyewe wapi angeipata.
 
Jaribu kuwaza baba mkwe wako naye huwa anapitia hapa JF. Mara lahaula anakutana na hii kitu, unahisi atajisikiaje? Vitu vingine sio poa kuvileta humu. Unaamua kukausha tu. Au unauliza katika namna ambayo mhusika hatajua kuwa anasemwa yeye.
Lala mbele bwana. Tusipangiane maisha. Wewe soma kama inakufaa chukua haikufai achana nayo hujaombwa ushauri wa kindugu. Kujisikia kwake wewe kunakuhusu nini? Atakavyojisikia utamtimizia? Acheni kuingilia issue ambazo haziwahusu kwa kujifanya wajuvi. Akijisikia anataka oa mke mdogo utakubali?
 
Pesa ya nyumbani mtoto wa nyumbani hivyo vyote ni vyenu.

Hesabu hasara ila wakati mwingine toa hela kwenye mambo muhimu kama ugonjwa.
 
Mpe muda Mkuu japo watu kama hao kuwapa pesa inabidi uwe na asilimia 50 kwa 50 kwani kuna kulipwa na kutokulipwa pia.

Na pia ndo jifunze kutokumpa mtu kiasi chote anachohitaji yaani hapo ungempa hata nusu yake au hata chini ya hapo nyingine angejua mwenyewe wapi angeipata.
Nimekumiss
Nje maada
 
Mkuu vitu vingine sio vya kuleta kwenye social media hata kidogo, kama baba mkwe msamehe tuu huna haja ya kutangaza kwenye haraiki ya watu namna hii
 
Kumkopesha nikama kutoa sadaka

Nisawa na kumkopesha baba yako mzazi

Huwezi kudai aslani.

Hesabu maumivu
 
Back
Top Bottom