Deni kwa baba mkwe linanisumbua kiasi

Deni kwa baba mkwe linanisumbua kiasi

Kama umesamehe humu jf unatafuta nini? Halafu wewe unaonekana siye maana baba mkwe akihitaji 80000/- si anamwambia mkewe na mkewe ambaye ni mama mkwe wako anamwambia mkeo halafu mkeo anakwambia unatoa hela unamkabidhi mkeo nae anazipeleka kunako husika. Wewe unauchuna kama kudai atadai mkeo, na kwa sababu umeamua kusamehe hata mkeo akipewa hiyo hela itakuwa yake aendee saluni. Full stop.
 
Ujue watu wana vipato tofauti hivyo kwake 80,000 ni kubwa kwako ni pesa ya salon.

Kwa baba mkwe sio kubwa. Na unaanzaje sasa kumdai baba mkwe? Sio hela kubwa bwana usimtetee...kwani huko kwao mkewe anakaa bure? Kuna gharama pia za kuhudumia mzazi.
 
Naomba mnisaidie hili tatizo wadau.

Siku za hivi karibuni mke wangu nimempeleka kwao kwa ajili ya kujifungua. Katika harakati za kwenda kumsalimia akiwa kwao, Baba mkwe aliniambie nimkopeshe pesa Shl.80,000/ kwa ajili ya kurekebisha mambo fulani.

Imepita muda alioniahidi na bado hajarejesha katika mazungumzo nae niliamua kujikaza/kujipendekeza kwake kwa kumuambia nimemsamehe lakini amekataa katakata.

Sasa nimejikuta niko njia panda maana pesa nazihitaji kumdai siwezi na kujitolea ili nimsamehe nitafute njia nyengine nayo pia anakataa.

Huyu ni mwanaume au mvulana??
Tanzania ina upungufu wa wanaume hakyanani
 
Kwani kumsamehe lazima umwambie? Kunyamaza tu bila kumdai ni kumsamehe tosha! !!
 
Mkuu we mdai tu maana hamna namna aiseeee elfu 80000/=palefu sana ujue
 
Kwa baba mkwe sio kubwa. Na unaanzaje sasa kumdai baba mkwe? Sio hela kubwa bwana usimtetee...kwani huko kwao mkewe anakaa bure? Kuna gharama pia za kuhudumia mzazi.

Kwenye suala la gharama za mzazi actually our minds are coupling i.e. nami nimefikiria hilo na nimekwisha mjibu mhusika. Kwa kifupi wakwe zake wamemuomba fadha kwa ajili ya mkewe na mtoto ki-utu uzima kwani yawezekana bila kuambiwa kukopeshwa asingetoa, halafu sasa asivyokuwa mwepesi kung'amua anadai pesa yake.

Halafu iweje mume umpeleke mkeo akajifungulie kwao wakati ulikwisha kabidhiwa.
 
Hata laki 8 siwezi kumdai baba wa mke wangu asilani.
 
We ni mwehu, kama ulimwambia umemsamehe ina maana ulikusudia ziacha, hata kama kakataa we assume kakubali na mwache mzee wa watu. Inaonekana wewe ni bahili sana na mke wako keshamwambia Babako ndio maana Mzee wa watu hata kama hana kaona wewe ni how come!
 
Kwa baba mkwe sio kubwa. Na unaanzaje sasa kumdai baba mkwe? Sio hela kubwa bwana usimtetee...kwani huko kwao mkewe anakaa bure? Kuna gharama pia za kuhudumia mzazi.

kwa matatizo tuliyonayo wabongo hiyo ela apewe au asipewe bado shida zake zipo palepale hivyo ni bora aziache unless kama ana special dozi ya dawa ambayo akikosa kwa siku mbili ni hatari na hiyo 80000 ndo itamfanya aunganishe dozi kwa kuwa hana hela anayoitegemea zaidi ya hiyo
 
Yaani elfu themanini unataka urudishiwe .Hapo hesabu kuwa umempa na si kumkopesha.Ila umenishangaza sana elfu themanini tena kwa mkweo unataka airudishe tena unasema hadharani.Mh!
 
Ila na wewe 80 ndo unamdai mkwe.....!!!! achana naye....atakuona wa maana kuliko ukimdai.....alikuwa anakuomba alishindwa kukwambia ukweli
 
Back
Top Bottom