KERO Demokrasia, Rushwa na ushiriki wa chama cha siasa kwenye serikali ya wanafunzi - kuna shida Mzumbe!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mmoja wa wanafunzi wa chuo kikuu MZUMBE, Ndaki Kuu (Morogoro).

Nalalamikia namna ambavyo serikali ya wanafunzi, ambayo kwa mujibu wa sheria za Nchi - universities Act, Mzumbe Charter na Katiba ya Serikali ya wanafunzi chuo Kikuu Mzumbe haviruhusu Shughuli ama kufungamana na vyama vya kisiasa chuoni lakini kwa Mzumbe chuo kikuu ni tofauti kabisa; mchakato wa uchaguzi umecheleweshwa kwa makusudi kabisa sababu ikiwa ni baadhi ya viongozi wanaomaliza muda wao na wakuu wa mihimili ya maamuzi ngazi ya serikali ya wanafunzi kubeba ajenda zinazofungamana na ajenda ya chama kimoja kikubwa cha siasa cha kuhakikisha viongozi wa Serikali ya wanafunzi ni wanachama wa chama hicho cha siasa, hali ambayo ni Kinyume cha misingi ya demokrasia na utawala bora kwani watanzania vijana wenye ndoto ya uongozi wanakoswa nafasi hiyo sababu tu hawafungamani na chama hicho cha siasa.

Kwa mujibu wa katiba ya serikali ya Wanafunzi chuo kikuu Mzumbe Tume ya Uchaguzi inapatikana kwa mchakato unaoongozwa na Bunge la wanafunzi, mchakato huu upo kikatiba na ulifanyika kuwapata wajumbe 12 ambao wangeunda Tume huru ya uchaguzi (Katiba haijatoa mamlaka kwa mtu yeyote yule wala chombo chochote ndani ya taasisi au chuoni kuunda tume) lakini, kwa kukiuka katiba na kuendeshwa na mlengo wa chama kimoja cha siasa bodi ya usuluhishi chuoni ambayo miongoni mwa wajumbe wake ni viongozi wa chama hicho cha kisiasa walivunja tume hiyo na kuendelea kuunda tume nyingine pasipo kuwa na mamlaka yoyote kikatiba; suala ambalo ni kinyume na misingi ya haki na utawala bora.

Kwa kutoridhishwa baadhi ya wanafunzi walipinga maamuzi hayo katika ngazi mbali mbali za uongozi chuoni bila kupata msaada wowote bila majibu yakiwa ni uongozi wa chuo hauingilii shughuli za wanafunzi zaidi ya kushauri tu!

Pasi na kusikiliza pande zote mbili zenye mgogoro (Tume ya uchaguzi iliyopatikana Bungeni na Tume iliyoundwa na bodi ya usuluhishi), kiongozi ya chuo (menejimenti) aliamua kutoitambua tume iliyou dwa na Bunge la wanafunzi, chombo chenye mamlaka na kuitambua tume iliyoundwa na tume ya usuluhishi pasi kuwa na mamlaka kisheria kitendo ambacho ni kinyume na misingi ya kimaamuzi na kukanyagwa kama siyo kupuuzwa kwa katiba ya serikali ya wanafunzi chuo kikuu Mzumbe.

IMG-20240523-WA0007.jpg

IMG-20240523-WA0006.jpg
 
Back
Top Bottom