Demokrasia na Maendeleo ndani ya CHADEMA

Demokrasia na Maendeleo ndani ya CHADEMA

kwa mtu timamu hakuna ushahidi uliotolewa ila kwa wewe mchumia tumbo ndo umeuafiki huo ushahidi wa kughushi.

Huyo mme aliposema mshahara wa waziri mkuu pinda ni 26,000,000 mbona hukuomba ushahidi na pale alipo sema mshahara wa kikwete ni mil 32 mbona huku hoji ushahidi...
 
Hata Zitto akisema hagombei Uenyekiti bado mtatafuta visingizio vingine
Mkuu kwa mtazamo wangu, zile allegations ni serious, haziwezi kumalizwa kwa Zitto kutogombea uenyekiti. Tunataka tujue ukweli ni upi.
 
SEHEMU YA KWANZA.
Sote tunajua jinsi Mwl Nyerere alivyopinga mfumo wa vyama vingi mwaka 1965 kwa kusema tunataka kujenga nchi yenye umoja na Mshikamano wa Taifa na baadaye akatofautiana na wenzie akina Kambona,kutoka mwaka 1965 mpaka 1992 ndipo ulikuwa ukomo wa mfumo wa chama kimoja.,Kipindi hicho chote mpiga kura alikuwa anakwenda kwenye Sanduku la Kura kwa kutia tiki kura ya ndiyo au hapana kwenye picha ya mgombea ,mgombea anakuwa mmoja,kama humtaki ,acha.Hivyo ilibana chaguo huru kwa wapiga kura.
Wanaharakati na wadau mbalimbali walipambana na mfumo huu kandamizi kwa muda mrefu na hatimaye tukafanikiwa mwaka 1992,ambapo sasa ukawa ni uhuru wa wananchi kuchagua mgombea wanayemtaka.Lakini mfumo huu haukubadirisha mfumo wa taasisi za Vyama vya Siasa ila ulifanikiwa kuleta vyama vingi vya Siasa ambavyo kila chama kitasimamisha mgombea wake,hivyo kama vyama vipo kumi(10)basi wagombea watakuwa 10.
Wanasiasa ni watu wa ajabu sana,wale wale waliodai kwamba mfumo wa chama kimoja uliwabana,haukuwapa wigo mpana wananchi demokrasia ya Kuchagua,ndio wakawa wanateua jina moja na kulipeleka katika Mkutano mkuu kwa Kupigiwa kura ya ndiyo au hapana.
Ndani ya chama hawaruhusu demokrasia ya wagombea kushindana kuomba kura ya kuchaguliwa,ila nje ya chama wanaomba demokrasia ya kushindana kuchaguliwa.,Vyama vya upinzani ambavyo vilitakiwa kuwa vyakwanza kuasisi demokrasia halisi vimeonekana vikiikwepa demokrasia vilivyoidai.

UCHAGUZI WA 2008 ULIO MWINGIZA MBOWE MADARAKANI KWA AWAMU YA PILI.

Kutokana na Chama kukua,tulifurahia kwamba sasa hatutakwenda nyumbani kwa mtu kumuomba atuongoze,bali tutatangaza nafasi za kuomba uongozi wa kuchaguliwa,watu watachukua fomu,Vikao vya kisheria vitatangaza mfumo mzima wa mwenendo wa uchaguzi,sifa za wagombea,muda wa kampeni na maadili ya kampeni.Hii tuliifurahia sana kwasababu tulitaka tuwaoneshe CCM jinsi uchaguzi unavyoweza kuwa huru na wa Haki.Tulitaka kuionesha Tume ya Uchaguzi Taifa ni jinsi gani unaweza kuendesha Chaguzi kwa uwazi,uhuru na bado ukawa na taasisi Imara.
Tulitaka tutume ujumbe katika Jamii ya kimataifa kwamba CHADEMA ikichukua dora,itaheshimu misingi ya demokrasia,ikiwemo namna tutakavyoendesha chaguzi zetu za nchi,tumpata mwenyekiti wa kitongoji,kijiji,Diwani,Mbunge na Rais kwa mfumo ulio wazi,huru na unaowajibika.Mana tulitaka Kutenda kwa Vitendo tunayoyahubiri na Kuyasimamia.
Tulishangaa ghafula baadala ya kumpongeza aliejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa ili ashindane na Freeman Mbowe ambaye alikuwa anatafuta kipindi cha pili,ikabaki kuwa taharuki ya hofu na wasiwasi juu ya Ujasiri wa Kijana mdogo Zitto Kabwe kugombea nafasi kubwa katika chama namna hiyo na kushindana na Mbowe.
Taharuki hiyo ikaleta maneno machafu Kwa Zitto Kabwe kwa kuonekana hamuheshimu Mbowe,kwanini anaitaka nafasi hiyo wakati Freeman bado hajamalizia kipindi cha pili,Kwanini Zitto asimsubiri Mbowe amalizie Kipindi chake cha Pili.,Wengine wakasema muda huu ni muda wa kujiandaa kuelekea uchaguzi Mkuu 2010,ambapo Kama Chama tunahitaji kwenda kwenye uchaguzi tukiwa hatujagawanyika.
Wazee wa Chama,wakaitwa na Kuwaita Freeman Mbowe na Zitto Kabwe wakiita ni kikao cha Usuruhishi!!!eti Kugombea nafasi ya Uenyekiti ni Mgogoro hivyo ulitakiwa Usuruhishwe na Wazee.
Wakamuomba Zitto Kabwe akubali kumwachia Freeman kipindi cha pili,yeye akiombwa asubiri Freeman akimaliza kipindi chake cha pili.,Basi kutokana na mvutano huo ikabidi Zitto Kabwe akubali kuachia nafasi hiyo ili Wapiga Kura ambao ni Wajumbe wa Mkutano mkuu wakachague Mtu na Kivuli(kura ya ndiyo au Hapana).
Uchaguzi ule ntaukumbuka jinsi ulivyoichafua demokrasia halisi,ningekuwa Freeman Mbowe nisingekubali kushindanishwa na Kivuli,kwani ni heshima kushindanishwa na binadamu mwenzangu kuliko kushindanishwa na Kivuli.
Wanachama tulikubali yaishe,ili tujenge umoja wa uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwan 2010,na Serikali za Mitaa 2009.

SEHEMU YA TATU KAMBI RASIMI YA UPINZANI BUNGENI.

Uchaguzi wa 2009 na 2010 ukawa umekwisha,tayari Freeman Mbowe alikuwa ameshinda uchaguzi jimbo la Hai akiwa Mbunge na Zitto Kabwe alikuwa ameshinda ubunge Kigoma Kaskazini.
Wakati huu,demokrasia ikawa Iinatakiwa kuwakutanisha Wabunge wote wa chadema,ambapo watatakiwa kushindania nafasi ya Ukiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni.
Wanasiasa wawili hawa Zitto Kabwe na Freeman wakaonesha nia ya kuomba kinyang'anyiro hicho cha nafasi ya juu huko bungeni.
Mbinu za kukwepa ushindani ikajirudia tena,Kwa Mwenyekiti wa Chama kusema kwamba bunge letu linafuata mfumo wa jumuiya ya madora,ambapo Kiongozi wa chama anapokuwepo bungeni basi moja kwa moja anakuwa kiongozi bungeni.
Hivyo kwasababu mwenyekiti wa Chama Taifa yupo bungeni basi automatically ndiye atakuwa kiongozi wa Kambi rasimi ya upinzani Bungeni na Naibu Katibu Mkuu utakuwa Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungen.
Vyama vya Upinzani lazima tusitafsiri vibaya misingi ya demokrasia,demokrasia isiwe demokrasia unapotafuta maslahi fulan,halafu ikawa siyo demokrasia unapokuwa una maslahi tayari.

SEHEMU YA NNE.KUELEKEA UCHAGUZI MKUU CHADEMA

Sababu zile zile zilizotumiwa kukwepa wanachama kushindania nafasi za uongozi wa juu wa chama mwaka2008,zinaelekea kuwa sababu hizo hizo zinazotaka kutumiwa kukwepa wanachama kushindania nafasi za juu za uongozi katika chama,kwani sababu zile zilikuwa umamluki wa CCM,Kujenga umoja na Mshikamano wakati huu wa kuelekea uchaguzi Serikali za Mitaa 2014 na Uchaguzi Mkuu.
Wanachama tunatambua thamani ya jukwaa la ushindani,kwamba wanachama wanaomba nafasi wanazoziona wanatosha kuziongoza,Wanachama watachujwa na wapiga kura ambao ni Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa,Watajieleza ni nini Wanataka Kukifanyia chama?,Wamekifanyia nini na maswali mengine Mengi.,Wanachama watawajua nani aliye na hoja za Msingi na Maono ya Kukiongoza Chama.
Haki kubwa kuliko zote zaUanachama wa Mwanachama ni KUWA NA HAKI YA KUFIKIRI,KUAMUA NA KUCHAGUA CHAGUO ALITAKALO PASIPO KUSHINIKIZWA NA MTU.

ANGALIZO MARA BAADA YA UCHAGUZI KATIKA UUNDAJI WA KURUGENZI
Wananchi wanataka Mabadiriko,Hawajaona utayari wa CCM kuwaletea Mabadiriko.,Wanaitegemea CHADEMA ,NCCR na CUF kuwaletea Mabadiriko.
Kwa chadema,Katiba inasema Wakurugenzi wote na Maafisa wa Chama Wataomba nafasi hizo kwa Katibu Mkuu Taifa,baada ya Katibu Mkuu kuteuliwa na Kuidhinishwa na Kamat Kuu,Baraza kuu na Mkutano Mkuu.
Katiba atayawasilisha Majina ya wanao omba nafasi hizo za Ukurugenzi na Uafisa,Kamati kuu itawajadili na Kuamua kwa kura.
Hivyo baada ya Kamati kuu kuamua,ndipo Katibu Mkuu atawaajiri.
WAKURUGENZI WOTE NA MAAFISA WALIOPO,HAKUNA HATA MMOJA ALIYEPITIA MCHAKATO HUO WA KUOMBA NA KUJADILIWA NA KAMATI KUU.
Uenyekiti wa Chama,Ukatibu Mkuu ,Ujumbe wa Kamati Kuu,Baraza Kuu na pengine Mkutano Mkuu ni Katiba na siyo vinginevyo.
Viongozi wetu wa Chadema lazima Muiheshimu Katiba hata kama ni Mbovu,Msipo iheshimu Katiba basi Hamuwezi Kuwaheshimu Wanachama wenu,chama Chenu,Katiba ya nchi na wananchi wenu.
Hatuwezi Kutwaa uongozi wa nchi nje ya Katiba ya Chama na ile ya Nchi,kinyume chake ni uasi.,mkifanya hivyo pia mtaondolewa kwa uasi.

USHAURI KWA CHADEMA.
Kwasasa kuna wimbi kubwa la wanachama na Viongozi wao kupenda kutumia informal communication(Mawasiliano yaliyo nje ya Katiba) hiki ni kiashiria cha kukosekana kwa uhuru wa kutoa maoni ndani ya chama,kama Uhuru upo basi ujue viongozi wetu na wanachama wetu wanaogopa Vitisho,Wanaogopa kuitwa majina mabaya wanayobambikiwa na viongozi wasio penda kusikia ushauri wa kiongozi mwenzie au mwanachama.
Madhara yake ni wimbi kubwa kutoa ushauri kupitia Jamii fourum hivyo Chama kushindwa kupata raslimali adhimu ya mawazo na Mbaya zaidi siri za chama kuwa hadharan.

Ni Mawazo kutoka Kwa Mwanachama na Kiongozi.
Asante.
UHURU WA KWELI,MABADIRIKO YA KWELI.

Umejitahidi kuelezea hasa kuhusu mambo ya uchaguzi. Hata wafanyeje, ZITTO KABWE atashinda tu endapo ataamua kugombea nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Taifa!
 
Mkuu sijakupata vizuri na uzi wako! kwa mujibu wa katiba ya CDM uchaguzi unatakiwa ufanyike 2014 na allowance ya mwaka kama kamati kuu itapendekeza, sasa, 2014 bado, unayajuaje uliyo yaandika? are you a fortune teller?
 
Kwahaya yanayomiminwa hapa jukwaani yanawafanya wanachama wengi wa chadema hata wasiporudisha kadi wanazichoma moto ndani kimyakimya.
Hii ni sawa na mtu mjanja aliyenunua kipande cha dhahabu kufika ndani akakuta kumbe ni fake ili kuficha aibu wasimwone mjinga akaamua kupasua hukohuko ndani na kujuta kwanini amedanganywa.

Haya yanayoendelea yanafanya vijana wengi kukata tamaa, wengi wanachoma kadi zao vyumbani, wengi wamekatishwa tamaa, sasa muelekeo ni kukosa mvuto kama uliokuwepo awali, Tumaini lao linafifia.

Taratibu kama ugonjwa wa Kansa Chadema inakufa.
 
utakufa ww chadema utaiacha
 
Chama cha kilaghai hakiwezi kuruhusu ushindani wa kweli.

Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai...
Hivi uchaguzi wa mwenyekiti wa CCM Taifa uliopita Kikwete alishindana na nani? je CCM hakukuwa na mwenye uwezo wa kugombea nafasi hiyo? Nyie mnajifanya mna Democrasia lakini ni KANDAMIZI ndio kilichomfanya Shibuda ahamie CHADEMA wakati ule.
 
SEHEMU YA KWANZA.
Sote tunajua jinsi Mwl Nyerere alivyopinga mfumo wa vyama vingi mwaka 1965 kwa kusema tunataka kujenga nchi yenye umoja na Mshikamano wa Taifa na baadaye akatofautiana na wenzie akina Kambona,kutoka mwaka 1965 mpaka 1992 ndipo ulikuwa ukomo wa mfumo wa chama kimoja.,Kipindi hicho chote mpiga kura alikuwa anakwenda kwenye Sanduku la Kura kwa kutia tiki kura ya ndiyo au hapana kwenye picha ya mgombea ,mgombea anakuwa mmoja,kama humtaki ,acha.Hivyo ilibana chaguo huru kwa wapiga kura.
Wanaharakati na wadau mbalimbali walipambana na mfumo huu kandamizi kwa muda mrefu na hatimaye tukafanikiwa mwaka 1992,ambapo sasa ukawa ni uhuru wa wananchi kuchagua mgombea wanayemtaka.Lakini mfumo huu haukubadirisha mfumo wa taasisi za Vyama vya Siasa ila ulifanikiwa kuleta vyama vingi vya Siasa ambavyo kila chama kitasimamisha mgombea wake,hivyo kama vyama vipo kumi(10)basi wagombea watakuwa 10.
Wanasiasa ni watu wa ajabu sana,wale wale waliodai kwamba mfumo wa chama kimoja uliwabana,haukuwapa wigo mpana wananchi demokrasia ya Kuchagua,ndio wakawa wanateua jina moja na kulipeleka katika Mkutano mkuu kwa Kupigiwa kura ya ndiyo au hapana.
Ndani ya chama hawaruhusu demokrasia ya wagombea kushindana kuomba kura ya kuchaguliwa,ila nje ya chama wanaomba demokrasia ya kushindana kuchaguliwa.,Vyama vya upinzani ambavyo vilitakiwa kuwa vyakwanza kuasisi demokrasia halisi vimeonekana vikiikwepa demokrasia vilivyoidai.

UCHAGUZI WA 2008 ULIO MWINGIZA MBOWE MADARAKANI KWA AWAMU YA PILI.

Kutokana na Chama kukua,tulifurahia kwamba sasa hatutakwenda nyumbani kwa mtu kumuomba atuongoze,bali tutatangaza nafasi za kuomba uongozi wa kuchaguliwa,watu watachukua fomu,Vikao vya kisheria vitatangaza mfumo mzima wa mwenendo wa uchaguzi,sifa za wagombea,muda wa kampeni na maadili ya kampeni.Hii tuliifurahia sana kwasababu tulitaka tuwaoneshe CCM jinsi uchaguzi unavyoweza kuwa huru na wa Haki.Tulitaka kuionesha Tume ya Uchaguzi Taifa ni jinsi gani unaweza kuendesha Chaguzi kwa uwazi,uhuru na bado ukawa na taasisi Imara.
Tulitaka tutume ujumbe katika Jamii ya kimataifa kwamba CHADEMA ikichukua dora,itaheshimu misingi ya demokrasia,ikiwemo namna tutakavyoendesha chaguzi zetu za nchi,tumpata mwenyekiti wa kitongoji,kijiji,Diwani,Mbunge na Rais kwa mfumo ulio wazi,huru na unaowajibika.Mana tulitaka Kutenda kwa Vitendo tunayoyahubiri na Kuyasimamia.
Tulishangaa ghafula baadala ya kumpongeza aliejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa ili ashindane na Freeman Mbowe ambaye alikuwa anatafuta kipindi cha pili,ikabaki kuwa taharuki ya hofu na wasiwasi juu ya Ujasiri wa Kijana mdogo Zitto Kabwe kugombea nafasi kubwa katika chama namna hiyo na kushindana na Mbowe.
Taharuki hiyo ikaleta maneno machafu Kwa Zitto Kabwe kwa kuonekana hamuheshimu Mbowe,kwanini anaitaka nafasi hiyo wakati Freeman bado hajamalizia kipindi cha pili,Kwanini Zitto asimsubiri Mbowe amalizie Kipindi chake cha Pili.,Wengine wakasema muda huu ni muda wa kujiandaa kuelekea uchaguzi Mkuu 2010,ambapo Kama Chama tunahitaji kwenda kwenye uchaguzi tukiwa hatujagawanyika.
Wazee wa Chama,wakaitwa na Kuwaita Freeman Mbowe na Zitto Kabwe wakiita ni kikao cha Usuruhishi!!!eti Kugombea nafasi ya Uenyekiti ni Mgogoro hivyo ulitakiwa Usuruhishwe na Wazee.
Wakamuomba Zitto Kabwe akubali kumwachia Freeman kipindi cha pili,yeye akiombwa asubiri Freeman akimaliza kipindi chake cha pili.,Basi kutokana na mvutano huo ikabidi Zitto Kabwe akubali kuachia nafasi hiyo ili Wapiga Kura ambao ni Wajumbe wa Mkutano mkuu wakachague Mtu na Kivuli(kura ya ndiyo au Hapana).
Uchaguzi ule ntaukumbuka jinsi ulivyoichafua demokrasia halisi,ningekuwa Freeman Mbowe nisingekubali kushindanishwa na Kivuli,kwani ni heshima kushindanishwa na binadamu mwenzangu kuliko kushindanishwa na Kivuli.
Wanachama tulikubali yaishe,ili tujenge umoja wa uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwan 2010,na Serikali za Mitaa 2009.

SEHEMU YA TATU KAMBI RASIMI YA UPINZANI BUNGENI.

Uchaguzi wa 2009 na 2010 ukawa umekwisha,tayari Freeman Mbowe alikuwa ameshinda uchaguzi jimbo la Hai akiwa Mbunge na Zitto Kabwe alikuwa ameshinda ubunge Kigoma Kaskazini.
Wakati huu,demokrasia ikawa Iinatakiwa kuwakutanisha Wabunge wote wa chadema,ambapo watatakiwa kushindania nafasi ya Ukiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni.
Wanasiasa wawili hawa Zitto Kabwe na Freeman wakaonesha nia ya kuomba kinyang'anyiro hicho cha nafasi ya juu huko bungeni.
Mbinu za kukwepa ushindani ikajirudia tena,Kwa Mwenyekiti wa Chama kusema kwamba bunge letu linafuata mfumo wa jumuiya ya madora,ambapo Kiongozi wa chama anapokuwepo bungeni basi moja kwa moja anakuwa kiongozi bungeni.
Hivyo kwasababu mwenyekiti wa Chama Taifa yupo bungeni basi automatically ndiye atakuwa kiongozi wa Kambi rasimi ya upinzani Bungeni na Naibu Katibu Mkuu utakuwa Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungen.
Vyama vya Upinzani lazima tusitafsiri vibaya misingi ya demokrasia,demokrasia isiwe demokrasia unapotafuta maslahi fulan,halafu ikawa siyo demokrasia unapokuwa una maslahi tayari.

SEHEMU YA NNE.KUELEKEA UCHAGUZI MKUU CHADEMA

Sababu zile zile zilizotumiwa kukwepa wanachama kushindania nafasi za uongozi wa juu wa chama mwaka2008,zinaelekea kuwa sababu hizo hizo zinazotaka kutumiwa kukwepa wanachama kushindania nafasi za juu za uongozi katika chama,kwani sababu zile zilikuwa umamluki wa CCM,Kujenga umoja na Mshikamano wakati huu wa kuelekea uchaguzi Serikali za Mitaa 2014 na Uchaguzi Mkuu.
Wanachama tunatambua thamani ya jukwaa la ushindani,kwamba wanachama wanaomba nafasi wanazoziona wanatosha kuziongoza,Wanachama watachujwa na wapiga kura ambao ni Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa,Watajieleza ni nini Wanataka Kukifanyia chama?,Wamekifanyia nini na maswali mengine Mengi.,Wanachama watawajua nani aliye na hoja za Msingi na Maono ya Kukiongoza Chama.
Haki kubwa kuliko zote zaUanachama wa Mwanachama ni KUWA NA HAKI YA KUFIKIRI,KUAMUA NA KUCHAGUA CHAGUO ALITAKALO PASIPO KUSHINIKIZWA NA MTU.

ANGALIZO MARA BAADA YA UCHAGUZI KATIKA UUNDAJI WA KURUGENZI
Wananchi wanataka Mabadiriko,Hawajaona utayari wa CCM kuwaletea Mabadiriko.,Wanaitegemea CHADEMA ,NCCR na CUF kuwaletea Mabadiriko.
Kwa chadema,Katiba inasema Wakurugenzi wote na Maafisa wa Chama Wataomba nafasi hizo kwa Katibu Mkuu Taifa,baada ya Katibu Mkuu kuteuliwa na Kuidhinishwa na Kamat Kuu,Baraza kuu na Mkutano Mkuu.
Katiba atayawasilisha Majina ya wanao omba nafasi hizo za Ukurugenzi na Uafisa,Kamati kuu itawajadili na Kuamua kwa kura.
Hivyo baada ya Kamati kuu kuamua,ndipo Katibu Mkuu atawaajiri.
WAKURUGENZI WOTE NA MAAFISA WALIOPO,HAKUNA HATA MMOJA ALIYEPITIA MCHAKATO HUO WA KUOMBA NA KUJADILIWA NA KAMATI KUU.
Uenyekiti wa Chama,Ukatibu Mkuu ,Ujumbe wa Kamati Kuu,Baraza Kuu na pengine Mkutano Mkuu ni Katiba na siyo vinginevyo.
Viongozi wetu wa Chadema lazima Muiheshimu Katiba hata kama ni Mbovu,Msipo iheshimu Katiba basi Hamuwezi Kuwaheshimu Wanachama wenu,chama Chenu,Katiba ya nchi na wananchi wenu.
Hatuwezi Kutwaa uongozi wa nchi nje ya Katiba ya Chama na ile ya Nchi,kinyume chake ni uasi.,mkifanya hivyo pia mtaondolewa kwa uasi.

USHAURI KWA CHADEMA.
Kwasasa kuna wimbi kubwa la wanachama na Viongozi wao kupenda kutumia informal communication(Mawasiliano yaliyo nje ya Katiba) hiki ni kiashiria cha kukosekana kwa uhuru wa kutoa maoni ndani ya chama,kama Uhuru upo basi ujue viongozi wetu na wanachama wetu wanaogopa Vitisho,Wanaogopa kuitwa majina mabaya wanayobambikiwa na viongozi wasio penda kusikia ushauri wa kiongozi mwenzie au mwanachama.
Madhara yake ni wimbi kubwa kutoa ushauri kupitia Jamii fourum hivyo Chama kushindwa kupata raslimali adhimu ya mawazo na Mbaya zaidi siri za chama kuwa hadharan.

Ni Mawazo kutoka Kwa Mwanachama na Kiongozi.
Asante.
UHURU WA KWELI,MABADIRIKO YA KWELI.

nakuonea huruma kamanda kama kweli na wewe ni kiongozi wa hili dude chadema,watakuchukunguza,na wakikujua huna chako ndani ya chadema,watakumwigamba!
 
Inapofikia wakati wa kutulazimu kusimama na kuongea ukweli daima lazima tutasimama na kuzungumza ukweli huo pasi na hofu ya kuogopa kutukanwa,kubezwa,kudharauliwa na kupachikwa kila aina ya majina kutoka kwa hao wanaojidai wana hubiri demokrasia.

Siku zote nimekuwa naiduru durusu katiba ya chadema,kitu kikubwa hapo mwanzao kilichokanipelekea niweze kuipa nafasi chadema fikran mwangu hata kabla bado sijaamua kuifatilia kwa undan ni KATIBA YAO,nilipokawa naingalia katiba yao kwa kweli niligundua ina utofauti mkubwa sana na ile ya CCM kwa mambo mengi,ilijpambanua kweli kweli kuwa ni MKOMBOZI HASA WA WATANZANIA,hapo mimi nikaamua kuwatilia maanani na kufatilia siasa zao na kuunga maono yao,hasa lilipokuja suala la UTAWALA WA MAJIMBO NA KUSHUSHA MADARAKA HADI NGAZI YA CHINI KWA WANANCHI,

LAKINI NAONGEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA KABISA NA WATANZANIA WENZANGU NAOMBA MNIZINGATIE,

NAJUA WAPO WATAKAOKUJA NA HOJA ZA KUNIITA LUMUMBA,MKANDA,MKABILA NA MCHOCHEZ LAKINI POTOLEA MBALI MIMI MISIMIMAMO YANGU IKO WAZI HUMU TOKEA NAINGIA KWENYE JUKWAA HILI NA KILA MWENYE FIKRA HURU ANALITAMBUA HILI,NILIAMUA KWA DHATI YANGU KUWA MSHABIKI WA SIASA ZA CHADEMA KWA KUWA NAJUA MIMI ADUI YANGU MKUBWA NI CCM,NA KATIKA CHAMA AMBACHO NIMEAPA KUJA KUTOKUKISAME MILELE DAIMA MAISHANI MWANGU NI CCM,SO NILIAMUA KABISA KUSHABIKIA CDM KWA KUJUA KWAMBA HAWA JAMAA NDIO MWARUBAIN WA KUIDONDOSHA CCM,KWANGU MIMI ILIKUWA LIWALO NA LIWE ILI MRADI CCM IANGUKE MADARAKANI TUANZE UPYA,NA BADO HADI KWA SASA HUO NDIO MSIMAMO WANGU,LAKINI M'BADALA WA HAYO SIWEZ TENA KUAMINI KUWA NI CHADEMA,

KWANIN NASEMA TUSIAMINI NA KUWAPA NAFASI CHADEMA KAMA M'BADALA??

1.Chadema kinajimbanua kuwa hiki ni chama cha demokrasia,mimi niliamin hivyo na watanzania wote tuliamin hivyo,

lakin uhalisia ulivyo hakuna demokrasia ndan ya chama hiko

HUWEZ UKAHUBIRI DEMOKRASIA UKASHINDWA KUWEKA UKOMO WA UONGOZ NDAN YA TAASISI YA KIDEMOKRASIA,UKIULIZA NI KWANIN JIBU LINAKUJA KILA NAFASI NDAN YA UONGOZ WA CHAMA HAINA UKOMO,NA MTU ATAENDELEA KUONGOZA AS LONG AS ANAKUBALIKA NA WENGI NDAN YA CHAMA NA ILI MRADI UONGOZ WAKE NI IMARA NA HAUNA KASORO BASI AENDELEE KUONGOZA CHAMA...!!

HIYO NI DEMOKRASIA GANI??WANA TOFAUTI GANI NA MUSEVENI AU ROBERT MUGABE??KAMA NDAN YA CHAMA HUO NDIO MSIMAMO WAO WAKIPEWA NCHI ITAKUAJE??HILO LA KWANZA,

2.Chadema kimekuwa ni chama kinachopandikiza uhasama baina yake na TAASISI kuu za serikali ambazo ziko imara kulinda usalama wa taifa hili,wanadhan nani atawaamin na kuwapa dhamana ya kuongoza TAIFA ili hali wanapandikza chuki baina ya chama chao na vyombo vya TAIFA??

(A)CHADEMA KILA SIKU INAITUKANA USALAMA WA TAIFA NA KUSEMA NI UMEKUWA KIBARAKA WA CCM,USALAMA WA TAIFA DHAIFU,USALAMA WA TAIFA WEZI,USALAMA WA TAIFA WANASHIRIKIANA NA MAFISADI KUHUMUJUMU TAIFA HILI NA KADHALIKA,

INAWEZEKANA IKAWA NI KWELI,SASA TUKIUWAULIZA USHAHID UKO WAPI JUU YA HAYO ILI TUAMIN HAWANA,SASA UNADHAN WATU HAWA TUKIWAPA NCHI ILI HALI TAASISI NYETIKAMA USALAMA WA TAIFA WAO WANAONA KUWA NI OPPONENT WAO KISIASA TUNAWEZA KUWA SALAMA??HATA KAMA WAO WANAONA HAWARIDHKI NA USALAMA WA TAIFA KWA NIN WASITUMIE NJIA STAHIKI KUZUNGUMZA NAO AU KUWASHITAKI KWA WATANZANIA KWA HOJA NA FACT NA USHAHID BILA KUWAKEJELI NA KUWATUKANA??UNADHAN NA HAO USALAMA WANAWEZA KUWA RADHI NA KUWAPA HAWA CHADEMA RIDHAA YA KUONGOZA TAIFA??

(B)CHADEMA KILA SIKU IKO KWENYE MALUMBANO NA JESHI LA POLISI.

Nakubali jeshi la polisi kuna wakati linaziingua na ni kero kubwa sana ndan ya taifa letu,
Kwa rushwa,kutowajibikia,kupemdelea CCM,kuchukua maamuz ya ukandamizaji na kadhalika,.hata SISI WATU WA KUSINI NI WAHANGA WA JESHI HILO,

Lakini kinachonishangaza ni kwa chadema kuwafanya jeshi hilo kuwa maadui zao wa wazi wazi kias cha kufikia hata kutaman kupigana nalo hasa pale wanapooona linakwena kinyume na matakwa yao,
Jeshi la polisi kama chombo cha serikali katika nch yyte daima wao hutii mamlaka ya serikali iliyoko madarakani,lakin tuseme ukweli kwamba kuna wakati wao kama wanadamu huwa wanachoka na mamlaka hizo na kuwa tayari kwa mabadiliko hasa kwa chama ambacho wanahisi kinaweza kuwa mtetezi wa haki na maslahi yao,sasa chadema kwanin kinajiingiza kwenye malumbano na jeshi hilo na kuacha kuonesha kuwa wao ni mkombozi wao??
Unadhan jeshi la polisi linaweza kuwa radhi kuiona chadema inachukua hatamu za uongozi??hilo haliwezekani hata kidogo...

(C)Na hapa karibun Chadema kilishajionesha kuingia kwenye utata hata na jeshi la wananchi wa tanzania na kusema ni jeshi bovu,jeshi lililoegemea CCM na kuacha kusimama kwenye utaifa na kadhalika,

Ni kweli kabisa,sisi wana kusini ni wahanga wa jeshi hili,na tumepewa vipigo vya kila aina hasa pale tulipoonesha tunasiama kupignia matumiz mazur ya RASIMALI GESI,lakin hatukuwahi kuthubutu kusimama na kulitukana jeshi hilo kwa kuwa tunajua wao pia hupewa AMRI na serikali iliyopo madarakani ambayo,ni ya CCM,

lakini kwa kuwa wao ni wanadamu kama sisi ukweli wanaujua,tunajua kwamba itafikia wakati hata wao wataichoka CCM na kuwa tayari kwa mabadiliko,kwahiyo kama wakiona chama chenye uelekeo ni chadema daima hawawez kuacha kukiunga mkono,lakini cha kushangaza chadema nao wamekuwa ni mahasimu wa jeshi hilo huku wakiamin siku moja wanaweza kuchukua uongozi wa taifa hili na kuilendesha jeshi hilo hilo wanalolitukana,hiyo inaingia vipi akilini??

Just to mention but a few of them hiyo ni katika kuonesha ni kwa namna gani chadema isivyopaswa kuamiminiwa na kupewa TRUST ya moja kwa moja kuongoza TAIFA HILI,
Yani ni watu flan ambao wapo na mission na vision zilizojificha na zisizoeleweka.

3.UKANDA,UDINI NA UKABILA

Mara nyingi ninaposoma katiba ya chadema hakuna sehemu naposoma kuwepo kwa vipengele vinavyohubiri ukanda,udini na ukabila ndan ya chama hiko,
Yan kwa ufupi sio itikadi za chadema kwa katiba yao kutukuza ukanda,udini na ukabila,

Hapo mwazo CUF ilivyokawa ipo juu miaka kadhaa iliyopita CCM ilikuja na propaganda ya udini kwa watanzani,na kusema kwamba chma hiko nii cha waislam na hivyo watanzania tusikiamin kwani kitakuja kuvuruga nchi,wengi tuliamin propaganda zile,na niseme wazi tuh hadi leo wapo wengi wanaziamin propanganda zile tena wengi wao ni wanachadema,

Sio mara moja wala mara mbili mimi nimeshawahi kukejeliwa humu ndan na wanachadema na kuniambia mimi sio chadema,niache kuyananga nanga mambo ya chadema na niende kwa waislam wenzangu CUF,sishangai hilo kwani tunatofautiana mawazo,

Nilirudishe hilo kwa Chadema,CCM wakaja tena na propaganda kama hiyo kwa CHADEMA,
CCM wakasema kwamba CHADEMA ni wakanda,wakabila na wadini,mimi nikawa nalifatilia hilo kwa umakin wa hali ya juu huku nikilinasibisha na propaganda zile za CUF,

Lakini kwa masikitko makubwa mimi naweza kusema kwamba nashawishika kuamin na propaganda zile kuwa ndan ya CHADEMA KUNA SIRI NZITO KUHUSU UKANDA,UDINI NA UKABILA,

KUJIUZULU KWA SAID ARFI NA KUSAKAMWA NA KWA ZITTO KABWE NA KITILA MKUMBO NAKUFANANISHA NA MADHILA YALIYOKAMPATA MAREHEMU CHACHA WANGWE NASHAWISHIKA KUAMINI KUWA KUNA HALI YA UTATA KUHUSU HILO NA AMBAYO INAPASWA KUMULIKIWA TOCHI YENYE MWANGA MKALI,

KATIBA YA CHADEMA HAIHUBIRI UDINI,UKANDA NA UKABILA,

LAKINI TUNAPIMA MAHUSIANO YA CHAMA HIKO NA PHILOSOPHIA HII YA UKANDA,UDINI NA UKABILA TUKIUNGANISHA DOTS TUNAPATA UKAKASI SANA KUAMIN KWAMBA WAO CHADEMA WANAWEZA KUKAA MBALI NA HILO,WENZAO CUF WAMEWEZA KUKAA MBALI NA PROPAGANDA HIYO,WAO NAONA WAMESHINDWA KUIPUNCH NA INAWATAFUNA,

ANGALIA TOP LAEADERSHIP YAO IKOJE,USHAWISH NA WENYE MAMLAKA YA KUATHIRI MAAMUZI NI WATU WA NAMNA GANI??UTAPATA PICHA HALISI,KAMA KWELI WANAHITAJIKA KUKUBAKIKA NA WATANZNIA NI LAZIMA WALIKUBALI HILO NA KUBADILISHA MFUMO WAO WA MAONO NDAN YA CHAMA,KWA SASA HAKUNA WA KUWEZA TENA KUWAAMIN..

Ni Muda tuh pekee ndio utakaowahukumu chadema,na kwa sasa kila mwenye akili timamu anafaham fika kwamba hakuna demokrasia ya dhati ndan ya chama hiko,

Kikubwa kilichopo ni kutumia mwamvuli wa demokrasia na kuwapumbaza wale wasiotambua aina ya siasa wanazozifanya wao chadema.

Watanzania tulio wengi tumeshoshwa moja kwa moja na UTAWALA WA CCM,na tuliamin moja kwa moja CHADEMA ingeweza kuwa M'BADALA SAHIHI WA CCM,lakin kwa masikitko makubwa tumeona ni jins gani chama hiki kilivyotupotezea muda wetu,klivyo vunja matumain yetu na ndoto zetu kwamba ipo siku moja wangekuja kuiangusha CCM na kuiondoa madarakani.,

Wamefeli kusimamia uongoz ndan ya chama,wameshindwa kusimamia demokrasia ndan ya chama,wameshindwa kuwaunganisha wananchi wa makabila mbali mbali,wananchi wa kanda mbali mbali,wananchi wa dini mbali mbali,

Pia Chadema wameshindwa kuziunganisha taasisi nyeti tunazozitegemea watanzania katika kuongoza nchi hii na kuwashawishi kuwa wao tukiwapa ridhaa wanaweza kuongoza taifa hili watawezaje kuchukua dola na kuongoza taifa??

SHUKRANI MUNGU KWA KUTUFUNULIA HILI,NA TUNASHUKURU TUMELIONA KWA WAKATI MUAFAKA...

TEAM ZITTO...
 
Hakuna demokrasia ya kutukana viongozi,kama katiba zitto anajua jinsi utaratibu wa kuibadirisha ulivyo, halafu jifunze kuandika vizuri, au ulipata division five
 
Mkuu hakuna demokrasia isiyokuwa na mipaka! Wahaini hutumia mwanya wa demokrasia kama utawala holela kwa lengo la kupandikiza watu wao... Zitto unamfahamu vizuri?
 
umeandika maelezo mengi lakn pumba tupu.ninapata wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri,SIO KAZI YA USALAMA WA TAIFA KAMA SIO WA CCM KUTUCHAGULIA VIONGOZI.VIONGOZI HUCHAGULIWA NA WATAWALIWA KUPITIA SANDUKU LA KURA.Na hao tiss na vyombo vyote vya usalama walikuwa wapi wakati pesa za EPA,KAGODA ZINAIBIWA? walikuwa wapi wakati mafisadi wanaiba twiga wetu na kuwapeleka uarabuni? biashara ya unga na majangili unataka kutuambia wahusika hawajulikani? wengi wa wanausalama hao unaowakingia kifua wanashirikiana na mafisadi wa ccm kuhujumu taifa huku wewe ukitaka wasisemwe hadharani? leo hii usalama wa taifa umegeuka kuwa uhujumu wa taifa.acha kujifedhehesha kwa vijipropaganda vya kipumbafu.
 
Back
Top Bottom