Asante na nimekuelewa vizuri kabisa.
Kwanza kabisa naomba nikwambie hili kwa usahihi kabisa kwamba Rasimu ya katiba iliyopo kwenye tovuti ya
www.katibampya.com ni pendekezo langu la katiba sio la serikali au la wananchi wote, pia pendekezo hilo haliondoi mchakato rasmi wa katiba. Hivyo basi yale yaliyokuwa humo yachukulie kama ni mchango wangu wa kisomi, kitaaluma na kiraia kwa taifa langu hasa pale nilipozungumzia kuhusu muundo wa dola lenye mihimili minne ya kitaifa, Yaani.
1.
Baraza la Usimamizi wa Taifa (huu ni muhimili wa usimamizi wa misingi yote ya taifa, ndio mamlaka ya kimuungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, mamlaka ya kutoa Tathmini za taifa na muongozo.)
2.
Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania (muhimili wa utendaji, utekelezaji wa sera za taifa, ulinzi na usalama na mengineyo mengi.)
3.
Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania (muhimili wa uwakilishi wa dhamiri mbali mbali za wananchi katika ngazi za majimbo, kutunga sheria, kupitisha bajeti na mengineyo )
4.
Mahakama ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania (muhimili wa utoaji haki, hukumu za kisheria, mtatuzi wa migogoro ya mihimili yote na mengineyo)
Ubora wa muundo huo ni kwamba hile hoja ya serikali tatu, au mbili unatatuliwa kwa kuongeza muhimili wa nne ambao kazi yake si kuunda serikalibali kusimamia misingi yote ya taifa, yaani usawa katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania, yaani kila upande wa muungano upate kilicho sawa, yaani ndio waangalizi wa wapi tumekwama kama taifa, yaani ndio mfano wa refa kwenye mechi za mpira wa miguu au vyovyote.
Pia Rasimu hiyo haijaishia hapo imezungumziq maswala mengine mbali mbali yenye tija kwa taifa letu.
Hivyo basi naomba nikubaliane na wewe kwamba rasimu hiyo ni maoni tu ya mtu mmoja na yanaweza kukubaliwa na wengi au kukatariwa kwa hoja iliyowazi kabisa.
Nikirudi kwenye maswali yako mengine nakumbaliana na wewe kwamba Miaka ya 80 tulikubaliana wote au kundi kubwa la watu kuitaji mfumo wa chama kimoja cha siasa lakini Nyerere hakaona sio sahihi kubaki kwenye chama kimoja. Lakini hoja hii nqomba tufanye hivi. Embu tujaribu kuuliza swali lile lile la zamani kwamba wananchi wanataka mfumo wa chama kimoja au vingi hivi leo kisha tuone majibu yao watasemaje...?
Mimi nadhani 80% watataka vyama vingi na hapa sasa ndipo unapoona kwamba zamani hawakuwa na utandawazi na uelewa wa kina lakini sana shilingi inapinduka. Kwaiyo hoja hile hile na swali lile lile la zamani likiulizwa leo litatoa jibu tofauti na la kushangaza kabisa.
Pia vitu vingine vyote ulivyosema hapo chini naunga mkono kwa ukamilifu isipokuwa tu mimi naona kwamba Tunapaswa kuwa na muhimili wa usimamizi wa misingi ya taifa hili isije kupotea au kuiga mataifa mengine ndio maana Pendekezo langu la mubimili wa nne inapata nguvu pia.
Let's say tuko na ujamaa kama unavyotaka, swali ni je bila kuwepo na mamlaka ya kusimamia misingi huo uoni kwamba wanaweza kuzaliwa wananchama kwenye chama hicho hicho na kuanza kudhoofisha chama chenyewe na msingi wenyewe.? Mfano huu ndio tunaosikia now days kuhusu "
CCM MTANDAO, WAUNI, WABAGAZAJI, N.K",
Kitu tunachobishana
mimi na
wewe ni chepesi sana, kwamba wewe
unataka turudi kwenye misingi bila nyoongeza nyingine yoyote, lakini mimi
nataka turudi kwenye misingi isipokuwa tuwe na muhimili wa usimamizi wa misingi hiyo.
Hivyo basi kurudi kwenye misingi bila kuunda chombo madhubuti cha kuilinda hiyo misingi ni
bahati nasibu, kamali, na kukosa mzizi ya kweli na mwisho
Tust me miaka kumi baadae tutarudi kulalamika tena kwamba turudi kwenye misingi lakini tukiwa na mamlaka yenye kazi hiyo tu.!
malalamiko yanakuwa ni kuikumbusha mamlaka hiyo intende wajibu wake sio kuanza kubishana tena wapi tumekwama.
Mimi nadhani Pendekezo la katiba nililolitoa linaitaji kupewa macho ya kisomi, kitaluma na kiraia na nina imani kuna kitu cha msingi sana kinaweza kulisaidia taifa letu.
Nawasilisha Hoja.
mrxtz2026
Chanzo:
www.katibampya.com