Demokrasia ilobagazwa

Demokrasia ilobagazwa

Ukiniuliza mimi nitasema hivi, Baraza la Wazee litachaguliwa pia na Wananchi. Utaratibu wake - Wataomba fomu kwa kujaza wasifu wao (Elimu, Utumishi n.k), Uanachama wa Chama cha Siasa, hili muhimu liwekwe wazi.

Upatikanaji wao - Kwanza hawatakuwa wengi labda nusu au robo ya idadi ya Wabunge.

Mathalan, Kila Wilaya itachagua Mjumbe mmoja halafu wengine watatoka taasisi muhimu za Kijamii kama tulivyofanya kwenye Bunge la Katiba bila kuwasahau TLS na Haki za Biadamu. Kikubwa ni uwezo wao wa kuhoji (Check and Balance).

Haya ni maoni yangu japo zIpo njia nyingi za kuwapata. Tunaweza pia kuiga nchi nyingine kama Kenya au Marekani wao wamefanyaje..
Bora tuwe na mabunge mawili tu ya uwakilishi kama ilivyo Marekani.
 
Kweli kabisa mambo ni mengi lakini kwanza tukubali Uhalisia tumejikwaa wapi?

Jiulize hivi, ikiwa Katiba ya mwaka 1977 ilifanyiwa marekebisha makubwa mwaka 1984 ikaongezwa Vyama vingi (Demokrasia) na Haki za Binadamu imetokeaje marekebisho hayo, leo hii hayaheshimiwi kabisa?

Iweje kila Sheria ilofanyiwa marekebisho toka 1977 ndio zinakiukwa sana kiasi kwamba unaweza kujiuliza hivi ni Sheria gani ndani ya Katiba hii inayoheshiwa? Wakiapishwa kuilinda wao ndio wanaoivunja. Katiba inasema Binadamu wote ni Sawa! Usawa huo upi?

Kwa hiyo tuna tatizo kubwa zaidi ya tunavyo fikiria, hata tukiandika Katiba Mpya kwa mwendo huu ni kujidaganya na kujitekenya wenyewe.

Tunahitaji muundo wa Serikali ambao Katiba itajieleza wazi wazi Kutenganisha Mihimili yote minne na sii kuonyesha tu shughuli zake bali iseme wazi Mihimili itakuwa HURU na haitaingiliwa na Mihimili mingine kufikia maamuzi yake.

Jambo jingine, kuna pahala huwa nawasikia watu wakisema Rais apunguziwe Madaraka. Sawa! Hayo madaraka ni yapi? utasikia asichague Majaji, Wakurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, na wakuu wengine kwa sababu za Kisiasa zaidi - Sawa kabisa.

Lakini Wananchi wanateseka na nini zaidi tunaposema Rais ana mamlaka makubwa zaidi? Utakuta ni vyombo vya Usalama ndio vinalaumiwa zaidi pamoja na viongozi walipewa dhamana ya kutumikia Wananchi.

Kwenye Usalama wananchi wanateseka na Utekaji, Ukamataji wa watu bila kufuata sheria. Wafungwa kukaa muda mrefu jela bila kufikishwa mahakanani, Migogoro ya ardhi, Mashamba, Utaifishaji wa mifugo, Uhamishaji wa Wananchi bila kulipwa fidia, na hata wakilipwa hailingani na thamani ya ardhi n.k

Yaani adha za wananchi sio kero tena zinajenga chuki baina ya Wananchi na Serikali kwa sababu Utendaji haulinganu kabisa na matakwa ya KATIBA. Tunatokaje hapa ikiwa hali yenyewe ndio hii? Katiba haiheshimiwi wqla haithaminiwi kama kwamba Katiba ni kitabu cha Hadithi..
Sahihi Mkuu, Shida pia ni huu Uchawa pia, Watu ni waoga kusema ukweli,Embe liitwe Embe bila kupepesa Midomo!
 
Kweli kabisa mambo ni mengi lakini kwanza tukubali Uhalisia tumejikwaa wapi?
Jibu: Tumejikwaa kwa kukosa mamlaka ya usimamizi wa misingi ya kitaifa. Binafsi kwa maoni yangu na kile nilichowai kukifanyia tafiti ni kwamba Kwa kukosa mamlaka ya kusimamia misingi ya kitaifa kama vile Misingi ya demokrasia ambayo ni
1. Uchaguzi huru, wazi na haki,
2. Uhuru wa vyombo vya habari
3. Ushiriki wa wananchi n.k

Nimetaka kutaja mambo haya kazaa hili uelewe hiyo misingi ni nayodai ni nini..? Na hapa nimetaja baadhi ya misingi ya demokrasia pekee, kuna misingi mingine kama ya utawala na nineweka haya kama mifano.

Nikijibu kwanini tumekosa mamlaka ya usimamizi wa misingi hiyo na kuchambua hoja yangu ya kitafiti niliyofanya ni kwamba Vyama vya siasa hasa vile vinavyotawala mala nyingi udhoofisha mamlaka za udhibiti au zinazoweka usawa wa kidemokrasia hili waendelee kubaki madarakani. Yaani "Wanatumia dola kubaki kwenye dola",
Hoja kuu kabisa ni kwamba tunapaswa kuwa na muhimili wa nne wenye jukumu hilo la Usimamizi wa misingi ya taifa. Na pendekezo langu la katiba lililopo kwenye tovuti ya www.katibampya.com limetoa jibu la swali hili.

Jiulize hivi, ikiwa Katiba ya mwaka 1977 ilifanyiwa marekebisha makubwa mwaka 1984 ikaongezwa Vyama vingi (Demokrasia) na Haki za Binadamu imetokeaje marekebisho hayo, leo hii hayaheshimiwi kabisa?
Jibu: Masharti hayo hayaheshimiwi kwasababu ya kutokuwepo na mamlaka yenye kusimamia misingi hiyo, yaani kutokuwepo na mamlaka ya uangalizi wa ufuasi wa katiba yenye nguvu za kutoa muongozo, Tathmini na amri pale ulinganifu wa nguvu za kikatiba unapoingia.
Iweje kila Sheria ilofanyiwa marekebisho toka 1977 ndio zinakiukwa sana kiasi kwamba unaweza kujiuliza hivi ni Sheria gani ndani ya Katiba hii inayoheshiwa? Wakiapishwa kuilinda wao ndio wanaoivunja. Katiba inasema Binadamu wote ni Sawa! Usawa huo upi?

Jibu: Kwenye Rasimu ya katiba iliyo kwenye Tovuti tajwa ibara ya 213 imetamka kuhusu "Tume ya haki jinai na usimamizi wa sheria",

Tatizo linalosababisha sheria zisifuatwe ni kutokana kwamba hakuna tume au chombo chenye kusimamia sheria zifuatwe au mwenye kusema kwamba sheria zimevunjwa.

Kwa mujibu wa katiba yenye ya sasa, yaani katiba ya mwaka 1977 haijaweka tume yenye kazi hiyo kabisa na tume iliyokuwepo ni utawala bora na haki za binadamu ambayo yenyewe haikuwekewa mamlaka yake bali imetambulishwa tu kwenye katiba na kuacha kwamba sheria itaweka mamlaka yake na mbaka leo hakuna sheria iliyoweka mamlaka ya maana kuihusu.

Hoja hapa ni kwamba Tanzania kwa sasa inategemea NGO's kama Kituo cha sheria na haki za binadamu ambacho kiuhalisia sio mamlaka ni taasisi ya kiraia inayopokea sehemu ya ruzuku za serikali na haina mamlaka yeyote zaidi wanatoa matamko tu kwamba hatukubaliani na jambo fulani, pia tunategemea taasisi kama TLS zipaze sauti wakati tunapaswa kuwa na Mamlaka ya kitaifa.

Tunahitaji muundo wa Serikali ambao Katiba itajieleza wazi wazi Kutenganisha Mihimili yote minne na sii kuonyesha tu shughuli zake bali iseme wazi Mihimili itakuwa HURU na haitaingiliwa na Mihimili mingine kufikia maamuzi yake.
Jibu: Rasimu ya katiba iliyopo kwenye tovuti tajwa ibara ya 313(14), imetamka wazi kwamba "Mihimili yote inatoka kwa wananchi kama chanzo cha mamlaka zote, itafanya kazi kwa uhuru kamili na kwa utaratibu wa katiba na sheria ", ibara hiyo imeendelea kuweka masharti na kusema "Hakuna muhimili utakaokuwa na uwezo wa kuvunja muhimili mwengine, kuondoa majukumu ya muhimili huo, au kuzuia jambo lilotolewa umamuzi na muhimili huo ispokuwa tu kwa shauri mbele ya mahakama ya katiba".

Jambo jingine, kuna pahala huwa nawasikia watu wakisema Rais apunguziwe Madaraka. Sawa! Hayo madaraka ni yapi? utasikia asichague Majaji, Wakurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, na wakuu wengine kwa sababu za Kisiasa zaidi - Sawa kabisa.

Lakini Wananchi wanateseka na nini zaidi tunaposema Rais ana mamlaka makubwa zaidi? Utakuta ni vyombo vya Usalama ndio vinalaumiwa zaidi pamoja na viongozi walipewa dhamana ya kutumikia Wananchi.

Kwenye Usalama wananchi wanateseka na Utekaji, Ukamataji wa watu bila kufuata sheria. Wafungwa kukaa muda mrefu jela bila kufikishwa mahakanani, Migogoro ya ardhi, Mashamba, Utaifishaji wa mifugo, Uhamishaji wa Wananchi bila kulipwa fidia, na hata wakilipwa hailingani na thamani ya ardhi n.k

Yaani adha za wananchi sio kero tena zinajenga chuki baina ya Wananchi na Serikali kwa sababu Utendaji haulinganu kabisa na matakwa ya KATIBA. Tunatokaje hapa ikiwa hali yenyewe ndio hii? Katiba haiheshimiwi wqla haithaminiwi kama kwamba Katiba ni kitabu cha Hadithi..
Mambo mengine haya yaliyobaki nayqjibu kwa hoja kwamba Rasimu hiyo ya katiba haijapunguzq madaraka ya rais bali imeondoa madaraka ya kumlisha mamlaka yenye maslahi ya kisiasa dhidi yake kwa mantiki kwamba yatatumika vibaya.

Aidha pia mambo mengine yaliyo hapo chini pia yamejibiwa kwa namna mbali mbali unaweza kujisomea.

Rasimu kamili hipo kwenye tovuti ya www.katibampya.com
 
Jibu: Tumejikwaa kwa kukosa mamlaka ya usimamizi wa misingi ya kitaifa. Binafsi kwa maoni yangu na kile nilichowai kukifanyia tafiti ni kwamba Kwa kukosa mamlaka ya kusimamia misingi ya kitaifa kama vile Misingi ya demokrasia ambayo ni
1. Uchaguzi huru, wazi na haki,
2. Uhuru wa vyombo vya habari
3. Ushiriki wa wananchi n.k

Nimetaka kutaja mambo haya kazaa hili uelewe hiyo misingi ni nayodai ni nini..? Na hapa nimetaja baadhi ya misingi ya demokrasia pekee, kuna misingi mingine kama ya utawala na nineweka haya kama mifano.

Nikijibu kwanini tumekosa mamlaka ya usimamizi wa misingi hiyo na kuchambua hoja yangu ya kitafiti niliyofanya ni kwamba Vyama vya siasa hasa vile vinavyotawala mala nyingi udhoofisha mamlaka za udhibiti au zinazoweka usawa wa kidemokrasia hili waendelee kubaki madarakani. Yaani "Wanatumia dola kubaki kwenye dola",
Hoja kuu kabisa ni kwamba tunapaswa kuwa na muhimili wa nne wenye jukumu hilo la Usimamizi wa misingi ya taifa. Na pendekezo langu la katiba lililopo kwenye tovuti ya www.katibampya.com limetoa jibu la swali hili.

Jibu: Masharti hayo hayaheshimiwi kwasababu ya kutokuwepo na mamlaka yenye kusimamia misingi hiyo, yaani kutokuwepo na mamlaka ya uangalizi wa ufuasi wa katiba yenye nguvu za kutoa muongozo, Tathmini na amri pale ulinganifu wa nguvu za kikatiba unapoingia.

Jibu: Kwenye Rasimu ya katiba iliyo kwenye Tovuti tajwa ibara ya 213 imetamka kuhusu "Tume ya haki jinai na usimamizi wa sheria",

Tatizo linalosababisha sheria zisifuatwe ni kutokana kwamba hakuna tume au chombo chenye kusimamia sheria zifuatwe au mwenye kusema kwamba sheria zimevunjwa.

Kwa mujibu wa katiba yenye ya sasa, yaani katiba ya mwaka 1977 haijaweka tume yenye kazi hiyo kabisa na tume iliyokuwepo ni utawala bora na haki za binadamu ambayo yenyewe haikuwekewa mamlaka yake bali imetambulishwa tu kwenye katiba na kuacha kwamba sheria itaweka mamlaka yake na mbaka leo hakuna sheria iliyoweka mamlaka ya maana kuihusu.

Hoja hapa ni kwamba Tanzania kwa sasa inategemea NGO's kama Kituo cha sheria na haki za binadamu ambacho kiuhalisia sio mamlaka ni taasisi ya kiraia inayopokea sehemu ya ruzuku za serikali na haina mamlaka yeyote zaidi wanatoa matamko tu kwamba hatukubaliani na jambo fulani, pia tunategemea taasisi kama TLS zipaze sauti wakati tunapaswa kuwa na Mamlaka ya kitaifa.

Jibu: Rasimu ya katiba iliyopo kwenye tovuti tajwa ibara ya 313(14), imetamka wazi kwamba "Mihimili yote inatoka kwa wananchi kama chanzo cha mamlaka zote, itafanya kazi kwa uhuru kamili na kwa utaratibu wa katiba na sheria ", ibara hiyo imeendelea kuweka masharti na kusema "Hakuna muhimili utakaokuwa na uwezo wa kuvunja muhimili mwengine, kuondoa majukumu ya muhimili huo, au kuzuia jambo lilotolewa umamuzi na muhimili huo ispokuwa tu kwa shauri mbele ya mahakama ya katiba".

Mambo mengine haya yaliyobaki nayqjibu kwa hoja kwamba Rasimu hiyo ya katiba haijapunguzq madaraka ya rais bali imeondoa madaraka ya kumlisha mamlaka yenye maslahi ya kisiasa dhidi yake kwa mantiki kwamba yatatumika vibaya.

Aidha pia mambo mengine yaliyo hapo chini pia yamejibiwa kwa namna mbali mbali unaweza kujisomea.

Rasimu kamili hipo kwenye tovuti ya www.katibampya.com
Niliweka maswala yanayowakabiri wananchi kwa malengo uloyatolea ufafanuzi kwa maana ile ile nilokuwa nikizungumzia Umuhimu wa Muhimili wa nne ambao una mamlaka kamili ya kumuita na kumhoji kiongozi yeyote wa Serikali au mtumishi wa Umma kuhusiana na Ukiukaji wa Sheria, maadam Viongozi wote hawatakuwa na KINGA tena ya kuwalinda wakiwa madarakani.

Kwa hiyo tupo pamoja sana tu. Ni swala la kuelewa shughuli za Mhimili huo. Na kuhusu HAKI za Binadamu tunatakiwa kuwa makini sana juu ya hili maanake siku hizi hawa NGOs na hata taasisi yenyewe wanatetea sana Ushoga kwa sababu wanafadhiliwa na mataifa makubwa yalohalalisha Ushoga na Usagaji.

Ni muhimu sana tu re define HAKI za Binadamu kulingana na mila na Tamaduni zetu. Maadam tuna Mihimili minne hatubitaji tena TUME za rais. Baraza la Wazee ndilo litakuwa Tume yenyewe.
 
Safi sana, kiukweli umegusa jambo zuri sana kuhusu kutafasiri Haki za kibinadamu kulingana na mila na desturi, na hapo jibu lake ni ibara ya 90 ya rasimu yetu ya katiba. Ambayo imezungumza kwamba haki yeyeto inadaiwa kuwa ni ya kibinadamu na haikuwekwa kwenye orodha ya SURA YA PILI ya katiba hii, haki hiyo itaangaliwa asili yake na endapo itakosa ushaidi wa kisayansi, au kwamba haiendani na mila na Tamaduni za taifa letu. Haki hiyo haitotumika ndani ya jamhuri ya muungano wa tanzania.

Ibara hiyo na ibara ya 91 ndizo zinazofunga kila kitu kuhusu madai ya haki za kibinadamu.
 
Back
Top Bottom