Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 12,980
- 11,561
Tulipopata uhuru mwaka 1961 Tanganyika ilikuwa na madaktari 16, mhandisi mmoja na wanasheria wawili. Hatukuwa na Chuo Kikuu. Chuo cha Dar es Salaam kilianzishwa Lumumba kikiwa na faculty ya sheria peke yake na kilikuwa kwenye jengo moja. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilianzishwa rasmi mwaka 1970. Faculty ya Uhandisi ilianzishwa mwaka 1973. Waliokuwa wanasimamia PWD walikuwa ni mafundi mchundo ambao tulikuwa tunawaita wahandisi. Mafundi walikuwa wanafanya trade test maana hakukuwa na Veta. Hamna mtu aliyesema kuwa ili uwe msomi ni lazima upitie Veta. Veta ni nia tu nyingine ya kukuongezea ujuzi.Mkuu; hizo degrees au tuseme hatujaanza kuwa na wasomi leo. Wasomi wamekuwepo toka kitambo na waliajiriwa bila kwenda veta. au nadanganya bro?
Ndipo walipokosea. Ni kama vile ambavyo walio kosa nafasi ya kwenda high schoolna hawakufanya vizuri ndio waliopelekwa kufundisha praimari. Sasa hivi tumeanza kujirekebisha na mitaala ya Veta imepanuliwa ili kuweza kuudumia kila aina ya watu.Veta ilitumika sana kwa vijana Std 7 ambao hawakubahatika kuendelea na masomo Sekondari, vijana F4 ambao hawakufaulu kuendelea na masomo A-level au vijana waliokatiza masomo yao kwa sababu fulani.
Hamna mtu anaewakweza. Tatizo ni kuwa baadhi yao wanadhani kusoma Veta ni kujishushia heshima. Kwa kufanya hivyo wanashindwa kuona nafasi ambazo zingeweza kuwasaidia kupata kile ambacho hawana. Kuna wakati wavulana walikuwa wanaona kazi ya unesi ni kujidhalilisha na ni ya wanawake. Leo wengi tuu wanaikubali.Sasa unapowaelekeza (kwa ushauri au agizo -whatever) wale waliokwishapita A-level na kumaliza chuo wafanye U-turn waende VETA huoni ni kama unawadhalilisha? Yan mheshimiwa anataka kusema hao vijana wasomi walikuwa vipofu (walijizima data/walijitoa ufahamu) hawakuiona VETA walipokuwa wanajiunga vyuoni???
Daktari akitaka kuingia kwenye biashara ya mabasi anaweza kwenda Veta kujifunza udereva makini au hata ufundi mekanika. Mhandisi anaetaka kuingia kwenye biashara ya kilimo bora anaweza kwenda Veta kujifunza ukulima makini. Au akiwa anapenda kupika na anataka kuanzisha mgahawa anaweza kwenda Veta kujifunza mambo ya professional cooking. Au mtu ambae amechoka kupigwa na mafundi wa mitaani kwa sababu hajui hata namna ya kubalisha oil, anaweza kupata ujuzi huo Veta. Sio sawa kabisa na kumtaka daktari aende kujifunza baiolojia. Veta ni sehemu ya kujenga skills ambazo mtu atadhani anahitaji kwa sababu zake mwenyewe. Hamna atakaelazimishwa kwenda Veta.Ujuzi wa kiwango cha juu ni ule unaopatikana kutokana na uzoefu(Field Experiance) kazini. Huko VETA ni mojawapo ya maeneo ya kujifunzia na kutoa cheti kuthibitisha umejifunzia wapi Utaalam wako. Vyuo vya VETA ni kama vyuo vingine ila ni chuo kwa kada za awali.
Kumwambia deg. holder aende veta ni sawa na kumwambia daktari arudi O-level akajifunze biology. Hiyo sio poa.
Amandla...