johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,968
- 141,976
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Mtama ( Lindi vijijini) na mkurugenzi wa umwagiliaji kanda ya kusini wametakiwa kuripoti ofisini kwa waziri mkuu kesho asubuhi bila kukosa.
Viongozi hao walitakiwa kuwepo kwenye msafara wa waziri mkuu alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa scheme ya umwagiliaji pale Mtama unaogharimu zaidi ya sh milioni 700.
Imeelezwa kuwa zaidi ya sh milioni 400 zimeshatumika lakini katika eneo la mradi hakuna kilichofanyika. Ndipo mh Majaliwa akawaita DED na boss wa umwagiliaji ili watoe maelezo lakini wote wawili hawakuwepo na simu zao zilikuwa zimezimwa.
Ndipo waziri mkuu akaagiza watafutwe na wamfuate uwanja wa ndege na wasipomuwahi basi wamfuate Dsm kesho asubuhi.
Hadi waziri mkuu anaondoka wakurugenzi hao walikuwa hawajafika na simu zao hazikupatikana, ndipo mh Majaliwa akarudia maagizo yake kuwa wamfuate Dsm kesho asubuhi bila kukosa vinginevyo atachukua maamuzi tarajiwa.
Source Channel ten !