DED wa Itigi: Ninapakaziwa kesi ya mauaji

Singida. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, Pius Luhende anayedaiwa kuhusika na mauaji ya Isaka Petro (28) amezungumza na Mwananchi akisema “nimepakaziwa tu.”

Luhende alitoa kauli hiyo baada ya mwandishi wetu kumtembelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida alikolazwa tangu Jumanne wiki hii baada ya kupewa rufaa kutoka Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.

Kwa mujibu wa mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Ng’hungu Kuzenza, Luhende anasumbuliwa na pumu (asthma) na mapigo ya moyo.

Mkurugenzi huyo ni miongoni mwa watu saba wanaoshikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo yaliyotokea Jumamosi iliyopita katika Kanisa la Wasabato Kijiji cha Kazikazi mkoani humo.

Inaelezwa kuwa mauaji hayo yalitokea baada ya Luhende kuwafuata watuhumiwa wa kosa la kuharibu mali ya mlalamikaji Rose Andrew aliyedai kuharibiwa mali yake iliyopo ndani ya shamba la Tanganyika Packers linalomilikiwa na halmashauri hiyo.

Taarifa ya Polisi inasema kuwa Luhende alipoingia ndani ya kanisa hilo ilitokea vurugu na akaamua kutoka nje kabla ya askari wanyamapori waliokuwa na silaha kufyatua risasi kadhaa na moja ikampiga Isaka na kufariki dunia papo hapo.

Hata hivyo, waumini waliokuwepo katika kanisa hilo wakati mauaji hayo yakitokea walizungumza na Mwananchi na kupingana na polisi wakisema kuwa mkurugenzi huyo ndiye alimfyatulia risasi Isaka.

Luhende ambaye alikuwa akilindwa na askari kanzu wanne wodini alisema bado kifua kinambana mara kwa mara hasa nyakati za usiku.

“Hata hivyo, namshukuru Mungu kwa kunipigania naendelea vizuri kuliko nilipokuwa hospitali ya Manyoni,” alisema Luhende ambaye alikuwa amejilaza kitandani huku mikononi akiwa hajafungwa pingu.

Katika maelezo yake, mkurugenzi huyo alisema amepakaziwa bila kufafanua zaidi kuhusu kauli yake hiyo.

Awali, Dk Kuzenza alisema mkurugenzi huyo alipofikishwa hospitalini hapo alikuwa na hali mbaya akibanwa kifua na tatizo la mapigo ya moyo.

“Tulipompokea alikuwa na hali mbaya kutokana na kubanwa mara kwa mara na kifua. Kwa upande wa mapigo ya moyo tatizo hilo lilianza kupungua. Kwa sasa tatizo la presha tumelidhibiti kiasi cha kutosha,” alisema. Alisema hata tatizo la asthma limeanza kupungua na kwamba atakuwa chini ya uangalizi hadi keshokutwa, “tukijiridhisha kuwa hali yake imeimarika, tutamruhusu kuondoka.”

Wakati huohuo, kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Isaya Mbughi amesema bado wanaendelea kukamilisha hatua za kisheria kabla watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani.

Alisema taratibu hizo zikishakamilika, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili. “Luhende endapo atakuwa ameruhusiwa kutoka hospitalini tutamuunganisha,” alisema kamanda huyo.

Juzi, kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike alisema “hatujawapeleka mahakamani, bado kuna taratibu nyingine hazijakamilika, kwa sasa tunaandaa taarifa ya kumpelekea mwendesha mashtaka wa Serikali ambaye ataandaa taratibu za kuwafikisha mahakamani.”

Mgogoro wa ushuru wa mashamba katika mbuga ya Kitongoji cha Boma la kati unatajwa kuwa ndiyo chanzo cha tukio kwani halmashauri inasema mashamba hayo ambayo awali yalikuwa yakimilikiwa na Tanganyika Packers ni sehemu yao.

Chanzo: Mwananchi
Huyu itakuwa kacheza dili alazwe hapo hospital asiende mahabusu huko akijaribu kucheza na upelelezi, apelekwe gerezani aachane na hizo juice na nyama anazokula akiwa katulia kitandani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu ukifuatilia kwa makini maelezo ya huyu DED ,tabia zake, maelezo ya polisi na mganga mfawidhi na waumini utabaini DED ndo kaua! swali ni je alikuwa na pumu kabla? kazi amesimamishwa au bado
Hapo hakuna cha pumu wala presha ni mazingiraa tu asikae lupango wao wanapenda kuweka wenzao kumbe wao waoga mkuki kwa nguruwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Singida. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, Pius Luhende anayedaiwa kuhusika na mauaji ya Isaka Petro (28) amezungumza na Mwananchi akisema “nimepakaziwa tu.”

Luhende alitoa kauli hiyo baada ya mwandishi wetu kumtembelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida alikolazwa tangu Jumanne wiki hii baada ya kupewa rufaa kutoka Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.

Kwa mujibu wa mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Ng’hungu Kuzenza, Luhende anasumbuliwa na pumu (asthma) na mapigo ya moyo.

Mkurugenzi huyo ni miongoni mwa watu saba wanaoshikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo yaliyotokea Jumamosi iliyopita katika Kanisa la Wasabato Kijiji cha Kazikazi mkoani humo.

Inaelezwa kuwa mauaji hayo yalitokea baada ya Luhende kuwafuata watuhumiwa wa kosa la kuharibu mali ya mlalamikaji Rose Andrew aliyedai kuharibiwa mali yake iliyopo ndani ya shamba la Tanganyika Packers linalomilikiwa na halmashauri hiyo.

Taarifa ya Polisi inasema kuwa Luhende alipoingia ndani ya kanisa hilo ilitokea vurugu na akaamua kutoka nje kabla ya askari wanyamapori waliokuwa na silaha kufyatua risasi kadhaa na moja ikampiga Isaka na kufariki dunia papo hapo.

Hata hivyo, waumini waliokuwepo katika kanisa hilo wakati mauaji hayo yakitokea walizungumza na Mwananchi na kupingana na polisi wakisema kuwa mkurugenzi huyo ndiye alimfyatulia risasi Isaka.

Luhende ambaye alikuwa akilindwa na askari kanzu wanne wodini alisema bado kifua kinambana mara kwa mara hasa nyakati za usiku.

“Hata hivyo, namshukuru Mungu kwa kunipigania naendelea vizuri kuliko nilipokuwa hospitali ya Manyoni,” alisema Luhende ambaye alikuwa amejilaza kitandani huku mikononi akiwa hajafungwa pingu.

Katika maelezo yake, mkurugenzi huyo alisema amepakaziwa bila kufafanua zaidi kuhusu kauli yake hiyo.

Awali, Dk Kuzenza alisema mkurugenzi huyo alipofikishwa hospitalini hapo alikuwa na hali mbaya akibanwa kifua na tatizo la mapigo ya moyo.

“Tulipompokea alikuwa na hali mbaya kutokana na kubanwa mara kwa mara na kifua. Kwa upande wa mapigo ya moyo tatizo hilo lilianza kupungua. Kwa sasa tatizo la presha tumelidhibiti kiasi cha kutosha,” alisema. Alisema hata tatizo la asthma limeanza kupungua na kwamba atakuwa chini ya uangalizi hadi keshokutwa, “tukijiridhisha kuwa hali yake imeimarika, tutamruhusu kuondoka.”

Wakati huohuo, kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Isaya Mbughi amesema bado wanaendelea kukamilisha hatua za kisheria kabla watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani.

Alisema taratibu hizo zikishakamilika, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili. “Luhende endapo atakuwa ameruhusiwa kutoka hospitalini tutamuunganisha,” alisema kamanda huyo.

Juzi, kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike alisema “hatujawapeleka mahakamani, bado kuna taratibu nyingine hazijakamilika, kwa sasa tunaandaa taarifa ya kumpelekea mwendesha mashtaka wa Serikali ambaye ataandaa taratibu za kuwafikisha mahakamani.”

Mgogoro wa ushuru wa mashamba katika mbuga ya Kitongoji cha Boma la kati unatajwa kuwa ndiyo chanzo cha tukio kwani halmashauri inasema mashamba hayo ambayo awali yalikuwa yakimilikiwa na Tanganyika Packers ni sehemu yao.

Chanzo: Mwananchi
Hata hivyo, namshukuru Mungu kwa kunipigania naendelea vizuri kuliko nilipokuwa hospitali ya Manyoni,” alisema Luhende ambaye alikuwa amejilaza kitandani huku mikononi akiwa hajafungwa pingu.

Huyu mungu mambo Mengi tunamsingizia...yaani umeingia kwenye nyumba ya ibada kwa fujo na silaha bila heshma na adabu,umeua aliyekua anaomba mungu then eti mungu anakupigania!!wewe kiongozi kweli?!aibu kwako....hata kama unalindwa na dola mungu atakuhukumu tu....hapa hapa duniani leo hii yupo wapi Ditopile?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes Yeye Atakuwa ama Shahidi upande wa Jamhuri Au Mtuhumiwa wa Mauaji!

Ila nimeshangazwa msiba kufanywa haraka sina Hakika Kama Postmoterm ilifanyika

Hiki tukio linanikumbusha tukio la Swahiba wangu Almarhuum Ukiwaona Ramadhan Mwinshehe Ditopile wa Mzuzuri ambae Kesi ile ilimnyima raha Pamoja Na kufarijiwa Sana Na Utawala Pamoja Na Ndugu wa Yule Dereva mpaka akazidiwa Na Msongo wa Mawazo Na Pressure Na hatimae akafariki Hotelini Morogoro

Kesi Za Mauaji zinasononesha Sana moyo Kuliko Za Ufisadi
Allah atuepushe Na vizazi vyetu mkosi huu wa kutoa nafsi ya Kiumbe pasi Na haki
ameen
 
Muongo mkubwa huyo!!! Alienda kufanya nini kanisani tena wameingia ndani ya kanisa!!!! That is blasphemy!!!!! Kufuru kubwa hiyo. Lupango inamgonja labda aokolewe na polisi maana naona washaanza kumokoa!!!!
 
Hata hivyo, namshukuru Mungu kwa kunipigania naendelea vizuri kuliko nilipokuwa hospitali ya Manyoni,” alisema Luhende ambaye alikuwa amejilaza kitandani huku mikononi akiwa hajafungwa pingu.

Huyu mungu mambo Mengi tunamsingizia...yaani umeingia kwenye nyumba ya ibada kwa fujo na silaha bila heshma na adabu,umeua aliyekua anaomba mungu then eti mungu anakupigania!!wewe kiongozi kweli?!aibu kwako....hata kama unalindwa na dola mungu atakuhukumu tu....hapa hapa duniani leo hii yupo wapi Ditopile?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanasahau sana hawa viongozi. Watatuonea wananchi lakini Mungu anaona. Dito yuko wapi? Umetukumbusha vizuri sana.
 
Yes Yeye Atakuwa ama Shahidi upande wa Jamhuri Au Mtuhumiwa wa Mauaji!

Ila nimeshangazwa msiba kufanywa haraka sina Hakika Kama Postmoterm ilifanyika

Hiki tukio linanikumbusha tukio la Swahiba wangu Almarhuum Ukiwaona Ramadhan Mwinshehe Ditopile wa Mzuzuri ambae Kesi ile ilimnyima raha Pamoja Na kufarijiwa Sana Na Utawala Pamoja Na Ndugu wa Yule Dereva mpaka akazidiwa Na Msongo wa Mawazo Na Pressure Na hatimae akafariki Hotelini Morogoro

Kesi Za Mauaji zinasononesha Sana moyo Kuliko Za Ufisadi
Allah atuepushe Na vizazi vyetu mkosi huu wa kutoa nafsi ya Kiumbe pasi Na haki
Si unaona na yeye mara pumu mara pressure!!! Huu ndiyo mwanzo. Alivyotoa amri alidhani kuna ngedere kanisani wanakula mahindi.Na bado!!!! Atatapatapa sana ila cha moto atakiona hata akiokolewa na dola.
 
Umeua acha kupindapinda stori
Ukikosa adhabu ya mwanadamu hakika Mungu atakuhukumu vibaya
Umemwaga damu kwenye nyumba ya Bwana nyumba ya kumwabudu
Ghorika inakujia tubu uwe na amani na Mungu wako
Umetengeneza laana ya vizazi vinne
'Nitakuangamiza wewe na uzao wako AsemanBwana wa Majeshi ambaye ni Mungu wa wote!
 
Kumtia Hatiani Mtu Kwenye kesi ya Jinai ya Mauaji sio jambo jepesi Kama kumtia Mtu hatiani kwa kusimama Na gari Kwenye Zebra

Risasi ikiyotumika Kwenye mauaji imepatikana?
DED ana miliki Silaha Na jee hiyo Silaha ina uhusiano Na Risasi iliyotumika?

Huyo Afisa Wanyamapori alikuwa Na Silaha ambayo inaweza kushabihiana Na Risasi iliyotumika?

Hukumu Za Mauaji hazitegemei Msimamo wa wengi Au matakwa ya wengi bali facts tupu
Simjui DED wala simjui huyo Afisa Wanyamapori lakin Ni dhambi kubwa kumsingizia Au kumuonea Mtu kwa Jinai Za aina hiyo

Tunapo urgue tusiingizie Mapenzi Au Chuki zetu Za Kisiasa Kwenye kuhukumu kesi hii
kumiliki silaha au kupatikana kwa risasi iliyoua sio ishu ya muhimu hapa, ingekuwa na umuhimu endapo mauaji yangekuwa yalifanyika halafu mwili ukaja onekana baadae bila ya mtu mwingine kuwepo eneo la tukio, sasa kwa mazingira ya watu wengi hivyo walioliona tukio na wakawa tayari kutoa ushahidi wa ilivyokuwa, kitachothibitishwa ni nia na utndekaji wa tukio, mchezo utaisha hapo.
 
Si unaona na yeye mara pumu mara pressure!!! Huu ndiyo mwanzo. Alivyotoa amri alidhani kuna ngedere kanisani wanakula mahindi.Na bado!!!! Atatapatapa sana ila cha moto atakiona hata akiokolewa na dola.

Hajatoa amri, aliua.

Hizi za eti alitoa amri ni conspiracies za kumlinda.
 
....ivi ameugua ghafla baada ya kushiriki tukio hilooo AMA ALIKUWA NA HISTORIA YA Kuuuguaaa? its only in african context ---TZ where mtuhumiwa hujitetea kwamba anaumwaa kumbe ni JANJA JANJAA tu....ila ka ni kweli alishika bunduki na kumwaga damu hakika DAMU YA MAREHEMU vyamliliaaa.

..Lakini pia mekuwa nikijiuliza walishindwa mchukua na kumweka chini ya vyombo vya ulinzi na usalaam, AMA LIPO JAMBO lafichwa huenda lipo jambo kubwa zaidi ambalo marehemu analijua ama AMELIFANYA na lingeleta ukakas zaidi,
 
Kumtia Hatiani Mtu Kwenye kesi ya Jinai ya Mauaji sio jambo jepesi Kama kumtia Mtu hatiani kwa kusimama Na gari Kwenye Zebra

Risasi ikiyotumika Kwenye mauaji imepatikana?
DED ana miliki Silaha Na jee hiyo Silaha ina uhusiano Na Risasi iliyotumika?

Huyo Afisa Wanyamapori alikuwa Na Silaha ambayo inaweza kushabihiana Na Risasi iliyotumika?

Hukumu Za Mauaji hazitegemei Msimamo wa wengi Au matakwa ya wengi bali facts tupu
Simjui DED wala simjui huyo Afisa Wanyamapori lakin Ni dhambi kubwa kumsingizia Au kumuonea Mtu kwa Jinai Za aina hiyo

Tunapo urgue tusiingizie Mapenzi Au Chuki zetu Za Kisiasa Kwenye kuhukumu kesi hii
Acha kutetea unyama wa hao wanyama wauaji, unawezaje kwenda kanisani kufanya fujo? hao walidhamilia wote wanakesi ya kujibu, huwezi ingia kanisani kumkamata mtuhumiwa wa uharibifu wa mali utadhani ni gaidi
 
Kuna watu waliisha elewa mchezo utaishahe, sio kwa kutabiria bali waliongea facts kabisa kuwa jamaa hapo kesi itazungushwa kuwa hahusiki
Yaani jamaa kauwawa mbele ya watu tena kweupeee na watu wakiwa wakiomba na baba mzazi kasema alishuhudia jamaa akiuwa.

Kweli mnyonge hana haki Africa

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
huyu afungwe tu iwe mfano, kwan mpk anaenda kumfata mhusika kanisani inamaana hakuna mamlaka zinazohusika? au hilo shamba ni mwanahisa humo mpk aende yy na sio mwenyeshamba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu waliisha elewa mchezo utaishahe, sio kwa kutabiria bali waliongea facts kabisa kuwa jamaa hapo kesi itazungushwa kuwa hahusiki
Yaani jamaa kauwawa mbele ya watu tena kweupeee na watu wakiwa wakiomba na baba mzazi kasema alishuhudia jamaa akiuwa.

Kweli mnyonge hana haki Africa

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
Jitu kma hili lilitakiwa nalo lipigwe mawe palepale
 
Kweli hii imekaa vibaya,utashangaa utapoambiwa maganda ya risasi hayajaonekana,sasa namba tunaisoma wote
 
Back
Top Bottom