DED wa Itigi: Ninapakaziwa kesi ya mauaji

DED wa Itigi: Ninapakaziwa kesi ya mauaji

Singida. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, Pius Luhende anayedaiwa kuhusika na mauaji ya Isaka Petro (28) amezungumza na Mwananchi akisema “nimepakaziwa tu.”

Luhende alitoa kauli hiyo baada ya mwandishi wetu kumtembelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida alikolazwa tangu Jumanne wiki hii baada ya kupewa rufaa kutoka Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.

Kwa mujibu wa mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Ng’hungu Kuzenza, Luhende anasumbuliwa na pumu (asthma) na mapigo ya moyo.

Mkurugenzi huyo ni miongoni mwa watu saba wanaoshikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo yaliyotokea Jumamosi iliyopita katika Kanisa la Wasabato Kijiji cha Kazikazi mkoani humo.

Inaelezwa kuwa mauaji hayo yalitokea baada ya Luhende kuwafuata watuhumiwa wa kosa la kuharibu mali ya mlalamikaji Rose Andrew aliyedai kuharibiwa mali yake iliyopo ndani ya shamba la Tanganyika Packers linalomilikiwa na halmashauri hiyo.

Taarifa ya Polisi inasema kuwa Luhende alipoingia ndani ya kanisa hilo ilitokea vurugu na akaamua kutoka nje kabla ya askari wanyamapori waliokuwa na silaha kufyatua risasi kadhaa na moja ikampiga Isaka na kufariki dunia papo hapo.

Hata hivyo, waumini waliokuwepo katika kanisa hilo wakati mauaji hayo yakitokea walizungumza na Mwananchi na kupingana na polisi wakisema kuwa mkurugenzi huyo ndiye alimfyatulia risasi Isaka.

Luhende ambaye alikuwa akilindwa na askari kanzu wanne wodini alisema bado kifua kinambana mara kwa mara hasa nyakati za usiku.

“Hata hivyo, namshukuru Mungu kwa kunipigania naendelea vizuri kuliko nilipokuwa hospitali ya Manyoni,” alisema Luhende ambaye alikuwa amejilaza kitandani huku mikononi akiwa hajafungwa pingu.

Katika maelezo yake, mkurugenzi huyo alisema amepakaziwa bila kufafanua zaidi kuhusu kauli yake hiyo.

Awali, Dk Kuzenza alisema mkurugenzi huyo alipofikishwa hospitalini hapo alikuwa na hali mbaya akibanwa kifua na tatizo la mapigo ya moyo.

“Tulipompokea alikuwa na hali mbaya kutokana na kubanwa mara kwa mara na kifua. Kwa upande wa mapigo ya moyo tatizo hilo lilianza kupungua. Kwa sasa tatizo la presha tumelidhibiti kiasi cha kutosha,” alisema. Alisema hata tatizo la asthma limeanza kupungua na kwamba atakuwa chini ya uangalizi hadi keshokutwa, “tukijiridhisha kuwa hali yake imeimarika, tutamruhusu kuondoka.”

Wakati huohuo, kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Isaya Mbughi amesema bado wanaendelea kukamilisha hatua za kisheria kabla watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani.

Alisema taratibu hizo zikishakamilika, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili. “Luhende endapo atakuwa ameruhusiwa kutoka hospitalini tutamuunganisha,” alisema kamanda huyo.

Juzi, kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike alisema “hatujawapeleka mahakamani, bado kuna taratibu nyingine hazijakamilika, kwa sasa tunaandaa taarifa ya kumpelekea mwendesha mashtaka wa Serikali ambaye ataandaa taratibu za kuwafikisha mahakamani.”

Mgogoro wa ushuru wa mashamba katika mbuga ya Kitongoji cha Boma la kati unatajwa kuwa ndiyo chanzo cha tukio kwani halmashauri inasema mashamba hayo ambayo awali yalikuwa yakimilikiwa na Tanganyika Packers ni sehemu yao.

Chanzo: Mwananchi
kwanini alienda sehemu ya kufanya ibada na kuingia ndani na kuleta vurugu akijua kabisa yeye ni kiongozi na juzi tu hapa Rais ametoka kuongea na viongozi wa dini na kusema kuwa ni vizuri huko wilayani na mikoni serikali ikawa na utaratibbu wa kuongea na viongozi wa dini mara kwa mara ili kusaidiana katika kutatua baadhi ya matatizo ya kijamii na kuangalia namna ya kuendeleza huduma za jamii kama elimu afya maji nk
 
Kumtia Hatiani Mtu Kwenye kesi ya Jinai ya Mauaji sio jambo jepesi Kama kumtia Mtu hatiani kwa kusimama Na gari Kwenye Zebra

Risasi ikiyotumika Kwenye mauaji imepatikana?
DED ana miliki Silaha Na jee hiyo Silaha ina uhusiano Na Risasi iliyotumika?

Huyo Afisa Wanyamapori alikuwa Na Silaha ambayo inaweza kushabihiana Na Risasi iliyotumika?

Hukumu Za Mauaji hazitegemei Msimamo wa wengi Au matakwa ya wengi bali facts tupu
Simjui DED wala simjui huyo Afisa Wanyamapori lakin Ni dhambi kubwa kumsingizia Au kumuonea Mtu kwa Jinai Za aina hiyo

Tunapo urgue tusiingizie Mapenzi Au Chuki zetu Za Kisiasa Kwenye kuhukumu kesi hii
Wewe kwako mtu kuamuru watu wenye silaha waende kufanya vurugu kwenye Ibada ni sahihi? Kulikuwa na uharaka gani wa kwenda kudai ushuru kanisani siku ya Ibada?
Jiweke wa ndugu wa marehemu halafu njoo na utetezi huu usio na mashiko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uwezo wako wa ku urgue nami unatofautiana Huenda wako upo juu Au wangu upo juu ndio sababu hujaelewa nilichoandika japo ume quote
 
AFE KABISA MUUAJI MKUBWA,
TANGU LINI KWENDA KWENYE IBADA KUHARIBU UTARATIBU WA IBADA? MAREHEMU HAKUWA NA KWAKE? HALAFU YEYE NI POLISI ? HALAFU HUYO ROSE ANDREW NI HAWALA YAKE?

MAANA KAMA MLALAMIKAJI WA KUHARIBU SHAMBA LAKE NI ROSE ENDREW HUYO NDO ALIPASWA AENDE POLIS AKAFUNGUE KESI POLIS WANGEMTAFUTA MTUHUMIWA WAO KWA WAKATI WAO.

MIMI HUUO SIMUONEI HURUMA NAMUOMBEA AFE KABISA NA KAMA MUNGU ANANISIKIA HEBU AONYESHE MIUJIZA YAKE KWENYE HILI TUKIO.
 
Huwezi ukauwa mbele ya umati wa watu halafu ukachomoka kwa kusema unapakaziwa, siyo rahisi ndugu ded jipange kumshawishi hakimu aamini maneno yako na atupilie mbali ushahidi wa watu waliokuwa jirani na marehem wakati anapigwa risasi!
 
analalia kitanga cha hospitali badala ya mkeka wa mahabusu? nivi ni kwa nini alienda kanisani na askari wanyamapori badala ya polisi?
 
Ingawa is jambo jipya kuingia katika NYUMBA za ibada na silaha,lakini tujiulize
Kwanini waingie na silaha kanisani ?
Walishindwaje kumdhibiti.huyo mtu HADI risasi itumike,muhanga.alikuwa na silaha na.hao askari walipitia mafunzo ya kukcabiliana mtu ASIE na silaha ?
Kwanini mkurugenzi alitoka nje wakati walikuja pamoja ?
 
1. Mwenye bomba hakai foleni.
2. Mtoto wa dada akiua hafungwi.
 
Mkurugenzi wa halmashauri kuongoza msafara wa askari wa wanyamapori kwenda kanisani kupiga waumini ndio alifundishwa kwenye semina elekezi? Mpaka hapo asiseme anapakaziwa cha kwanza anatakiwa ajiuzuru wadhifa wake ili aviachie kazi vyombo vya usalama na sheria vifanye kazi yake
 
Hata kama akufyatua yeye risasi kama anavyodai bado anayo kesi ya kujibu tena kesi ya mauaji ya kukusudia kwani yeye ndiye alitoa melekezo na hata mazingira yote ya tukio yanamuhusisha yeye kama mtuhumiwa namba moja..tunazokumbukumbu za kesi mbali mbali za namna hii mfano ni kesi ya hivi karibuni ya bilionea Msuya wa Arusha..waliofungwa sio tu waliommiminia risasi bilionea msuya bali hata waliopanga mauaji pia
Mbona hiyo ya bilionea Msuya ni ya mbali. Ya karibu ni hii kesi inayowatesa akina Mbowe, Matiko na viongozi wengine wa CHADEMA ambao kesi yao imetokana na mazingira yaliyopelekea kifo cha mwanachuo wa NIT Aquilina. Wao hawakuua lakini kesi ya mauaji imefunguliwa dhidi yao. Sioni tofauti ya kesi hii na ya huyo DED tena ambaye alikosa hekima ya kumsubiri marehemu hata nje ya mazingira ya kanisa ili kuonana nae.

Halafu binadamu tulivyo na dharau kwa mwenyezi Mungu huyo DED akiwa hospitali anadai kumshukuru Mungu kwa kumpigania kwa hali yake ya sasa huku alishindwa kumheshimu huyo huyo Mungu na kuingilia ibada. Kwa hasira unaweza kutamani hiyo pumu inayomsumbua isiachie iendelee kumbana hadi na yeye akate pumzi yake ya mwisho.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Singida. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, Pius Luhende anayedaiwa kuhusika na mauaji ya Isaka Petro (28) amezungumza na Mwananchi akisema “nimepakaziwa tu.”

Luhende alitoa kauli hiyo baada ya mwandishi wetu kumtembelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida alikolazwa tangu Jumanne wiki hii baada ya kupewa rufaa kutoka Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.

Kwa mujibu wa mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Ng’hungu Kuzenza, Luhende anasumbuliwa na pumu (asthma) na mapigo ya moyo.

Mkurugenzi huyo ni miongoni mwa watu saba wanaoshikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo yaliyotokea Jumamosi iliyopita katika Kanisa la Wasabato Kijiji cha Kazikazi mkoani humo.

Inaelezwa kuwa mauaji hayo yalitokea baada ya Luhende kuwafuata watuhumiwa wa kosa la kuharibu mali ya mlalamikaji Rose Andrew aliyedai kuharibiwa mali yake iliyopo ndani ya shamba la Tanganyika Packers linalomilikiwa na halmashauri hiyo.

Taarifa ya Polisi inasema kuwa Luhende alipoingia ndani ya kanisa hilo ilitokea vurugu na akaamua kutoka nje kabla ya askari wanyamapori waliokuwa na silaha kufyatua risasi kadhaa na moja ikampiga Isaka na kufariki dunia papo hapo.

Hata hivyo, waumini waliokuwepo katika kanisa hilo wakati mauaji hayo yakitokea walizungumza na Mwananchi na kupingana na polisi wakisema kuwa mkurugenzi huyo ndiye alimfyatulia risasi Isaka.

Luhende ambaye alikuwa akilindwa na askari kanzu wanne wodini alisema bado kifua kinambana mara kwa mara hasa nyakati za usiku.

“Hata hivyo, namshukuru Mungu kwa kunipigania naendelea vizuri kuliko nilipokuwa hospitali ya Manyoni,” alisema Luhende ambaye alikuwa amejilaza kitandani huku mikononi akiwa hajafungwa pingu.

Katika maelezo yake, mkurugenzi huyo alisema amepakaziwa bila kufafanua zaidi kuhusu kauli yake hiyo.

Awali, Dk Kuzenza alisema mkurugenzi huyo alipofikishwa hospitalini hapo alikuwa na hali mbaya akibanwa kifua na tatizo la mapigo ya moyo.

“Tulipompokea alikuwa na hali mbaya kutokana na kubanwa mara kwa mara na kifua. Kwa upande wa mapigo ya moyo tatizo hilo lilianza kupungua. Kwa sasa tatizo la presha tumelidhibiti kiasi cha kutosha,” alisema. Alisema hata tatizo la asthma limeanza kupungua na kwamba atakuwa chini ya uangalizi hadi keshokutwa, “tukijiridhisha kuwa hali yake imeimarika, tutamruhusu kuondoka.”

Wakati huohuo, kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Isaya Mbughi amesema bado wanaendelea kukamilisha hatua za kisheria kabla watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani.

Alisema taratibu hizo zikishakamilika, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili. “Luhende endapo atakuwa ameruhusiwa kutoka hospitalini tutamuunganisha,” alisema kamanda huyo.

Juzi, kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike alisema “hatujawapeleka mahakamani, bado kuna taratibu nyingine hazijakamilika, kwa sasa tunaandaa taarifa ya kumpelekea mwendesha mashtaka wa Serikali ambaye ataandaa taratibu za kuwafikisha mahakamani.”

Mgogoro wa ushuru wa mashamba katika mbuga ya Kitongoji cha Boma la kati unatajwa kuwa ndiyo chanzo cha tukio kwani halmashauri inasema mashamba hayo ambayo awali yalikuwa yakimilikiwa na Tanganyika Packers ni sehemu yao.

Chanzo: Mwananchi
Inawezekana haumwi hizo ni Technics tu kujinasua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes Yeye Atakuwa ama Shahidi upande wa Jamhuri Au Mtuhumiwa wa Mauaji!

Ila nimeshangazwa msiba kufanywa haraka sina Hakika Kama Postmoterm ilifanyika

Hiki tukio linanikumbusha tukio la Swahiba wangu Almarhuum Ukiwaona Ramadhan Mwinshehe Ditopile wa Mzuzuri ambae Kesi ile ilimnyima raha Pamoja Na kufarijiwa Sana Na Utawala Pamoja Na Ndugu wa Yule Dereva mpaka akazidiwa Na Msongo wa Mawazo Na Pressure Na hatimae akafariki Hotelini Morogoro

Kesi Za Mauaji zinasononesha Sana moyo Kuliko Za Ufisadi
Allah atuepushe Na vizazi vyetu mkosi huu wa kutoa nafsi ya Kiumbe pasi Na haki
Umenikumbusha Braza Ditto. Utoto wa Mjini ulizidi mnoo na alitambulika kwa hilo na hilohilo ndilo lililomuondoa. Naamini kabisa aliibeba ile silaha kama mkwara wa Watoto wa mjini hata kama angepigwa kibao asingefyatua.

Kusababisha kifo ni mtihani sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..sawa askari ndiye atatolewa awe kafara...na sadaka, ili DED asifungwe

lakini kwa namna tukio lilivyotokea na jaribio LA kufanya siri...na kauli tofauti kutoka kwa polisi na wale waamini wa hilo kanisa

ni wazi mhusika anatengenezewa mazingira ya kusafishwa.Wale waumini wasabato hawadanganyi..

Na hili tukio linataka kufanana na LA yule kamanda muuaji Zombe...tena bora ya Zombe na wenzake waliongozwa na tamaa ya Mali

*DED nakuona unachungulia JF bila pingu mikononi na miguuni...huchomoki.!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi ukauwa mbele ya umati wa watu halafu ukachomoka kwa kusema unapakaziwa, siyo rahisi ndugu ded jipange kumshawishi hakimu aamini maneno yako na atupilie mbali ushahidi wa watu waliokuwa jirani na marehem wakati anapigwa risasi!
Hivi sijui atachomokaje iwapo mashahidi walioshuhudia akiua ni hao hao waumini ambao kwa kumwogopa Mungu wao watatakiwa kutoa ushahidi bila kupindisha kwamba ni yeye aliua? Atawaonga wote ili kupindisha maneno? Au mashahidi wa mauaji hayo watakuwa ni akina nani kama siyo hao waumini kwa wingi wao?
 
Haya yote ni matokeo yakufanya kazi kwa mihemko.Ded mzima unaendaje kufanya kazi za kipolisi,tena hadi makanisani.Kiongozi yoyote akiweka masifa mbele na busara na hekima nyuma matokeo yake ndo kama haya.
 
Baba wa marehemu amesema amemuona DED kwa macho lake akifyatua risasi kwa kijana wake.

Hawa vijana wawe na huruma kwa mjomba wao, yule mwingine ametuambia CCM isipotaka haipeleki maendeleo na cha kuwafanya hatuna.
 
Hata kama akufyatua yeye risasi kama anavyodai bado anayo kesi ya kujibu tena kesi ya mauaji ya kukusudia kwani yeye ndiye alitoa maelekezo na hata mazingira yote ya tukio yanamuhusisha yeye kama mtuhumiwa namba moja..tunazokumbukumbu za kesi mbali mbali za namna hii mfano ni kesi ya hivi karibuni ya bilionea Msuya wa Arusha..waliofungwa sio tu waliommiminia risasi bilionea msuya bali hata waliopanga mauaji pia
Wanavyosema kuwa ni ndugu wa jiwe hapo hakuna kesi labda Mungu ahukumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom