DED wa Itigi: Ninapakaziwa kesi ya mauaji

DED wa Itigi: Ninapakaziwa kesi ya mauaji

Jitu kma hili lilitakiwa nalo lipigwe mawe palepale
Ndio ilikuwa hukumu yake hiyo
Watu wanafiki sana yaani mwizi wa mihogo anachomwa moto na njaa yake, lakini watu wanaingia na kuuwa wanatoka salama


Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Kwanini waliingia Kanisani Na Silaha?

Huenda ni Kweli Yeye binafsi hajahusika lakin akiwa Kama Kiongozi aliona Ni busara Kweli kuvamia Mkusanyiko Tena ndani ya Nyumba ya Ibada ukiwa Na Askari wenye Silaha Za Moto?

Kama pale kanisani kungekuwa Na Waumini wenye silaha Za Moto Pia si ingekuwa Zahmatu minal balaa?

Nabii Suleiman Alayhissalam aliomba Sana Hikma kwa Kuwa Hikma ndio Msingi wa Uongozi bora sio Elimu kwa Kuwa Wasaidizi wako wanatosha kukushauri kitaalam nawe ukaamua kwa hekma

Mkurugenzi alikosa Hikma
Acha kumtetea DED mtoto wa dada yake Jiwe, angekua mngine hapo, release letter ya utenguzi ingeshatoka siku nyingi na masimango juu.
 
Hajatoa amri, aliua.

Hizi za eti alitoa amri ni conspiracies za kumlinda.
Taarifa za mwanzo walisema alitoa amri. Hata kama alitoa amri yeye ndiye muuaji. Kama yeye ndiye kaua ni sawa tu na kutoa amri. Yuko lupango na asubiri kukaa jela hata aliokolewa atkiona cha moto tu. Kutoa roho ya binadamu si mchezo. Lazima alipe. Eti anajidai anamshukuru Mungu, Mungu gani huyo? Labda mungu mwenye m ndogo lakini si Mungu Yawe, Elohim, El Gibbor, Alpha na Omega na majina mengi mazuri aliyo nayo Mungu wetu muumbaji.
 
Unafikiri kukutwa na hatia kwa kesi ya mauaji ni mpaka bastola ufyatue mwenyewe? Waulize kina papa msofe wanaoza ngome na hata kwenye tukio hawakuwepo...sasa huyu kaenda kabisa na watu wake kanisani kuanzisha shari mpaka mtu ameuawa na watu wake...anachomoka vipi hapo kihalali?
Kumtia Hatiani Mtu Kwenye kesi ya Jinai ya Mauaji sio jambo jepesi Kama kumtia Mtu hatiani kwa kusimama Na gari Kwenye Zebra

Risasi ikiyotumika Kwenye mauaji imepatikana?
DED ana miliki Silaha Na jee hiyo Silaha ina uhusiano Na Risasi iliyotumika?

Huyo Afisa Wanyamapori alikuwa Na Silaha ambayo inaweza kushabihiana Na Risasi iliyotumika?

Hukumu Za Mauaji hazitegemei Msimamo wa wengi Au matakwa ya wengi bali facts tupu
Simjui DED wala simjui huyo Afisa Wanyamapori lakin Ni dhambi kubwa kumsingizia Au kumuonea Mtu kwa Jinai Za aina hiyo

Tunapo urgue tusiingizie Mapenzi Au Chuki zetu Za Kisiasa Kwenye kuhukumu kesi hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa nimemshangaa kweli..maana hata kama sio risasi ya DED iliyouwa na badala yake ni ya askari...hao askari wanafuata maagizo ya nani?
Acha kutetea unyama wa hao wanyama wauaji, unawezaje kwenda kanisani kufanya fujo? hao walidhamilia wote wanakesi ya kujibu, huwezi ingia kanisani kumkamata mtuhumiwa wa uharibifu wa mali utadhani ni gaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taarifa za mwanzo walisema alitoa amri. Hata kama alitoa amri yeye ndiye muuaji. Kama yeye ndiye kaua ni sawa tu na kutoa amri. Yuko lupango na asubiri kukaa jela hata aliokolewa atkiona cha moto tu. Kutoa roho ya binadamu si mchezo. Lazima alipe. Eti anajidai anamshukuru Mungu, Mungu gani huyo? Labda mungu mwenye m ndogo lakini si Mungu Yawe, Elohim, El Gibbor, Alpha na Omega na majina mengi mazuri aliyo nayo Mungu wetu muumbaji.

Wahuni hawa, wanaweza kupiga kata funua ukashtukia kesi anaikwepa.

Kumbuka Zombe na Ditopile.
 
Singida. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, Pius Luhende anayedaiwa kuhusika na mauaji ya Isaka Petro (28) amezungumza na Mwananchi akisema “nimepakaziwa tu.”

Luhende alitoa kauli hiyo baada ya mwandishi wetu kumtembelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida alikolazwa tangu Jumanne wiki hii baada ya kupewa rufaa kutoka Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.

Kwa mujibu wa mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Ng’hungu Kuzenza, Luhende anasumbuliwa na pumu (asthma) na mapigo ya moyo.

Mkurugenzi huyo ni miongoni mwa watu saba wanaoshikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo yaliyotokea Jumamosi iliyopita katika Kanisa la Wasabato Kijiji cha Kazikazi mkoani humo.

Inaelezwa kuwa mauaji hayo yalitokea baada ya Luhende kuwafuata watuhumiwa wa kosa la kuharibu mali ya mlalamikaji Rose Andrew aliyedai kuharibiwa mali yake iliyopo ndani ya shamba la Tanganyika Packers linalomilikiwa na halmashauri hiyo.

Taarifa ya Polisi inasema kuwa Luhende alipoingia ndani ya kanisa hilo ilitokea vurugu na akaamua kutoka nje kabla ya askari wanyamapori waliokuwa na silaha kufyatua risasi kadhaa na moja ikampiga Isaka na kufariki dunia papo hapo.

Hata hivyo, waumini waliokuwepo katika kanisa hilo wakati mauaji hayo yakitokea walizungumza na Mwananchi na kupingana na polisi wakisema kuwa mkurugenzi huyo ndiye alimfyatulia risasi Isaka.

Luhende ambaye alikuwa akilindwa na askari kanzu wanne wodini alisema bado kifua kinambana mara kwa mara hasa nyakati za usiku.

“Hata hivyo, namshukuru Mungu kwa kunipigania naendelea vizuri kuliko nilipokuwa hospitali ya Manyoni,” alisema Luhende ambaye alikuwa amejilaza kitandani huku mikononi akiwa hajafungwa pingu.

Katika maelezo yake, mkurugenzi huyo alisema amepakaziwa bila kufafanua zaidi kuhusu kauli yake hiyo.

Awali, Dk Kuzenza alisema mkurugenzi huyo alipofikishwa hospitalini hapo alikuwa na hali mbaya akibanwa kifua na tatizo la mapigo ya moyo.

“Tulipompokea alikuwa na hali mbaya kutokana na kubanwa mara kwa mara na kifua. Kwa upande wa mapigo ya moyo tatizo hilo lilianza kupungua. Kwa sasa tatizo la presha tumelidhibiti kiasi cha kutosha,” alisema. Alisema hata tatizo la asthma limeanza kupungua na kwamba atakuwa chini ya uangalizi hadi keshokutwa, “tukijiridhisha kuwa hali yake imeimarika, tutamruhusu kuondoka.”

Wakati huohuo, kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Isaya Mbughi amesema bado wanaendelea kukamilisha hatua za kisheria kabla watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani.

Alisema taratibu hizo zikishakamilika, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili. “Luhende endapo atakuwa ameruhusiwa kutoka hospitalini tutamuunganisha,” alisema kamanda huyo.

Juzi, kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike alisema “hatujawapeleka mahakamani, bado kuna taratibu nyingine hazijakamilika, kwa sasa tunaandaa taarifa ya kumpelekea mwendesha mashtaka wa Serikali ambaye ataandaa taratibu za kuwafikisha mahakamani.”

Mgogoro wa ushuru wa mashamba katika mbuga ya Kitongoji cha Boma la kati unatajwa kuwa ndiyo chanzo cha tukio kwani halmashauri inasema mashamba hayo ambayo awali yalikuwa yakimilikiwa na Tanganyika Packers ni sehemu yao.

Chanzo: Mwananchi
Polisi wanatakiwa kuitafuta na kuipata bunduki iliyotumika. Namba za bunduki zitatumika kumjua miliki wake na ndie atakuwa mtuhumiwa.
 
Ditopile wa Mzuzuri aliua, wakasema ni manslaughter, akafungwa, kisha akaachiwa huru. Lakini aliye juu, huyo hana upendeleo( The Most High GOD), si alibebwa akiwa chumbani Ati anasali. Chezeya Mfalme wa haki weye!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti anasumbuliwa Athma..aende mahabusu wampakizie na Inhaler akawe anajipulizia huko akisubiri upelelezi ukamilike..au la aende maduka ya kisuni kuna dawa za asthma wampe akaendelee kunywea mahabusu shenzytype huyoo alafu hana pingu...!mxiew sana hili linchi jaman
 
Tutulie wananchi, hizi sio zile zama za unajua mimi ni nani

Hakuna atakaechomoka hapo

Haki itatendeka
 
Back
Top Bottom