Eric Cartman
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 11,960
- 11,222
Eric,
Katika Demokrasia ,vyama vya upinzani na hata chama Tawala vina wajibu na dhamana ya kuwaelimisha wananchi kuhusu misingi ya Demokrasia.Kwa bahati mbaya suala hili limekua tofauti nchini mwetu
Ni Chama cha demokrasia na Maendeleo pekee kilichoamua kuvunja utamaduni huu na kuamua kuanzisha mkakati wa kutoa elimu ya Uraia kwa wananchi wake kuanzia OPERESHENI SANGARA hadi sasa tuna vuguvugu la mabadiliko M4C(Movement for Change) nakuanzisha utamaduni mpya(usher in a new culture) unaojenga uwezo na kuongeza ari kwa wananchi katika kushiriki,kushinikiza na kuiwajibisha serikali yao
CHADEMA kinaamini kwamba wananchi wanapoielewa vyema misingi ya demokrasia inakua Rahisi kwao katika kushiriki katika Nyanja zote za utawala.
Katika Dira,Falsafa na Mtazamo wa CHADEMA unalenga kuweka nguvu ya umma au wananchi mbele katika shughuli zote zinazohusu utawala na maamuzi kupitia falsafa yake ya nguvu ya umma ambayo ndiyo msingi wa maamuzi na kichocheo cha mfumo au muundo wa utawala wa majimbo badala ya kulundika mamlaka yote kwa watawala kama ilivyo sasa na hasa sehemu moja bila kuwa na mawasiliano ya karibu ya wananchi.Ni kukasimisha madaraka kutoka makao makuu na kuyapeleka kwenye utawala wa kikanda kupitia mgawanyo huu(decentralization through zoning).Kulundika mamlaka sehemu moja kama ilivyo sasa ni kujiweka mbali na hisia za wananchi na hili limekua tatizo kubwa katika uendeshaji wa nchi na hata katika Mashirika makubwa.
Muundo huu wa majimbo unaoendana na uwezo wetu kiuchumi unatoa Taswira Chanya ya serikali ya Baadae ya itakayoundwa na CHADEMA na sasa CHADEMA kimeamua kwa muda huu ulioaki kiunde mfumo wa aina hii katika kipindi hiki cha mpito kabla ya kuchukua Dola mwaka 2015 ili wananchi wapate kuona ubora wa mfumo huu utakaoleta matumaini mapya,Uhuru na fursa katika kufanya maamauzi bna kushiriki moja kwa moja katika kuendesha Taifa lao kwa ufanisi zaidi
Raslimali tulizo nazo ni akili,ubunifu na uzalendo wa kutosha wa viongozi na wanachama wetu.Kuchangishana ni njia inayotumika kuleta mageuzi ya Kizalendo.Hata TANU waliitumia kumuondoa mkoloni mweupe.
Hao waliofukuzwa wangekua kwenye muundo huu wasingeshughulikiwa huku juu kwani huko ngazi za chini tayari wangekua easly detected!
Kuhusu suala la CCM kuja huku,ni bora waje ili waturahisishie kazi.
Ben
Unachokizungumzia hapa sio sera ya majimbo (if by that we mean federalism) all you do is describing problems with the current politics and its democratic deficit. Hence you seem to think decentralization only occurs under majimbo then you go and explain the need for local governance and its importance on people participation whilst trying to solve local problems using local resources and thinking.
That is not federalism it is just decentralization of powers into local authorities (local governments) and it is embraced both in unitary and federal states. And I do agree on this argument.
But federalism is a completely different ball game from what you're describing.
mfumo wa majimbo ni suluhisho la matatizo mengi saana, hasa kwa nchi yetu, wapo wanaoupinga, si vibaya ila watoe hoja za msingi na si kejeli
True na kuna sababu hapo, kwa sababu federal states nying zimetokana na miuongano ya mataifa ambayo iliona ulazima wa kubakiza sehemu za mamlaka yao na baadhi ya vitu vifanyike katika muono wao mfano sheria zao (kumbuka sheria utungwa na moral values of the time katika jamii husika) na mengine ambayo hawakutaka yaamuliwe kwengine.Si lazima DECENTRALIZATION iletwe na sera ya majimbo lakini kumbuka SERA YA MAJIMBO yenyewe ni DECENTRALIZATION.Katika kila FEDERALISM kuna DECENTRALIZATION lakini si kila DECENTRALIZATION inaletwa na FEDERALISM.
Ben Saanane
Hiii sera ndio umeiweka kuwamaliza kabisa. Tutafutane after mwaka mmoja mkianza kuitekeleza mungu akijalia uniambie.
Naomba nieleweke sipingani na sera yenyewe kama yenyewe bali uwezo wa ku-implement CDM hamna.
Jiulize mahitaji ya sera hii ni yepi hilo moja kwa kuwasaidia...,nijuavyomie ili sera yenu iwe effective kitu cha kwanza nilazima muwe na watu firm ambao wanaweza kuisimamia kwa implicitly hasa ngazi ya chini huko mnaposhusha nguvu za maamuzi. Wapo wapi watu hao?je wapo firm na unauhakika??BAVICHA tu imewashinda watu wamebadilishwa muelekeo itakua nchi nzima????na tena wanakua na mahamuzi ebu fikiria mfano ndio mmoja wa mliowatimua yupo mkoa wenye nguvu kama dar na madaraka ya maamuzi anayo patachimbika..nawambieniCCM wanawafata huko huko kuwamaliza..hamna resources na capabilities za kutosha kuendesha mfumo huu..hauwezi kuweka mfumu huu kwa chhama ambacho hata uwezo wa kifedha bado kinachangisha hata kama mfumo ni mzuri ukafanya kazi.
Thax
True na kuna sababu hapo, kwa sababu federal states nying zimetokana na miuongano ya mataifa ambayo iliona ulazima wa kubakiza sehemu za mamlaka yao na baadhi ya vitu vifanyike katika muono wao mfano sheria zao (kumbuka sheria utungwa na moral values of the time katika jamii husika) na mengine ambayo hawakutaka yaamuliwe kwengine.
In short mengi yalioachwa ni makubaliano katika kulazimisha kuungana kwakuwa hicho ndicho kilichokuwa muhimu. A modern example at it's ealiest stage ni muungano wa EU ambao ulianza like a trade-block, as days go by more and more powers are transferred to Brussels that affect all member states kiasi cha waingereza kuanza kujiuliza kulikoni.
Lakini hata huko kwenye federalism na states ambazo wamebakiza certain powers inorder to achieve good governance they still need to decentralize power even further just as a unitary state does(matter of fact almost in similar ways).
Kwa maana hiyo there is no differences in the approach of good governance style, isipokuwa where federal is concerned ni nchi ziliungana au kingdoms na ziliamua kubakiza baadhi ya mamlaka na trust me there different views on most of these states and huge efforts on propaganda are needed to build a sense of national identity, sehemu kama marekani the media, CIA, FBI and hollywood play important roles on implementing a sense of national patriotism and we are talking of the superpower of our time.
Ukitaka kuona matatizo nenda kaangalie huko India (kumbuka Pakistani not long ago was part of hers) and the current problems it still has in keeping some states au huko Russia na China.
These are not easy states to bring about a sense solidarity and building a sense of national patriotism, there is the danger of people pledging their loyalties into their states and cause problems kama Nigeria. Na hizo ni nchi ambzo atuzipati hata chembe kwa scholars who can advice on how to win support,huko most of us here are nobodies in their scholarly word (kutokana na amount of publications ambazo zimekuwa implemented world wide) na wanashindwa.
Sasa kweli sisi tunalilia federalism kisa decentralization wakati wenzetu walifanya hivyo hili kuungana, halafu watu waanze kuweka fikra za kimila pengine katika muono wao katika katiba zao bila ya kuingiliwa. Considering the ignorance level who is to say ukabila autashamiri na kuleta matatizo makubwa huko mbele au wanasiasa hawatumia hisia kadhaa hata za ndani ya states kuendelea kubagua (the debate here is long and needs evidence which is vastly available).
In another words tunalazimisha mfumo ambao miuondo yake si ya taifa moja yaani ni sawa na sehemu kama "Michigan States" in USA wajigawe tena kwa namna ya sera ya CDM.
By the way decentralization through democracy also entails election kama unavyoona mayoral election where it concerns or local counselors election where it is concerned, kwa maana hiyo what we have in Tanzania needs to be modernized na vyeo vingine viondoke lakini si majimbo.