Dear Mange na wanaharakati wengine wa mtandaoni

sinza pazuri

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
3,704
Reaction score
9,920
Kwanza kabisa, heshima kwa kazi mnayofanya. Kiukweli mmeziba gap kubwa sana kwenye mapambano dhidi ya dhulma, ufisadi, uonevu, uchawa, watu kutekwa, kupotezwa na kuuwawa.

Zamani sehemu kubwa ya kazi hii ilikuwa inafanywa na wanasiasa. Wakati nafasi ya kufanya siasa ilipobanwa, wanaharakati wa mtandaoni waka-cover hiyo gap. Mchango wenu ni mkubwa, hakuna mwenye akili timamu anayeweza kuubeza.

Na najua si rahisi. Kubezwa, kuitwa majina, kuchonganishwa, kukimbiwa na ndugu na marafiki, kupoteza uhuru, mali na wakati mwingine usalama. Pamoja na hayo bado mnasonga mbele.

Mange au Maria Sarungi, kwa mfano, pengine kama wasingeingia kwenye haya mapambano wangeendelea na maisha yao na kutafuta pesa zao. Wangekuwa na pesa za kutosha, nitakuwa wa mwisho kuamini Mange anaingiza hela ya maana kwenye harakati zaidi ya biashara yake ya umbeya. Tunajua pia Maria ni mpambanaji na sio haba alikuwa pazuri sana. Lakini wameamua kutumia platforms zao kwenye harakati. Hilo linahitaji kuheshimiwa.

Lakini sasa kwenye point yangu.
Nadhani baadhi yenu mmeanza kwenda too far kwa sababu ya hisia kali, frustration au kutaka matokeo ya haraka.

Tatizo ni kwamba wakati mwingine mnaanza kuamini kila taarifa mnayopewa, hata kama haijathibitishwa.

Mfano sakata la Mange kuhusu Lema na ndugu wa Lissu kupewa makazi Sea Cliff......kama taarifa yenyewe ilikuwa haijathibitishwa, basi si vizuri kukomaa nayo kama fact hata baada ya kuibuka maswali.

Maria Sarungi naye juzi alitoa taarifa iliyomhusu Mzee Kikwete, halafu kesho yake tukamuona mtu mwenyewe akiwa mtaani. Hapa pia lesson ni ileile: kuwa na source hakumaanishi kila source iko sahihi.

Sativa naye kuna kipindi alikuwa akiwashambulia viongozi wa BAKWATA, lakini namna ujumbe ulivyokuwa unaenda wakati mwingine ilionekana kama anaukosoa Uislamu kwa ujumla. Hapo ndipo unahitaji caution.
Hilda Newton tumeshamzoea kwa matangoporina.

Sio kwamba wanaharakati hawaruhusiwi kukosea. Wanaruhusiwa.
Tatizo ni pale unapokuwa na audience kubwa, una influence kubwa, halafu ukikosea hutaki kurekebisha.
Hapo unaharibu credibility uliyoijenga kwa muda mrefu.

Na tusifanye kosa jingine la kuwaita wanaharakati wote emotional, wajinga, waongo au hysterical. Hiyo nayo ni generalization isiyo na haki.
Wapo wanaharakati ambao wamepitia mambo mazito sana kwenye miaka hii. Wengine wamepoteza mali, uhuru, mahusiano, ndugu na marafiki. Huwezi kupuuza hiyo reality.

Lakini influence kubwa inahitaji discipline kubwa.
Kuwa na followers 500K hakufanyi kila taarifa yako iwe true.
Kuwa na “intel” hakumaanishi kila intel ni sahihi.
Na followers nao wasigeuke nyumbu mpaka kila anachosema mtu fulani wanafatisha tu.

Halafu kuna hili la “sisi ndio tumefanikisha”.
Sisi ndio tuliingiza watu mtaani.
Sisi ndio tumefanikisha milioni 300 za Tone Tone.
Sisi ndio tulifanya hiki.
Hizi kauli hazisaidii.
Kwa sababu harakati na vyama vya siasa vinahitajiana.

CDM bila harakati itakuwa na limitation zake.
Lakini harakati bila political organization nayo ina limitation zake.

Wanasiasa wana institutional responsibility, negotiation na political strategy.
Wanaharakati wana pressure, public attention na uwezo wa kuamsha jamii.
Kwa hiyo kwanini tushindane wenyewe kwa wenyewe?
CDM inahitaji wanaharakati. Wanaharakati wanahitaji political organization.
Lakini wote wanahitaji accountability.

Nadhani alichofanya Mnyika jana kwenye suala la discipline kina point kubwa: movement haiwezi kujengwa kwa kila mtu kufanya anachotaka kwa sababu tu ana followers wengi.
Tunahitaji kuheshimiana, ustaarabu, staha na discipline.
Kwa kifupi, wanaharakati wasipunguze nguvu zao......wapunguze tu reckless reactions.

Wanasiasa wasiwadharau wanaharakati.......lakini pia wasiwe mateka wa pressure zao.
Kila upande ubaki na independence yake, lakini wote wajue wanapigania nini.
Kwa sababu mwisho wa siku, tunahitaji wote.

Na hakuna upande ambao hauwezi kukosea.
 
Nakiri kuwa kwa mara ya kwanza nimesoma uzi wako wote nikaumaliza, nikauelewa vyema.

Kongole sana kwa ushauri mzuri sana, si kwa hao wanaharakati tu uliowataja, bali ni ushauri utufaao sisi sote kama wana Jamii Forums.

Uliyoyaandika ni sahihi kabisa.
Tuwe tunatafuta ukweli wa habari zetu kabla ya kuziweka public na tuwe na utayari wa haraka kuomba msamaha pale tunapokuwa tumepotosha/tumepotoshwa.

Kongole sana kwa mara nyingine tena.
Kwanza kabisa, heshima kwa kazi mnayofanya. Kiukweli mmeziba gap kubwa sana kwenye mapambano dhidi ya dhulma, ufisadi, uonevu, uchawa, watu kutekwa, kupotezwa na kuuwawa.

Zamani sehemu kubwa ya kazi hii ilikuwa inafanywa na wanasiasa. Wakati nafasi ya kufanya siasa ilipobanwa, wanaharakati wa mtandaoni waka-cover hiyo gap. Mchango wenu ni mkubwa, hakuna mwenye akili timamu anayeweza kuubeza.

Na najua si rahisi. Kubezwa, kuitwa majina, kuchonganishwa, kukimbiwa na ndugu na marafiki, kupoteza uhuru, mali na wakati mwingine usalama. Pamoja na hayo bado mnasonga mbele.

Mange au Maria Sarungi, kwa mfano, pengine kama wasingeingia kwenye haya mapambano wangeendelea na maisha yao na kutafuta pesa zao. Wangekuwa na pesa za kutosha, nitakuwa wa mwisho kuamini Mange anaingiza hela ya maana kwenye harakati zaidi ya biashara yake ya umbeya. Tunajua pia Maria ni mpambanaji na sio haba alikuwa pazuri sana. Lakini wameamua kutumia platforms zao kwenye harakati. Hilo linahitaji kuheshimiwa.

Lakini sasa kwenye point yangu.
Nadhani baadhi yenu mmeanza kwenda too far kwa sababu ya hisia kali, frustration au kutaka matokeo ya haraka.

Tatizo ni kwamba wakati mwingine mnaanza kuamini kila taarifa mnayopewa, hata kama haijathibitishwa.

Mfano sakata la Mange kuhusu Lema na ndugu wa Lissu kupewa makazi Sea Cliff......kama taarifa yenyewe ilikuwa haijathibitishwa, basi si vizuri kukomaa nayo kama fact hata baada ya kuibuka maswali.

Maria Sarungi naye juzi alitoa taarifa iliyomhusu Mzee Kikwete, halafu kesho yake tukamuona mtu mwenyewe akiwa mtaani. Hapa pia lesson ni ileile: kuwa na source hakumaanishi kila source iko sahihi.

Sativa naye kuna kipindi alikuwa akiwashambulia viongozi wa BAKWATA, lakini namna ujumbe ulivyokuwa unaenda wakati mwingine ilionekana kama anaukosoa Uislamu kwa ujumla. Hapo ndipo unahitaji caution.
Hilda Newton tumeshamzoea kwa matangoporina.

Sio kwamba wanaharakati hawaruhusiwi kukosea. Wanaruhusiwa.
Tatizo ni pale unapokuwa na audience kubwa, una influence kubwa, halafu ukikosea hutaki kurekebisha.
Hapo unaharibu credibility uliyoijenga kwa muda mrefu.

Na tusifanye kosa jingine la kuwaita wanaharakati wote emotional, wajinga, waongo au hysterical. Hiyo nayo ni generalization isiyo na haki.
Wapo wanaharakati ambao wamepitia mambo mazito sana kwenye miaka hii. Wengine wamepoteza mali, uhuru, mahusiano, ndugu na marafiki. Huwezi kupuuza hiyo reality.

Lakini influence kubwa inahitaji discipline kubwa.
Kuwa na followers 500K hakufanyi kila taarifa yako iwe true.
Kuwa na “intel” hakumaanishi kila intel ni sahihi.
Na followers nao wasigeuke nyumbu mpaka kila anachosema mtu fulani wanafatisha tu.

Halafu kuna hili la “sisi ndio tumefanikisha”.
Sisi ndio tuliingiza watu mtaani.
Sisi ndio tumefanikisha milioni 300 za Tone Tone.
Sisi ndio tulifanya hiki.
Hizi kauli hazisaidii.
Kwa sababu harakati na vyama vya siasa vinahitajiana.

CDM bila harakati itakuwa na limitation zake.
Lakini harakati bila political organization nayo ina limitation zake.

Wanasiasa wana institutional responsibility, negotiation na political strategy.
Wanaharakati wana pressure, public attention na uwezo wa kuamsha jamii.
Kwa hiyo kwanini tushindane wenyewe kwa wenyewe?
CDM inahitaji wanaharakati. Wanaharakati wanahitaji political organization.
Lakini wote wanahitaji accountability.

Nadhani alichofanya Mnyika jana kwenye suala la discipline kina point kubwa: movement haiwezi kujengwa kwa kila mtu kufanya anachotaka kwa sababu tu ana followers wengi.
Tunahitaji kuheshimiana, ustaarabu, staha na discipline.
Kwa kifupi, wanaharakati wasipunguze nguvu zao......wapunguze tu reckless reactions.

Wanasiasa wasiwadharau wanaharakati.......lakini pia wasiwe mateka wa pressure zao.
Kila upande ubaki na independence yake, lakini wote wajue wanapigania nini.
Kwa sababu mwisho wa siku, tunahitaji wote.

Na hakuna upande ambao hauwezi kukosea.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom