DDP: Tukio la tindikali Zanzibar sio ugaidi

DDP: Tukio la tindikali Zanzibar sio ugaidi

Baada ya maelezo yangu ya kushangaa, napendekeza yafuatayo:
1. Serikali isimamie sheria inazotunga kupitia Bunge. Mawaziri wanaojaribu kufuata sheria mbona wanasifiwa? Tanzania tunazo sheria ambazo zinaweza kutusaidia kudhibiti baadhi ya mambo paoja na kwamba zinamapungufu. Hatuzitumii/ kuzifuata. Sheria ya udhibiti wa kemikali (Industrial and Consumer chemical (Management and Control) 2003 na marekebisho yake ni nzuri na haina mchezo juu ya uzalishaji, usafirishaji, utunzaji na matumizi ya kemikali! Kemikali nyingi zimetajwa na meno ni makali haswa! Kwa nini haifuatwi?????
2. Sheria ya kudhibiti vyakula, dawa na mamlaka zake; Food, Drugs and cosmetics Act 2003, hazina mapungufu makubwa juu ya udhibiti hata wa kadili juu ya umiliki na matumizi ya kemikali. Sheria zote zinamaelekezo na matakwa kisheria ya kuzalisha, kusafirisha, kutumia, kuhifadhi na kutupa!!!!

Tunataka vyombo vifuatavyo vifanye kazi zao
1. GCLA - Mkemia mkuu
2. NEMC - Mazingira
3. TFDA -
4. OSHA Tanzania
5. DPP
6. Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali

Wote hao wana nafasi ya kudhibiti mienendo yote ya Kemikali kama nivyotaja hapo juu. FANYENI KAZI ACHENI MAZOEA! Kodi Mnayolipwa mishahara, maghari, masomo, vitumbua na chai ofisini vinafaida gani kwa Mwananchi???
 
Narudia kusema ugaidi hauwezi kuwa ugaidi mpaka uchunguza ufanyike na kubaini kuwepo kwa mazingira ya ugaidi tukio haliwei kuitwa ugaidi kabla ya kuwepo vibainishi vya ugaidi.
 
Narudia kusema ugaidi hauwezi kuwa ugaidi mpaka uchunguza ufanyike na kubaini kuwepo kwa mazingira ya ugaidi tukio haliwei kuitwa ugaidi kabla ya kuwepo vibainishi vya ugaidi.

Chunguza akili yako vizuri. Je, uchunguzi wa siku moja umebainisha kuwa tukio lile siyo la Kigaidi? Kama ndiyo kwa nini matuko mengine yanachukua wiki, miezi kabla ya Tamko? Kama wameshatoa ufafanuzi huu mapema ikija kubainika ni la kigaidi watasemaje?. Kama matukio mengine yanayo fanana na hilo wanasema ni matukio ya kigaidi why this not?
 
ni wazi kabisa jeshi la polisi limeshindwa kazi yake.

DPP Mwigulu Nchemba toa maelekezo kwa Feleshi juu ya hili pia.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mimi nakuwa kinyume kabisa na wewe kwa sababu inawezekana kabisa kujihusisha kwetu na usuluhishi wa nje kukawa sababu ya kushambuliwa ili na sisi tuonekane hatuna amani , nasema hivyo kwa sababu Tanzania haikuanza leo kusaka amani katika mataifa jirani, wakati matukio ya kumwagiana tindikali ni ya juzi tu na hayana muda mrefu.

Hoja Dhaifu sana.
 
Narudia kusema ugaidi hauwezi kuwa ugaidi mpaka uchunguza ufanyike na kubaini kuwepo kwa mazingira ya ugaidi tukio haliwei kuitwa ugaidi kabla ya kuwepo vibainishi vya ugaidi.

la rwakatare na henry kileo mlikurupuka hadi bungeni na kuyaita ni ugaidi na mwisho wa siku jaji wa tabora juzi ametoa somo la ugaidi mahakamani.
naona somo limewaingia vema hasa ukizingatia hili linachafua kuanzia nchi hadi serikali na chama kilichopo madarakani.
 
Kwa sheria za Tanzania neno gaidi linatumika tu pale CHADEMA inapotakiwa kuhusishwa na uhalifu.
 
Mi ngoja niwasaidie kutangaza maana naona DPP jamaa yake Mwigulu wamekua na kigugumizi. Kwakua kitu kilichotumika ni kemikali aina ya Tindikali Basi Mimi nasema au natangaza waziwazi shambulio la Zanzibar ni la kigaidi maana tindikali ikitumika Basi ni ni Ugaidi. Au vp Wana Cdm
 
Nadhani umefika wakati sisi kama watanzania tujitazame kwa jicho la tatu namaana tuangalie mambo yanayosumbua nchi yetu ili kuboresha amani Tanzania, Haiwezekani tunashughulikia matukio ya nchi nyingine wakati ya ndani hatujayatatua," KAMA UMESHINDWA KUIONGOZA FAMILIA YA MKE, WATOTO, kAMWE HUWEZI ONGOZA TAIFA" Nadhani tunaitaji Mabadiliko Ya haraka katika taifa letu
Kuna mambo mengi mabaya yaliyop lakini yanafumbiwa macho. Nilikuwa Zanzbar miezi kama minne iliyopita nikasikiliza redio moja ikihamasisha kuwachukulia watalii hatua kali kwani hawafuati mila na desturi za kiislamu wanapokuja Z'bar. Mtangazaji alitolea mfano wa mavazi wanayovaa kuwa hayaendani na utamaduni wa dini ya Kiislamu. Nikiunganisha kuwa tukio hili limetukia mwezi mtukufu wa Ramadhani, sipati picha. Kwanini matangazo kama yale yanaruhusiwa na redio husika haichukuliwi hatua? Au ni kwa kuwa ni ya dini yetu? Haya ndo matokeo.
 
duh DPP Kaogopa sasa hata polisi hawajamaliza kuchunguza kshasema si ugaidi HII KALI YA MWAKA
 
Vyombo vip sasa??? Hivi vya sasa hopulesi
Nadhani ni mapema kuhusisha tukio la zanzibar na ugaidi, tuvipe vyombo vya dola muda ya kujiridhisha ili tupate taarifa iliyokamilika.

wizara ya utalii itunge sheri
 
Narudia kusema ugaidi hauwezi kuwa ugaidi mpaka uchunguza ufanyike na kubaini kuwepo kwa mazingira ya ugaidi tukio haliwei kuitwa ugaidi kabla ya kuwepo vibainishi vya ugaidi.

msemaj wa wizara ya mambo ya ndani???
 
Nadhani DPP yuko sahihi, siyo vizuri kuhusisha tukio hilo na ugaidi kwa vile hata wruhumiwa hawajakamatwa.

Acha uvivu wa kufikilia wewe aliye kuambia ili uite ugaidi lazima mtuhumiwa akamatwe nani? Sept 11 wamarekani walipo sema ni ukio la kigaidi la Osama walikuwa wamemkamata? wewe kubali ukweli kuwa dpp anatumika kisiasa na akina mwigulu kani suala la kukamatwa au kutokukamatwa halifuti muundo wa tukuio kama la kigaidi au la.
 
Narudia kusema ugaidi hauwezi kuwa ugaidi mpaka uchunguza ufanyike na kubaini kuwepo kwa mazingira ya ugaidi tukio haliwei kuitwa ugaidi kabla ya kuwepo vibainishi vya ugaidi.
Na baada ya uchunguzi tunaangalia kama mtuhumiwa ana sura kama Pinda au Wasira basi huyo atakuwa gaidi. Lakini akiwa na sura nzuri huyo si gaidi.... kwikwikwikwikwiww
 
Haijalishi kama ni tukio la kigaidi au siyo tunachotaka sisi kama watanzania ni kukomesha matukio haya kuhakikisha kuwa tindikali haiuzwi wala kumilikiwa na watu ovyo ovyo.

suala la UGAIDI ni muhimu sana. unajua serikali ya ccm haikujua kwamba WHAT GOES AROUND COMES AROUND. kama walikuwa macho pima kuanzisha kesi za ugaidi dhidi ya CHADEMA, inakuwaje sasa wanapata kigugumizi? kwa sababu hakuna mtu wa kumsweka rumande akose dhamana kwa sababu anashtakiwa kwa kesi ya ugaidi? au kwa sababu hili linafuatiliwa kimataifa kwa hiyo wakitamka neno UGAIDI litaripotiwa? shame!!!
 
Chunguza akili yako vizuri. Je, uchunguzi wa siku moja umebainisha kuwa tukio lile siyo la Kigaidi? Kama ndiyo kwa nini matuko mengine yanachukua wiki, miezi kabla ya Tamko? Kama wameshatoa ufafanuzi huu mapema ikija kubainika ni la kigaidi watasemaje?. Kama matukio mengine yanayo fanana na hilo wanasema ni matukio ya kigaidi why this not?
Hizo porojo nenda mkafarijiane na jamaa zako. Ukweli uko wazi hakuna Ugaidi Tanzania wala isitake kukitetea mpk uchunguzi ufanyike mara Cjui Ugaidi mpk iwe niño! Ukweli ni kwamba dhana ya Ugaidi imehasisiwa na Ccm ili kuukandamiza upinzani. Mlifamikiwa kuizohofisha Cuf lakini kwa Cdm mmechemka. Na jamaa yenu Tendwa mlikua mnamtegemea awasaidie kukufuta Cdm ndo huyo amesepa. Amebaki DPP. Naye kuzi Amepewa Somo Kule Tabora na bwana jaji. Sasa ccm mmekwisha hiyo dhana yenu imegonga Mwamba. Chadema oyeeeeeee! Kibatala na Safari na Lissu na Mabele Malando juuuuuu!
 
Back
Top Bottom