DDP: Tukio la tindikali Zanzibar sio ugaidi

DDP: Tukio la tindikali Zanzibar sio ugaidi

Nadhani umefika wakati sisi kama watanzania tujitazame kwa jicho la tatu namaana tuangalie mambo yanayosumbua nchi yetu ili kuboresha amani Tanzania, Haiwezekani tunashughulikia matukio ya nchi nyingine wakati ya ndani hatujayatatua," KAMA UMESHINDWA KUIONGOZA FAMILIA YA MKE, WATOTO, kAMWE HUWEZI ONGOZA TAIFA" Nadhani tunaitaji Mabadiliko Ya haraka katika taifa letu

Mkuu mimi nakuwa kinyume kabisa na wewe kwa sababu inawezekana kabisa kujihusisha kwetu na usuluhishi wa nje kukawa sababu ya kushambuliwa ili na sisi tuonekane hatuna amani , nasema hivyo kwa sababu Tanzania haikuanza leo kusaka amani katika mataifa jirani, wakati matukio ya kumwagiana tindikali ni ya juzi tu na hayana muda mrefu.
 
Huyu dpp ni takataka kabisa, sijui jk alimtoa wapi huyu kenge maji.

Maneno kama hayo uliyoyaandika yanwaudhi sana TCRA, kama hauna hoja bora ukakaa kimya mkuu, Mods wanaweza kukusaidia kama itabidi.
 
Kwenye 24 hrs...naona jinsi ctu wanavyojaribu kuzuia matukio tarajiwa na kubuni mbinu za kuwakamata wahalifu.....si mchezo mambo yapo kwa teknolojia ya nguvu.....tiss walipaswa kuiga....ila siamin kama hapa bongo twaweza zuia uhalifu tarajiwa....longolongo tu...mungu tusaidie.

Duh, sitaki kusema lolote, ila ninavyojua na kuwa kuona movie nyingi kama za akina VANDAME, CHECKNORIS, na wengine wengi huwezi kufananisha na real world events.
 
Inawezekana umezoea jina la shuleni(kizungi). Tindikali kwa kimombo ni ACID, bado hujajua kazi yake?

Acid ziko za aina nyingi Bibikizee
Usije kumix Acid za CCM na Acid za mwalimu wako wa Chemistry Darasani kama vile HCL,H2SO4 etc etc
 
Last edited by a moderator:
Nadhani ni mapema kuhusisha tukio la zanzibar na ugaidi, tuvipe vyombo vya dola muda ya kujiridhisha ili tupate taarifa iliyokamilika.

La Igunga je???
Acha upoyoyo
 
Tukisema vyombo vya dola vinatumiwa na wanasiasa hasa ccm hawataki sasa kwanini na hili wasiseme ni ugaidi? Angekuwa ni Mtanzania kamwagiwa hio tindikali hakuna ambae angejali? ombaomba ccm wanaogopa wafadhili wao kuwanyima misaada
Sidhani kama ni sahihi kuhusisha tukio na ugaidi kabla ya uchunguzi wa awali haijakamilika. nakumbuka waliotuhumiwa na ugaidi kama akina Lwakatare, na wale makamanda wa tukio la Tabora hatua hiyo ilifikiwa baada ya uchunguzi, nadhani tusubiri kwanza uchunguzi ufanyike na vyombo husika vitatupa taarifa sahihi kuliko kuwanza kulazimisha kuwa ni ugaidi eti kwa sababu tu makamanda nao walituhumiwa kwa ugaidi.
 
Wakuu ninaomba kuelewa: Tindikali inapatikana wapi? Ni nani anaeruhusiwa kuwa nayo kihalali? Je matumizi yake halali ni yapi?

nafikiri dr slaa na lwakatare wanajua zaidi wapi inapatikana maana ni miongoni mwa silaha baridi wanazotumia kujijenga kisiasa
 
Maneno kama hayo uliyoyaandika yanwaudhi sana TCRA, kama hauna hoja bora ukakaa kimya mkuu, Mods wanaweza kukusaidia kama itabidi.

Umetumwa na nani na unalipwaje ????
 
Kama uchunguzi ungekuwa umefanyika na ikajulikana kuwa ni swala la kupangwa na kundi la watu tungeita ni ugaidi lakini uchunguzi bado haujafanyika.
 
La Igunga je???
Acha upoyoyo
Nadhani haukumuelewa Mahoka2 alichojaribu kusema ni kuwa, hayo matukio ambayo makamanda wa Cdm walituhumiwa kuwa ni ugaidi yalishafanyiwa uchunguzi, hili la zanzibar ndo kwanza limetokea , kwa hiyo huwezi kukimbilia kusema ni ugaidi kabla ya kuwa na ushahidi huo.
 
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi amesema tukio la kumwagiwa tindikali kwa raia wawili wa Uingereza sio la kigaidi. "matukio haya yasichukuliwe jumla jumla, sisemi moja kwa moja kuwa tukio hilo ni la kigaidi ila naomba tuhamasishe jamii ya watanzania utii wa sheria bila shuruti, na tusaidie vita dhidi ya matumizi mabaya ya tindikali" - Alikuwa anajibu swali kama tukio la Tindikali nalo ni la kigaidi kama yale aliyopitisha ofisini kwake yafunguliwe mashtaka ya Ugaidi yaliyokataliwa na Mahakama

IGP- Amekwepa swali la kuwa endapo yupo tayari kujiuzulu kwani matukio mabaya yamekuwa yakiendelea tu.
"Kwanini usijiuzulu kwa kuwa matukio kama haya yamekuwa yakijirudia, na wewe umekalia kiti hicho?"

Hayo yamejiri kwenye ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani muda mchache kulikuwa na Press conference, Wazungumzaji walikuwa ni IGP, DPP na Mkemia Mkuu wamechanganyikiwa na tukio la Waingereza kumwagiwa Tindikali. Pamoja na hayo, hoja yangu je Serikali inaamka wageni wakiguswa? tangu lini matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameanza kutokea na serikali haichukui hatua, wala kukamata watuhumiwa. Mabomu yamelipuka hatujawahi kusikia serikali ikitoa maelezo na namna ya kujilinda. Leo la tindikali la Waingereza IGP, DPP na Mkemia Mkuu wanafika kueleza namna ya kudhibiti tindikali, na namna ya kupata taaarifa za tindikali.

Nasubiri kuiona na kusikiliza hiyo press conference. Ni kwa nini DPP amekuwa na haraka ya kutoa maamuzi kuwa kitendo hicho siyo ugaidi? Inaniwia vigumu kukubaliana naye kwa sababu ikiwa watendaji nia yao ni kuwaogopesha wageni wasije Tanzania sioni tafasiri ingine zaidi ya ugaidi.
 
Naona lile somo la Jaji wa Igunga limewaingia sawasawa, Jaji aliwaambia msipende kuhusisha kila tukio na ugaidi mtaharibu taswira nchi.

Kama mnaweza mngeendelea na cd yenu ya ugaidi muone waingereza wanavyowaisaidia kuipa promo ya hali ya juu.!!
 
Feleshi haueleweki baadae utakuja kusema la kigaidi kama vp njoo ule eid home:
=============
Mualiko wa EID:
Nakualika uje wewe na rafiki yako katika sikukuu ya EID nyumbani kwetu, Nakutegemea kama Rafiki wa karibu, Panda gari la gongo la mboto shuka gongo la mboto mwisho alafu chukua magari ya Pugu kajiungeni shuka mwisho wa gari halaf panda vigari vya kwenda kisarawe teremka kwa sangita, ukifika chukua bajaj mwambie akulete kwa mama davina kisha panda pikipiki mpaka Kisarawe social hall ukifika kuna baiskel mwambie akulete hadi Uwanja wa somji, ukifika angalia mbele kuna kanisa pita kichochoro mbele utaiona shule ya msingi Ndama, Nyuma ya shule ndo kwetu Karibu Ndugu yangu.
 
Kwa kuwa wamemwagiwa wazungu hilo tukio si la kigaidi hao waliomwaga si magaidi,lakini Mwigulu kutangaza tu kuwa eti CHADEMA imemmwagia tindikali huyo jamaa aliyemwagiwa na green guard fasta DPP akafungua kesi ya ugaidi kwa wana chadema.Huyu jamaa ni hamna kitu ni debe tupu kichwani anaendeshwa na CCM na si taaluma yake!!!!
 
Kama uchunguzi ungekuwa umefanyika na ikajulikana kuwa ni swala la kupangwa na kundi la watu tungeita ni ugaidi lakini uchunguzi bado haujafanyika.

Kama uchunguzi haujafanyika kwa nini mukurupuke kusema sio ugaidi.?

Tatizo viongozi wetu wengi wanaendeshwa na wanasiasa aina ya Mwigulu na kudhalilisha taaluma zao.!!
 
Tuna viongozi wa kukurupuka na kupangiwa ya kusema; anajuaje Kama ni ugaidi Au la kabla hata wahusika hawajakamatwa!
 
kwa kuwa suspects sio chadema tukio hili haliwezi kuwa la kigaidi.
ndio maana tunasisitizwa kuwa kabla ya kuchukua uamuzi wa kuongea kitu tena hadharani inabidi kufikiri japo kidogo. Hizi kauli za huyu mkuu zinanikumbusha IGP Omari Mahita na visu vya CUF, chukulia isiengelisemaga hivyo unadhani heshima yake ingelikuwa kama hivi leo japo kastaafu!?
 
Back
Top Bottom