DDP: Tukio la tindikali Zanzibar sio ugaidi

DDP: Tukio la tindikali Zanzibar sio ugaidi

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi amesema tukio la kumwagiwa tindikali kwa raia wawili wa Uingereza sio la kigaidi. "matukio haya yasichukuliwe jumla jumla, sisemi moja kwa moja kuwa tukio hilo ni la kigaidi ila naomba tuhamasishe jamii ya watanzania utii wa sheria bila shuruti, na tusaidie vita dhidi ya matumizi mabaya ya tindikali" - Alikuwa anajibu swali kama tukio la Tindikali nalo ni la kigaidi kama yale aliyopitisha ofisini kwake yafunguliwe mashtaka ya Ugaidi yaliyokataliwa na Mahakama

IGP- Amekwepa swali la kuwa endapo yupo tayari kujiuzulu kwani matukio mabaya yamekuwa yakiendelea tu.
"Kwanini usijiuzulu kwa kuwa matukio kama haya yamekuwa yakijirudia, na wewe umekalia kiti hicho?"

Hayo yamejiri kwenye ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani muda mchache kulikuwa na Press conference, Wazungumzaji walikuwa ni IGP, DPP na Mkemia Mkuu wamechanganyikiwa na tukio la Waingereza kumwagiwa Tindikali. Pamoja na hayo, hoja yangu je Serikali inaamka wageni wakiguswa? tangu lini matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameanza kutokea na serikali haichukui hatua, wala kukamata watuhumiwa. Mabomu yamelipuka hatujawahi kusikia serikali ikitoa maelezo na namna ya kujilinda. Leo la tindikali la Waingereza IGP, DPP na Mkemia Mkuu wanafika kueleza namna ya kudhibiti tindikali, na namna ya kupata taaarifa za tindikali.

Wala sishangai, UGAIDI wanafanya CDM wakiandamana. hawakusema kuwa FBI na CIA wapo nchi kusaidia kama ilivyokuwa kule Arusha???????????
 
Nadhani ni mapema kuhusisha tukio la zanzibar na ugaidi, tuvipe vyombo vya dola muda ya kujiridhisha ili tupate taarifa iliyokamilika.

Nini maana ya Ugaidi? Gaidi ni nani? Matendo ya Kigaidi ni ya aina gani?
 
ndio maana tunasisitizwa kuwa kabla ya kuchukua uamuzi wa kuongea kitu tena hadharani inabidi kufikiri japo kidogo. Hizi kauli za huyu mkuu zinanikumbusha IGP Omari Mahita na visu vya CUF, chukulia isiengelisemaga hivyo unadhani heshima yake ingelikuwa kama hivi leo japo kastaafu!?

Kwenye nyekundu hapo, lugha gani hiyo?
 
Nini maana ya Ugaidi? Gaidi ni nani? Matendo ya Kigaidi ni ya aina gani?

pole sana mkuu, ugaidi siyo kwa sababu ya TINDIKALI, uchunguzi wa namna Tindikali hiyo ilivyotumika ndiyo unaweza kutoa tafsiri kama tukio ni la kigaidi au la.
 
Magamba on work!!!!!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
nafikiri dr slaa na lwakatare wanajua zaidi wapi inapatikana maana ni miongoni mwa silaha baridi wanazotumia kujijenga kisiasa
Maboss wako wamesema kumwagiwa Tindikali wale waingereza sio ugaidi-Tunajua palipo na mtu wa CDM ndio huwa ugaidi.Kwenye hili mtakuwa mmekosea mkadhani wanachama wa IYDA waliokuwa pale DAr, Mmebugi na msaada ndio basi. Najeti ya 85% dependent kwa wahisani mwaka huu hakuna.
 
Daaah hii nchi ngumu sana,tuvumiliane tu hivyo hivyo 2015 sio mbali jamani.
 
Hakuna uhuru wa mawazo nchi hii. Tindikali ya mtu wa magamba mnasema ugaidi ya wazungu sio ugaidi. Hamnazo kweli nyie, mnapelekwapelekwa tu kwa kuwekewa maneno ya kusema. Hakuna cha DPP, TAKUKURU wala IGP wote mmefungwa gavana.
 
Mkuu mimi nakuwa kinyume kabisa na wewe kwa sababu inawezekana kabisa kujihusisha kwetu na usuluhishi wa nje kukawa sababu ya kushambuliwa ili na sisi tuonekane hatuna amani , nasema hivyo kwa sababu Tanzania haikuanza leo kusaka amani katika mataifa jirani, wakati matukio ya kumwagiana tindikali ni ya juzi tu na hayana muda mrefu.

Una uhakika na ulichokiandika?
 
Kama uchunguzi ungekuwa umefanyika na ikajulikana kuwa ni swala la kupangwa na kundi la watu tungeita ni ugaidi lakini uchunguzi bado haujafanyika.

Kwa iyo unadhan walikurupuka kuwamwagia au walijipanga!
Hii ni dalili ya elimu ya chuo hii.
 
Nakumbuka kuna mtalii aliuawa Serengeti, vyombo vyote vya ulinzi vilienda tena kwa helikopter.
Mchina alipouawa na wachina kufunga barabara, ilibidi vyombo vyote vya ulizi viende vikawaombe msamaha.
Kwa albino , sio ishu saana.
 
kama sio UGAIDI ilikuwaje huyu huyu DDP akawafungulia mashitaka ya ugaidi wafuasi wa CDM wanaotuhumiwa kumumwagia tindikali kada wa CCM Mussa Tesha?!

Huyu DPP hafai kabisa anatumika KISIASA, shame on your face Feleshi
Tumuombe Mwigulu awaelekeze kama ni ugaidi au nini? Maana wanapokea maelekezo toka kwake,
 
Maneno kama hayo uliyoyaandika yanwaudhi sana TCRA, kama hauna hoja bora ukakaa kimya mkuu, Mods wanaweza kukusaidia kama itabidi.

Kipi kinachoudhi zaidi: Watu kumwagiwa tindikali, watu kubambikiwa kesi za ugaidi au dpp kuitwa kenge maji? You have to think twice dude!
 
Mhhh.... Tanzania???.

Siungi mkono na Nashanga kwa nini Watanzania tunamwagiana kemikali! Kwa nini serikali ya vyombo vyake havichukui hatua zinazonekana na zenye kukomesha matukio haya? Je, vyombo vya dola vimeshindwa kazi? Kimsingi yanayoendelea ndani ya Taifa hili yanathibitisha viongozi kushindwa kazi. Na je, kwa nini viongozi hawawajibiki kitaaluma au kisiasa pale wanaposhindwa kuzuia vitendo viovu ndani ya jamii waliyoapa kuilinda? Je, viongozi hawa wanaaminiwa na Watanzania walio wengi? Kama jibu ni hawaaminiwi na vitendo viovu vinazidi kuota mizizi kwa nini hawang'atuki? Kwa nini wang'ang'anie madaraka waliyoshindwa kutekeleza?

Ni matukio mangapi yametokea ya kumwagikiwa tindikali yameripotiwa mpaka sasa? Ni mangapi kati ya hayo hayakuitwa ya Kigaidi?

Kwa taarifa hii DPP, IGP na Mwanasheria Mkuu wana maanisha nini kusema kuwa kitendo hicho cha kumwagia Tindikali huko Zanziba hivi karibuni kuwa siyo cha Kigaidi? Je, hii inamaana sasa Viongozi hao wame elewa maana ya neno gaidi na matukio ya namna hiyo? Je, wamepata kuelewa hivyo baada ya hakimu kutoa somo kule Tabora? Je, kwa nini watu hushitakiwa kwa matukio yanayofanana na hilo lakini hali NA TAFSIRI VIWE TOFAUTI kwa hili linalohusu raia wa nje? Je, hii kwa watu wanaopenda kuchambua mambo ina maana gani?

1. Je, nikuficha ukweli ili kutochafua sura ya Nchi Kimataifa kwamba Tanzania kuna matukio ya Kigaidi?
2. Je, kama 1 hapo juu ni sahihi, kwa nini tuthamini ya nje kuliko ndani?
3. Maana yake ni kuwa utu wa Mtanzania hauna thamani nchini kwake? Nani atajali utu wetu kama sisi hatujijali?
4. Kwa nini viongozi wetu wajali watu wa nje kuliko wa ndani? Hili limeota mizizi kila Nyanja, mfano Uwekezaji nk??
5. Kama moja ni sahihi je, hii inatusaidia sisi kama taifa? Hii si sawa na kuficha maradhi?
6. SERIKALI LAZIMA IFANYE KAZI. USIRI HAUTAJENGA NCHI. UNAFIKI HAUTUSAIDII. UKWELI DAIMA UKO WAPI?

Nadhani tumeshazidi mahali pa kusema sasa umwagianaji wa Tindikali basi WATOSHA! Kwa nini tunalea mambo?
 
Nadhani ni mapema kuhusisha tukio la zanzibar na ugaidi, tuvipe vyombo vya dola muda ya kujiridhisha ili tupate taarifa iliyokamilika.
Unachoongea ni sahihi lakini suala linakuja kwa huyu DPP tunajiuliza maswali mengi Sakata la Lwakatare alitumia Clip ya video ya kwenye Youtube kumuandalia Lwakatare mashitaka ya Ugaidi, sakata la Tindikali kwa Musa Tesha aliandaa mashitaka ya Ugaidi kwa wale wafuasi wa CDM na leo hii anakuja kusema sakata la Tindikali kwa wale mabinti sio Ugaidi why?
 
Wakuu ninaomba kuelewa: Tindikali inapatikana wapi? Ni nani anaeruhusiwa kuwa nayo kihalali? Je matumizi yake halali ni yapi?

inapatikana maduka ya vifaa vya maabara, inatumika maabara. Shule zote za sekondari zenye maabara zinazo
 
Back
Top Bottom