A
Anonymous
Guest
Sisi Wakazi wa Lugagala tunanyanyasika sana ikiwemo kufanyiwa fujo katika mashamba na makazi yetu ya asili. Mpaka wa Vijiji hivii umekuwa kero kwa Watendaji wa Halmashauri Wilaya ya Songea.
Licha ya kukumbushia mgogoro huu wa barua mbalimbali katika ngazi ya Halmashauri kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Songea hakuna mafanikio yoyote.
Wanakijiji wa Zomba wamevuka mpaka na kuuza kwa wageni mashamba ya Lugagala wakishirikiana na mwenyekiti na diwani ambaye anaishi Zomba. Jamani tusisubiri maafa tunaomba mkuu wa wilaya tuma timu ya ardhi ikatafsiri mpaka wala sio kurekebisha mpaka kama viongozi wa Zomba wanavyodai.
Maana wanasema wamewaweka mfukoni watu wa ardhi wa halmashauri ambao wanashikirikiana na diwani kukataa kwenda kusoma mpaka kwa kuwa diwani anatoka Kijiji cha Zomba. Mpaka wa vijiji hivi una point tatu tu 181 ya Kaskazini 186 ipo katikati na 185 ipo Kusini.
Mara ya kwanza wakimtumia Afisa Tarafa Mstaafu walifoji barua wakasema mpaka umetatuliwa wala hiyo barua haikufika kwa Mkuu wa Wilaya. Mara ya pili watu wa Zomba wakafanya fujo kwa kuwa wakati wa zoezi la uhakiki ilionyesha wamevamia Zaidi ya kilometa tano kutoka mpaka halisi. Maombi yetu Mkuu wa Wilaya usimamie hizi zoezi na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ili kuhakikisha hakuna fujo.
Pia, tunaomba washikirikishwe tu watu wachache kama Watendaji wa Vijiji vyote, wenyeviti wa vyote, na kamati yako kutoka wilayani, wala sisi wanachi tusiwepo tusionekana tunavutia upande wa kwenye mashamba yetu yaliyouzwa na mwenyekiti wa Zomba.
Tunajua wewe Mkuu wa Wilaya ni msikivu na ni mchapakazi ila tu watendaji wako wa ardhi kwa kuwa wamewekwa mfukoni na viongozi wa muongano wakiongozwa na Mwenyekiti wao.
Viongozi wa ardhi halmashauri ukiwauliza wanatoa visingizio ambavyo hata Jeshi la Polisi Wilaya hawana taarifa kama walitishiwa usalama kipindi cha kutafsiri huo mpaka wa vijiji hivi viwili. Tunatanguliza shukrani zetu za dhati sisi Wanakijiji wa Lugagala.