DC wa Iramba ajitumbua mwenyewe

Chief wa kibena

JF-Expert Member
Mar 13, 2016
686
394
Katika hali isiyotarajiwa DC wa Iramba Lucy Mayenga ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu amuomba Rais amuache kwenye uteuzi wa wakuu wa wilaya kwani ukuu wa wilaya umemsababishia biashara zake huko Shinyanga kwenda vibaya.

Hii aliongea wakati alipokutana na UWT huko Shinyanga ambapo inasemekana Waziri Mkuu alivyopita pande hizo Mkuu huyo wa Wilaya alimuomba Waziri Mkuu amwambie Rais asimteue tena.

Mheshimiwa Waziri Mkuu akamwambia asubirie uteuzi mpya na amesema isitafsiriwe kuwa ameshindwa kwenda na kasi ya Rais.

My take:
Inawezekanaje mteule wa Rais aseme sasa kuwa biashara zake zinaenda vibaya kisa ukuu wa wilaya? Je hapo mwanzo hakuliona hilo?
Source: magazeti ya leo.
 
Automatically Lucy anakosa sifa kutokana na sheria ya Utumishi wa Umma unaomtaka mfanyakazi kuacha kazi ya serikali Mara akishateuliwa kuwa mbunge na NEC

Kwa hiyo ameona hilo ndio maana ameamua kuomba na asingeweza kuendelea kutokana na sheria hiyo iliyoanza kutumika mwaka Jana!
 
Mwaka huu hakuna kubebana vyeo 2 mtu mmoja! Wabunge wote wataukosa u DC: Kina Stella Manyanya na wengine walibebwa sana maana walikuwa wanavuta mishahara 2!
 
Ameangalia mbali hali ya hewa sio inabidi tu ajiweke kando maana hakuna namna.

katika hali isiyo tarajiwa DC wa iramba Lucy mayenga ambaye pia ni mbunge wa viti maalumu amuomba rais amuache kwenye uteuz wa wakuu wa wilaya. kwani ukuu wa wilaya umemsababishia biashara zake huko shinyanga kwenda vibaya, hii aliongea wakati alipokutana na uwt huko shyinyanga. inasemekana WAZIRI MKUU alivyopita pande hixo mkuu huyo wa wilaya alimuomba waziri mkuu amwambia rais asimteue tena, mh wazir MKUU akamwambia asubirie uteuz mpyya, na amesema isitafsiriwe kuwa ameshindwa kwenda na kas ya mh.

my take!! inawezekanaje mteule wa Rais aseme sasa kuwa biashara zake zinaenda vibaya kisa ukuu wa wilaya hapo mwanzo hakuliona hilo.
source magazet ya leo
 
Mnataka kusema bi faiza foxy aliambulia nini kwa kumtetea wa dini yake miaka yote? Au ndo kuwa tu nyumba ndogo ya kiimani tu basi? Maana sijamsikia kwenye ubunge,ukuu wa wilaya labda tusubiri ukuu wa wilaya. Though kwa Dr Magufuli sidhan maana Huyu Dr aliyeenda shule kiukwel ana nia ya dhati ya kulikomboa taifa hili lililohujumiwa kwa miaka 10
 
Uwe na biashara Shinyanga halafu upewe U DC wilaya yoyote nje ya mkoa huo, ni wazi kwamba biashara hiyo utanufaisha watu wengine tu. Mshika mawili...
 
Back
Top Bottom