DC wa CCM amtapeli kimada wake mamilioni ya fedha

DC wa CCM amtapeli kimada wake mamilioni ya fedha

Huy mwanamke atakuwa ni Mchagga.
Ungemalizia kabisa kwamba Mchagga na ni mkristo! Anyway, jadiri sasa topic iliopo, mkuu wa wilaya kamtapeli hawala yake, hilo likoje? Kumbuka pia mkuu huyo wa wilaya anatokea kwenye kile kile chama ukipendacho.
 
Akili yako ina matege..
Wezi wapo chadema na hawataki kuhojiwa. Mbowe anachota mamilioni ya
ruzuku anaenda kununua majumba dubai, slaa anajichotea ruzuku ya chama
anaenda kuvinjari na hawara ulaya. Jiulize kwanini hawataki kujibu hoja
za mwigamba na zile za mkakati wa mabadiliko 2013

Wew ni mla vya MaCCM na yaweza kuwa pesa za kifisadi zimekukuza ndio maana unatetea wizi wa hao ndugu zako,
 
Ungemalizia kabisa kwamba Mchagga na ni mkristo! Anyway, jadiri sasa topic iliopo, mkuu wa wilaya kamtapeli hawala yake, hilo likoje? Kumbuka pia mkuu huyo wa wilaya anatokea kwenye kile kile chama ukipendacho.

Hajatapeliwa huyo kaona kapigwa kibuti sasa ana-haha.
 
Huyu mwanamke hazimtoshi unakopaje hela hili umfurahishe bwana.
Huko kwenye taasisi zinazokopesha hawaelezwi madhumuni ya mikopo.
Ina maana wakati anaenda kukopa kwa niaba ya huyo bwana, Kumchaya alikuwa hakopesheki?.
Atuache tuendelee kuombeleza kifo cha Madiba wetu,yeye aendeleze pillow talk na Kumchaya.

mkuu, huyu kimada alikuwa anapalilia penzi. mapenzi ya siku hizi ni aghali kuliko unavyoweza kudhani.
 
Mleta mada amevurugwa kweli kweli. Naamini amekunywa gongo asbh ndio imemfikisha hapo.

ccm haina mkuu wa wilaya.

umekunywa maji ya chooni? kwani huyo mkuu wa wilaya umeambiwa ni wa CHADEMA au CUF?
 
Hata kama chanzo ni Nipashe Jumapili, wewe umeiweka hapa pashakuwa Gazeti la udaku hapa JF? unadhani hapa ni ijumaa weekenda? au risasi?
 
Hata kama chanzo ni Nipashe Jumapili, wewe umeiweka hapa pashakuwa Gazeti la udaku hapa JF? unadhani hapa ni ijumaa weekenda? au risasi?

unasemaje? kwani habari zilizopatikana kwenye chombo kingine cha habari haziwezi kuingia humu? kama huna cha kuongea si ukae kimya tu?
 
Akili yako ina matege.. Wezi wapo chadema na hawataki kuhojiwa. Mbowe anachota mamilioni ya ruzuku anaenda kununua majumba dubai, slaa anajichotea ruzuku ya chama anaenda kuvinjari na hawara ulaya. Jiulize kwanini hawataki kujibu hoja za mwigamba na zile za mkakati wa mabadiliko 2013
Wewe akili yako isiyokuwa na matege, unashindwa nini kujiuluza"kwa nini serikali ya CCM haichunguzi huo ufisadi uliosema? CDM wanapokea ruzuku toka serikali, CDM kimesajiriwa na serikali ya CCM, kwanini serikali inaogopa kuwafuashitaka Mbowe na Slaa? Acha kufikiria kwa kutumia makalio yako FOOL
 
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini , Suleiman Kumchaya, ameingia kwenye kashifa nzito ya kumtapeli mama mmoja fedha taslimu kiasi cha Sh. milioni 50.

Kumchaya ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Betty Matemba, anadaiwa kufanya utapeli huo katika vipindi tofauti mara baada ya kushindwa ubunge 2010.

Akizungumza na gazeti hili, Betty alisema Kumchaya wakati akiwa mbunge walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na walikuwa wakiishi kama mtu na mumewe.

Unajua huyu bwana alikuwa mshauri wa Rais Mkapa, baadaye aligombea ubunge katika kipindi cha awamu ya kwanza ya serikali ya Rais Kikwete na alishinda lakini awamu ya pili hakuweza kupata.

Wakati akiwa ni mbunge, bado alikuwa na uwezo mdogo sana kifedha, alinishawishi kumkopea fedha benki lakini siku zinavyokwenda mwenzangu hata halipi deni ndiyo nikachukua uamuzi wa kwenda bungeni ili akatwe marupurupu yake ya ubunge lakini ikaonekana hakuwa na hata senti mmoja, alisema Betty.

Kwa mujibu wa Betty, mkuu huyo wa wilaya alipomaliza kipindi chake cha ubunge, maisha yake yakawa magumu kwani hakuwa na fedha wala mradi ingawa alikuwa akimiliki mamia ya ekari.

Anao uwezo wa kunilipa, anazo ekari 60 za mikorosho Mtwara Vijijini, ekari 500 za ardhi huko Nachingwea akiziuza ni rahisi yeye kunilipa lakini anachonifanyia ni uhuni.

Awali tulikubaliana anilipe fedha hizo ili nilipe madeni yote ninayodaiwa, alisema. Akiwa na makabrasha yanayoonyesha michanganuo ya fedha alizomtapeli, Betty anasema baada ya kupata ukuu wa wilaya alianza kumlipa kidogo kidogo ambapo Juni 28 mwaka jana alilipa Shilingi milioni moja na Julai 31 mwaka jana, alilipa Shilingi milioni moja na baada ya hapo hakuendelea tena.

Alisema wakati fulani walishauriana yeye (Betty) na Kumchaya wanunue vigari vidogo vya mizigo ili vimsaidie kusogeza maisha yake.

Ilishindikana kununua hiyo gari kwani fedha ninayoitegemea ndiyo hiyo Jumamosi (jana) kuna uwezekano wa kuondolewa kwenye nyumba niliyopanga Sinza kwani nimepandishiwa kodi na sina uwezo, alisema na kuongeza kuwa kodi ya mwaka anatakiwa kulipia Sh. milioni 3.6 na kwamba mwenye nyumba tayari ameshamkabidhi barua ya kuondoka.

Betty alisema fedha hizo alitarajia kununua nyumba ambayo wakati huo ilikuwa ikiuzwa Sh. milioni 70 lakini kutokana na mheshimiwa huyo kumrubuni, ilishindikana.

Alisema kutokana na jinsi alivyokuwa akimsumbua (Kumchaya) kulipa deni hilo, mkuu huyo wa wilaya alianza kutumia nguvu za giza.

Kumchaya akiwa na mkewe mwingine Mpemba na rafiki yangu mmoja na mumewe, walikwenda Mbagala kwa mganga wa kienyeji wakitaka kuniua au kunifanya kichaa.

Huyu mganga nilikuwa si mfahamu, lakini alipata namba yangu akanipigia akitaka nimuonenilikwenda na wifi yangu (dada yake Kumchaya), tulipofika alinieleza yote pamoja na fedha aliyolipwa...," alisema.

Dada yake Kumchaya , alilipopigiwa simu kutoka Masasi, alikiri kutambua uhusiano uliopo wa Betty na Kumchaya.
huyu Betty ni wifi yangu kabisa, mkewe Selemani, ni wifi yangu ninayempenda sana.

Ni kweli Kumchaya na mkewe Fatma walikwenda kwa huyo mganga huko Dar es Salaam wakitaka kumroga Betty. Huyu mganga alimvuta Betty kimadawa hadi alipompata na siku hiyo tulikwenda wote kwa huyo mganga. Betty Mungu anampenda sana...," alisema Mwajuma kwa lafudhi ya Kimakonde.

Miongoni mwa fedha ambazo Betty anadai kuzikopa kwenye taasisi za fedha kwa ajili ya kumridhisha Kumchaya ni pamoja na Shilingi milioni saba (NMB), Shilingi milioni tisa (International Bank), Shilingi milioni 10 (Akiba Commercial) na Shilingi milioni 4.2 (Vission Saccos), hizo ni mbali na zile alizokopa kutoka kwa watu binafsi.

Ilifikia kipindi aliniomba nikope Sh. milioni tisa kwa ajili ya kufanyia harusi ya mtoto wake, nilifanya hivyo na harusi ilikuwa nzuri sana.

Nilipoona hana muelekeo wa kulipa madeni hayo ilibidi tuandikishiane, alisema huku akionyesha nyaraka hizo.

Betty anasema pamoja na kumuitia wazee wa heshima na viongozi wa dini ya Kiislamu ili wazungumze na Kumchaya alipwe deni lake, ilishindikana kabisa.

Mimi sina ugomvi na huyu bwana, ninachotaka anilipe deni langu tu ili tuishi kwa amani, alisema.

Mkuu wa Wilaya, Kumchaya alipotafutwa kwa siku tatu mfululizo kwa simu akiwa Tabora, alisema yuko kwenye kikao apigiwe baadaye lakini alipopigiwa simu yake ilikuwa ikiita bila majibu.

Unajua huyu mwanamke anakichaasubiri niwasiliane na mwanasheria wangu nipigie baadaye, alisema.

Hata hivyo, mwandishi wa habari hizi alipoendelea kumpigia simu yake ya mkononi, iliita bila majibu.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI :sad:
Huyu mwanamke sio kichaa ila hayuko sawa. She is insane!.
Kukopeshana mkoposhane kwenye mapenzi, lakini kudaiana ndio mje magazetini!.

Kiukweli ni kwa wasio jua tuu ndio wataamini lengo huyo dada kwenda kwenye media ni ili alipwe deni lake!, ukweli huyo dada kilichomuumiza ni kukosa penzi tuu la huyo jamaa, ili kumwadhibu, ameamua kumchafua!. Mtu anayedai deni lake kihalali anajua mahali pa kwenda na sio kwenye media!.

Ukiona mwanamke aliyekuwa kimada tuu, akijinasibisha kuwa tumeishi wote kama mume na mke ili hali anajua kabisa huyo mwanamume ni mume wa mtu, then mwanamke huyo anakuwa hayuko sawa!.

Suleimam Kumchaya namfahamu toka akiwa mtangazaji wa RTD, ni mtu mstaarabu sana!, hakustahili kutendwa haya na mwanamke!, kama ni kusaidiwa na wanawake, mbona wengi tuu tumesaidiwa!, wengine hadi kujengewa nyumba na kununuliwa magari in the name of love!. Leo penzi limegeuka inageuka deni la kutangaziana magazetini!.

Japo siujui mwanzo wa uhusiano wao, kwa mujibu wa hii picha, hii ndio ile miajianamke inayojitongozesha yenyewe kwa wanaume kwa jeuri ya pesa, ikiamini money can buy love!, mwanaume katumia pesa yake na ameopota kabinti kazuri ka Kipemba, hakana kitu!, jimama linashangaa kuachwa na mijipesa yote lililomvest kwenye love!, ndio linapeleke maumizi magazetini kujifariji!.

Enyi wanaume wenzangu, baadhi ya wanawake ni vichaa wa mapenzi, ukifuatwa na vichaa hao, atakupa kila unachotaka, ili siku akiachwa!, jua shughuli unayo!.
Pasco
 
Shit for shit either communion or confession!!!!!!
(Pippi De Lena et al..in The Last Don by Mario Puzo 1996)
 
Kumchaya kamroga huyu betty mpaka akawa anatoa mamilion,dawa imeisha ndio betty kastuka,hivi sinza kupanga nyumba nzima kodi kwa mwaka sh. 3.6m? Au ni sinza ile ya Tandale/Manzese?

Itakuwa ndio huko uzuri..tandale..na manzese
 
Back
Top Bottom