DC wa CCM amtapeli kimada wake mamilioni ya fedha

Sasa ukopeshane pesa na mtu(Mpenzi kama kweli) kimya kimya mnaoshindwa kulipana mnakuja JF ili tufanyeje? thats rubbish!
 
Kidumu chama cha mapinduziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!
 
Kumchaya kamroga huyu betty mpaka akawa anatoa mamilion,dawa imeisha ndio betty kastuka,hivi sinza kupanga nyumba nzima kodi kwa mwaka sh. 3.6m? Au ni sinza ile ya Tandale/Manzese?

Hiyo ni kodi ya chumba kimoja na ukumbi nachomlipia mdogo wangu hapo Sinza,
 
Huy mwanamke atakuwa ni Mchagga.


aisee, hivi walitaja na kabila lake kumbe? kumbe yawezekana na dini zao zimetajwa, nazo utakuwa umeziona, wala hatuzihitaji kwani hazitusaidii, mshaurini tu DC arudishe mkopo kwa kuepuka aibu hizi kwa chama
 
Wanywa gongo wenzako ndio wataamini huu uzushi

Hebu tulia gamba, huyo DC aliyemtapeli Mwl nyumba yake ipo hapa Masasi mtaa wa Mtandi kbarabara ya kuelekea Mtandi mission hospital na mwl aliyemtapeli anafundisha S/M MIGONGO ni PM nikupe na namba za huyo Mwl aliyetapeliwa na DC wenu yaani ni majanga
Acha kiburi gamba
 
Kumchaya ni fisadi la kimapenzy. Kwanini hasa linataka kufaidi vyote---mbunye na rupia? Mtaka vyote hukosa vyote--kama hili fisadi litaendelea kufisidi mbunye na rupia za vimada kama hivi, linaweza kujikuta zinalitokea puani siku moja. Lisemwalo lipo.....
 
Betty huyu nadhani ni majina tu!Betty Machangu ni mbunge vitu maalum!

Kumchaya ni DC wa Tabora lakini si kwao kule!yeye anatokea Ntwara huko!

Kumchaya anaishi maisha ambayo sio yake!ashukuru huruma ya JK ama la saa hizi angekuwa jela kwa utapeli wake!wanajifanya usalama wa taifa wanapita kuomba na kukopa pesa mitaani!njaa mbaya sana
 
Kwanza hivi vyeo vya uDC vifutwe kwenye katiba mpya--pesa za umma zinapotea bure kuwagharamia hawa mchwa wasiokuwa na tija yoyote kwenye taifa hili.
 
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini , Suleiman Kumchaya, ameingia kwenye kashifa nzito ya kumtapeli mama mmoja fedha taslimu kiasi cha Sh. milioni 50.

Kumchaya ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Betty Matemba, anadaiwa kufanya utapeli huo katika vipindi tofauti mara baada ya kushindwa ubunge 2010.

Akizungumza na gazeti hili, Betty alisema Kumchaya wakati akiwa mbunge walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na walikuwa wakiishi kama mtu na mumewe.

Unajua huyu bwana alikuwa mshauri wa Rais Mkapa, baadaye aligombea ubunge katika kipindi cha awamu ya kwanza ya serikali ya Rais Kikwete na alishinda lakini awamu ya pili hakuweza kupata.

Wakati akiwa ni mbunge, bado alikuwa na uwezo mdogo sana kifedha, alinishawishi kumkopea fedha benki lakini siku zinavyokwenda mwenzangu hata halipi deni ndiyo nikachukua uamuzi wa kwenda bungeni ili akatwe marupurupu yake ya ubunge lakini ikaonekana hakuwa na hata senti mmoja, alisema Betty.

Kwa mujibu wa Betty, mkuu huyo wa wilaya alipomaliza kipindi chake cha ubunge, maisha yake yakawa magumu kwani hakuwa na fedha wala mradi ingawa alikuwa akimiliki mamia ya ekari.

Anao uwezo wa kunilipa, anazo ekari 60 za mikorosho Mtwara Vijijini, ekari 500 za ardhi huko Nachingwea akiziuza ni rahisi yeye kunilipa lakini anachonifanyia ni uhuni.

Awali tulikubaliana anilipe fedha hizo ili nilipe madeni yote ninayodaiwa, alisema. Akiwa na makabrasha yanayoonyesha michanganuo ya fedha alizomtapeli, Betty anasema baada ya kupata ukuu wa wilaya alianza kumlipa kidogo kidogo ambapo Juni 28 mwaka jana alilipa Shilingi milioni moja na Julai 31 mwaka jana, alilipa Shilingi milioni moja na baada ya hapo hakuendelea tena.

Alisema wakati fulani walishauriana yeye (Betty) na Kumchaya wanunue vigari vidogo vya mizigo ili vimsaidie kusogeza maisha yake.

Ilishindikana kununua hiyo gari kwani fedha ninayoitegemea ndiyo hiyo Jumamosi (jana) kuna uwezekano wa kuondolewa kwenye nyumba niliyopanga Sinza kwani nimepandishiwa kodi na sina uwezo, alisema na kuongeza kuwa kodi ya mwaka anatakiwa kulipia Sh. milioni 3.6 na kwamba mwenye nyumba tayari ameshamkabidhi barua ya kuondoka.

Betty alisema fedha hizo alitarajia kununua nyumba ambayo wakati huo ilikuwa ikiuzwa Sh. milioni 70 lakini kutokana na mheshimiwa huyo kumrubuni, ilishindikana.

Alisema kutokana na jinsi alivyokuwa akimsumbua (Kumchaya) kulipa deni hilo, mkuu huyo wa wilaya alianza kutumia nguvu za giza.

Kumchaya akiwa na mkewe mwingine Mpemba na rafiki yangu mmoja na mumewe, walikwenda Mbagala kwa mganga wa kienyeji wakitaka kuniua au kunifanya kichaa.

Huyu mganga nilikuwa si mfahamu, lakini alipata namba yangu akanipigia akitaka nimuonenilikwenda na wifi yangu (dada yake Kumchaya), tulipofika alinieleza yote pamoja na fedha aliyolipwa...," alisema.

Dada yake Kumchaya , alilipopigiwa simu kutoka Masasi, alikiri kutambua uhusiano uliopo wa Betty na Kumchaya.
huyu Betty ni wifi yangu kabisa, mkewe Selemani, ni wifi yangu ninayempenda sana.

Ni kweli Kumchaya na mkewe Fatma walikwenda kwa huyo mganga huko Dar es Salaam wakitaka kumroga Betty. Huyu mganga alimvuta Betty kimadawa hadi alipompata na siku hiyo tulikwenda wote kwa huyo mganga. Betty Mungu anampenda sana...," alisema Mwajuma kwa lafudhi ya Kimakonde.

Miongoni mwa fedha ambazo Betty anadai kuzikopa kwenye taasisi za fedha kwa ajili ya kumridhisha Kumchaya ni pamoja na Shilingi milioni saba (NMB), Shilingi milioni tisa (International Bank), Shilingi milioni 10 (Akiba Commercial) na Shilingi milioni 4.2 (Vission Saccos), hizo ni mbali na zile alizokopa kutoka kwa watu binafsi.

Ilifikia kipindi aliniomba nikope Sh. milioni tisa kwa ajili ya kufanyia harusi ya mtoto wake, nilifanya hivyo na harusi ilikuwa nzuri sana.

Nilipoona hana muelekeo wa kulipa madeni hayo ilibidi tuandikishiane, alisema huku akionyesha nyaraka hizo.

Betty anasema pamoja na kumuitia wazee wa heshima na viongozi wa dini ya Kiislamu ili wazungumze na Kumchaya alipwe deni lake, ilishindikana kabisa.

Mimi sina ugomvi na huyu bwana, ninachotaka anilipe deni langu tu ili tuishi kwa amani, alisema.

Mkuu wa Wilaya, Kumchaya alipotafutwa kwa siku tatu mfululizo kwa simu akiwa Tabora, alisema yuko kwenye kikao apigiwe baadaye lakini alipopigiwa simu yake ilikuwa ikiita bila majibu.

Unajua huyu mwanamke anakichaasubiri niwasiliane na mwanasheria wangu nipigie baadaye, alisema.

Hata hivyo, mwandishi wa habari hizi alipoendelea kumpigia simu yake ya mkononi, iliita bila majibu.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI :sad:
Wabunge wote wa CCM matepeli tu; hakuna mwenye unafuu
 
Back
Top Bottom