DC wa CCM amtapeli kimada wake mamilioni ya fedha

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,775
18,189
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini , Suleiman Kumchaya, ameingia kwenye kashifa nzito ya kumtapeli mama mmoja fedha taslimu kiasi cha Sh. milioni 50.

Kumchaya ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Betty Matemba, anadaiwa kufanya utapeli huo katika vipindi tofauti mara baada ya kushindwa ubunge 2010.

Akizungumza na gazeti hili, Betty alisema Kumchaya wakati akiwa mbunge walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na walikuwa wakiishi kama mtu na mumewe.

“Unajua huyu bwana alikuwa mshauri wa Rais Mkapa, baadaye aligombea ubunge katika kipindi cha awamu ya kwanza ya serikali ya Rais Kikwete na alishinda lakini awamu ya pili hakuweza kupata.

“Wakati akiwa ni mbunge, bado alikuwa na uwezo mdogo sana kifedha, alinishawishi kumkopea fedha benki lakini siku zinavyokwenda mwenzangu hata halipi deni ndiyo nikachukua uamuzi wa kwenda bungeni ili akatwe marupurupu yake ya ubunge lakini ikaonekana hakuwa na hata senti mmoja,” alisema Betty.

Kwa mujibu wa Betty, mkuu huyo wa wilaya alipomaliza kipindi chake cha ubunge, maisha yake yakawa magumu kwani hakuwa na fedha wala mradi ingawa alikuwa akimiliki mamia ya ekari.

“Anao uwezo wa kunilipa, anazo ekari 60 za mikorosho Mtwara Vijijini, ekari 500 za ardhi huko Nachingwea akiziuza ni rahisi yeye kunilipa lakini anachonifanyia ni uhuni.

Awali tulikubaliana anilipe fedha hizo ili nilipe madeni yote ninayodaiwa,” alisema. Akiwa na makabrasha yanayoonyesha michanganuo ya fedha alizomtapeli, Betty anasema baada ya kupata ukuu wa wilaya alianza kumlipa kidogo kidogo ambapo Juni 28 mwaka jana alilipa Shilingi milioni moja na Julai 31 mwaka jana, alilipa Shilingi milioni moja na baada ya hapo hakuendelea tena.

Alisema wakati fulani walishauriana yeye (Betty) na Kumchaya wanunue vigari vidogo vya mizigo ili vimsaidie kusogeza maisha yake.

“Ilishindikana kununua hiyo gari kwani fedha ninayoitegemea ndiyo hiyo… Jumamosi (jana) kuna uwezekano wa kuondolewa kwenye nyumba niliyopanga Sinza kwani nimepandishiwa kodi na sina uwezo,” alisema na kuongeza kuwa kodi ya mwaka anatakiwa kulipia Sh. milioni 3.6 na kwamba mwenye nyumba tayari ameshamkabidhi barua ya kuondoka.

Betty alisema fedha hizo alitarajia kununua nyumba ambayo wakati huo ilikuwa ikiuzwa Sh. milioni 70 lakini kutokana na ‘mheshimiwa’ huyo kumrubuni, ilishindikana.

Alisema kutokana na jinsi alivyokuwa akimsumbua (Kumchaya) kulipa deni hilo, mkuu huyo wa wilaya alianza kutumia nguvu za giza.

“Kumchaya akiwa na mkewe mwingine Mpemba na rafiki yangu mmoja na mumewe, walikwenda Mbagala kwa mganga wa kienyeji wakitaka kuniua au kunifanya kichaa.

“Huyu mganga nilikuwa si mfahamu, lakini alipata namba yangu akanipigia akitaka nimuone…nilikwenda na wifi yangu (dada yake Kumchaya), tulipofika alinieleza yote pamoja na fedha aliyolipwa...," alisema.

Dada yake Kumchaya , alilipopigiwa simu kutoka Masasi, alikiri kutambua uhusiano uliopo wa Betty na Kumchaya.
“…huyu Betty ni wifi yangu kabisa, mkewe Selemani, ni wifi yangu ninayempenda sana.

Ni kweli Kumchaya na mkewe Fatma walikwenda kwa huyo mganga huko Dar es Salaam wakitaka kumroga Betty. Huyu mganga alimvuta Betty kimadawa hadi alipompata na siku hiyo tulikwenda wote kwa huyo mganga. Betty Mungu anampenda sana...," alisema Mwajuma kwa lafudhi ya Kimakonde.

Miongoni mwa fedha ambazo Betty anadai kuzikopa kwenye taasisi za fedha kwa ajili ya kumridhisha Kumchaya ni pamoja na Shilingi milioni saba (NMB), Shilingi milioni tisa (International Bank), Shilingi milioni 10 (Akiba Commercial) na Shilingi milioni 4.2 (Vission Saccos), hizo ni mbali na zile alizokopa kutoka kwa watu binafsi.

“Ilifikia kipindi aliniomba nikope Sh. milioni tisa kwa ajili ya kufanyia harusi ya mtoto wake, nilifanya hivyo na harusi ilikuwa nzuri sana.

Nilipoona hana muelekeo wa kulipa madeni hayo ilibidi tuandikishiane,” alisema huku akionyesha nyaraka hizo.

Betty anasema pamoja na kumuitia wazee wa heshima na viongozi wa dini ya Kiislamu ili wazungumze na Kumchaya alipwe deni lake, ilishindikana kabisa.

“Mimi sina ugomvi na huyu bwana, ninachotaka anilipe deni langu tu ili tuishi kwa amani,” alisema.

Mkuu wa Wilaya, Kumchaya alipotafutwa kwa siku tatu mfululizo kwa simu akiwa Tabora, alisema yuko kwenye kikao apigiwe baadaye lakini alipopigiwa simu yake ilikuwa ikiita bila majibu.

“Unajua huyu mwanamke anakichaa…subiri niwasiliane na mwanasheria wangu nipigie baadaye,” alisema.

Hata hivyo, mwandishi wa habari hizi alipoendelea kumpigia simu yake ya mkononi, iliita bila majibu.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI :sad:
 
Kumbe kina Kapuya wapo wengi sana ndani ya CCM. Nawashangaa sana jinsi wanavyopenda ngono na kibaya zaidi ni kwamba wameamua kuwekeza fedha za umma kwenye ngono binafsi. Hili suala lazima litazamwe kwa jicho la tatu, hasa na wananchi ambao ndio waathirika wakubwa wa ufisadi huu wa kimapenzi. Kama ikibidi, kuna haja ya kuchukua uamuzi mgumu kama ule waliouchukua wananchi wa Mwanza leo mchana.
 
Huyu mwanamke hazimtoshi unakopaje hela hili umfurahishe bwana.
Huko kwenye taasisi zinazokopesha hawaelezwi madhumuni ya mikopo.
Ina maana wakati anaenda kukopa kwa niaba ya huyo bwana, Kumchaya alikuwa hakopesheki?.
Atuache tuendelee kuombeleza kifo cha Madiba wetu,yeye aendeleze pillow talk na Kumchaya.
 
Do pole sana mama sijui kama utapata hakiyako maana kama ni Mkuu wa wilaya yana Mwana CCM Sali sana.
 
Kumchaya kamroga huyu betty mpaka akawa anatoa mamilion,dawa imeisha ndio betty kastuka,hivi sinza kupanga nyumba nzima kodi kwa mwaka sh. 3.6m? Au ni sinza ile ya Tandale/Manzese?
 
Yaani hawa MADC wa CCM ni tatizo, kuna mwingine aliyewahi kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Masasi na sasa DC kama sikosei yupo wilaya ya Mwanga anaitwa Ndemanga amemtapeli Mwl mmoja hapa Masasi sh 300,000/= kwa ajili ya pango la nyumba yake lakini baadae nyumba hiyo alimpangisha mwingine bila kurudisha fedha ya mwl aliyeichukua mwanzo na kila akipigiwa simu kwa sasa anakata na hapokei ila akibadiishiwa namba anapokea na akigunduwa ni mdaiwa wake anakata simu.
 
Mleta mada amevurugwa kweli kweli. Naamini amekunywa gongo asbh ndio imemfikisha hapo.

ccm haina mkuu wa wilaya.
 
Yaani hawa MADC wa CCM ni tatizo, kuna mwingine aliyewahi kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Masasi na sasa DC kama sikosei yupo wilaya ya Mwanga anaitwa Ndemanga amemtapeli Mwl mmoja hapa Masasi sh 300,000/= kwa ajili ya pango la nyumba yake lakini baadae nyumba hiyo alimpangisha mwingine bila kurudisha fedha ya mwl aliyeichukua mwanzo na kila akipigiwa simu kwa sasa anakata na hapokei ila akibadiishiwa namba anapokea na akigunduwa ni mdaiwa wake anakata simu.
Wanywa gongo wenzako ndio wataamini huu uzushi
 
It seems like wizi ni sifa ya viongozi wengi ndani ya CCM?
Akili yako ina matege.. Wezi wapo chadema na hawataki kuhojiwa. Mbowe anachota mamilioni ya ruzuku anaenda kununua majumba dubai, slaa anajichotea ruzuku ya chama anaenda kuvinjari na hawara ulaya. Jiulize kwanini hawataki kujibu hoja za mwigamba na zile za mkakati wa mabadiliko 2013
 
Back
Top Bottom