figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,717
- 55,819
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela alishiriki katika kuzima moto uliounguza bweni wanalo kaa watoto yatima katika kituo cha Mgongo. Moto huo ilioanza kwa hitalafu ya umeme umeteketeza bweni 3 na kuunguza mali za watoto hao ikiwemo nguo, madaftari magodoro. Kikosi cha zimamoto chini ya Mrakibu Komba kilifanya kazi ya ziada kuzuia moto huo usieneee majengo mengine. Wananchi wa eneo la Mgongo wamefanya kazi kubwa wakisaidiana na jeshi la zima moto.
Akizungumza na wananchi Mh Kasesela ameahidi kuomba wahisani pia kuangalia uwezekano wa kuwasaidia waathirika wa janga hili la moto. Inakadiriwa watoto zaidi ya 45 wameathirika na moto huu ingawaje hamna majeruhi hata mmoja. " Pongezi ziwandee jeshi la Zimamoto pamoja na changamoto walifanikiwa kuzima moto huo" aliesema Mkuu wa Wilaya. Mkuu wawilaya alikutana na watoto na kuwapa matumaini serikali ipo pamoja nao.