DC Mbarali apigwa mawe, anusurika kifo!

Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,700
1,086
Mkuu wa wilaya ya mbarali mkoani mbeya amenusurika kifo baada ya gari lake kupigwa mawe na kuchomwa matairi kwa kutumia misumari.
Balaa hilo limemkuta baada ya kutoa amri ya kufungwa kwa chuo cha uuguzi cha red cros kilichopo wilayani hapo kwa madai kwamba hakina usajili.
Baada ya kutoa amri hiyo na kuondoka wanafunzi walisimamisha gari na kuanza kumshambulia kwa mawe.
Mpaka sasa polisi inashikilia wanafunzi 32.

Source 1:E.born fm
2.niko mbeya
 
Hawa watawala inabidi waangalie namna ya kufanya kazi na wananchi, wasichukulie kuwa nyakati zimeganda. Wakae wakijua raia wana hasira na wanatafuta sehemu ya kuzitolea. Mfano angeweza kabisa kusaidia chuo kisajiliwe ili kitoe huduma kihalali badala ya kukifunga.
 
Kajitakia kwanini asifuate taratibu za ukaguzi na kama kunamapungufu angeupa uongozi muda wa kukamilisha usajiri, kwani mgeni na mbeya? Hasomi historia, amuulize kandoro yaliomkuta.
 
Wacha apigwe maana anaingilia kazi zisizo zake! Dc amepata mamlaka wapi ya kufunga chuo?
 
Hao MaDC wengi wao ni vihiyo kupindukia. Kazi yao kuvaa suti zilizoshonwa chini ya miembe. Na watachezea vichapo ile mbaya
 
bora wangemmalizia kabisa ,huwezi kufunga chuo ghafla wakati wazazi tumelipa ada tayari na wanafunzi hawana pa kwenda.
 
Kwanini amekwenda chuoni na kutoa mari ya kufunga chuo bila kuzingatia maslahi ya wanafunzi ambao tayari wamelipa pesa zao na kama ni uzembe ni wa serikali kwa kutofuatilia mapema kuhakikisha kwamba chuo kinakamilisha taratibu za usajili kabla hakijaanza kudahili wanafunzi.

Ama ni kwanini hakuona umuhimu wa kuupa uongozi/mmiliki wa chuo muda wa kukamilisha usajili kabla hajafikia uamuzi wa kufunga chuo?
 
Mkuu wa wilaya ya mbarali mkoani mbeya amenusurika kifo baada ya gari lake kupigwa mawe na kuchomwa matairi kwa kutumia misumari.
Balaa hilo limemkuta baada ya kutoa amri ya kufungwa kwa chuo cha uuguzi cha red cros kilichopo wilayani hapo kwa madai kwamba hakina usajili.
Baada ya kutoa amri hiyo na kuondoka wanafunzi walisimamisha gari na kuanza kumshambulia kwa mawe.
Mpaka sasa polisi inashikilia wanafunzi 32.

Source 1:E.born fm
2.niko mbeya

Mkuu, jana jioni defender mbili za FFU zilipita wangu wangu na siraha/ mabomu ya machozi hapa eneo la ccm (Mbeya) kwenda Kumuokoa huyo magamba. Leo hii muda huu ndo tena wanapita hapa askali woote wamepauka usoni kwa sababu ya kupambana wapigania haki wa elimu katika bonde la Usangu. Mwaka huu ni mbaya kwa magamba katika mkoa wa Mbeya.
 
Hao wanafunzi watakuwa wanavuta bangi tu. Haiwezekani umpige mawe mtu ambaye ana umri sawa na wazazi wako. Mitoto ya siku hizi haina adabu kabisa kwasababu ya mindumu.
 
Kwanini amekwenda chuoni na kutoa mari ya kufunga chuo bila kuzingatia maslahi ya wanafunzi ambao tayari wamelipa pesa zao na kama ni uzembe ni wa serikali kwa kutofuatilia mapema kuhakikisha kwamba chuo kinakamilisha taratibu za usajili kabla hakijaanza kudahili wanafunzi.

Ama ni kwanini hakuona umuhimu wa kuupa uongozi/mmiliki wa chuo muda wa kukamilisha usajili kabla hajafikia uamuzi wa kufunga chuo?

Mkuu Malanya, siri-kali yenyewe ya ccm!! Inategemea zaidi amri badala ya kuongoza.
 
Mwanzo mzuri, tukiendelea na mwendo huu watatuheshimu na kuacha kunyanyasa na kuibia raia.
 
Back
Top Bottom