DC Mbarali apigwa mawe, anusurika kifo!

DC Mbarali apigwa mawe, anusurika kifo!

Kupigana sio njia stahili ya kutafuta suluhisho la mambo. Ila arrogance ya watawala na wanaotawaliwa ndio chanzo cha haya tunayoyaona sasa hivi. Tubadilike tutaiharibu nchi yetu.
 
Mkuu Domy hawa watu walikuwa wanatumika sana enzi za ukoloni mwalimu alikopy na kupeste kwenye serikali yake sasahivi nimzigo tu kwa walipa kodi vyeo hivi tupigane kwenye katiba vifutwe tubaki tu na wakurugenzi na tuanzishe majimbo yatawaliwe na magavana tena wachaguliwe na wananchi mkuu.

Pamoja na ku-C&P, Mwalimu alijaribu kubadilisha jina na kuwapachika ma Area Commissioners (AC) na wakati wa ujamaa walijulikana zaidi kwa title ya Kiswahili 'wakuu wa wilaya'. Lakini tuliporejea katika kukumbatia 'soko-huria' uchwara, basi lile jina la kikoloni la u-DC nalo likarejeshwa ili kusisitiza thamani inayofikiriwa kuwemo katika cheo hicho - na hilo limewaongezea kiburi kweli kweli. Hawataki kusikia wanaitwa wakuu wa wilaya, wanata kuitwa ma-DC. Ninasikia wengine wanapekuapekua makabrasha ya enzi za mkoloni ili kujielimisha jinsi ma-DC wa mama Queen walivyokuwa wakiendesha maeneo yao!!! Bongo haitaacha kuwa jumba la sinema.
 
MATUKIO MBEYA
1.JK alipigwa mawe
2.mama Salma kurushiwa makopo ya maji mwanjelwa
3.waziri Shamsi V.Nahodha alipigwa mawe tunduma.
4.Mbunge viti maalum CCM aliokolewa na polisi mwanjelwa.
5.Kandoro aliambiwa aondoke
6.Dc mbarali kupompolewa mawe.
Hayo ndio matukio makubwa ninayokumbuka watu hawajifunzi tu.kweli wamechoka
 
Hawa wakuu wa Wilaya wanakazi na elimu itolewayo na Chadema.
 
Aaaah Radhia, kwa cheo, uwezo na Elimu ya huyo DC alipashwa tambua kua yeye ni sehemu ya suluhisho na c tatizo. Kufunga chuo ni janga, wanafunzi waende wapi? Hao anawafungia shule ndo mabos zake. Au kwakua yeye analipwa hela asizo zitolea jasho???!
 
Nimeangalia kwenye habari I.T.V nimeona mkuu wa wilya anavyokifunga chuo kwa jeuri! Eti kuanzia sasa nimekifunga hiki chuo na kila mtu atawanyike arudi kwao na sitaki Maswali yeyote du jamaa anatumia ubabe kweli!
 
Ma DC wa Dhaifu hawa, wengine hata kuandika majina yao shida wameukwaa basi tu kwa sababu ni washkaj wa lile jambazi Rz1 au lile teja ! Soon utasikia hata Wema, Diamond, pinto, kisaka na Ruge nao ni washauri ktk ofisi ya rais !!

Kuna DC mmoja alinipiga mzinga na nimempa deadline, akichelewa tu nimemwambia ntamshukia kwa kosovo la nguvu tena siku anaongoza kikao cha kamati ya ulinzi, uzinzi, fitna na usalama !!
 
DC ana mamlaka ya kufunga chuo cha uuguzi?
Ndio.


Kajitakia kwanini asifuate taratibu za ukaguzi na kama kunamapungufu angeupa uongozi muda wa kukamilisha usajiri,
Unajuaje hakufuata uratatibu na hakuupa uongozi muda?

Hebu nambie: Utaratibu ukoje?

kwani mgeni na mbeya?
Mgeni na Mbeya? Kwani Mbeya ina sheria zake?

All are equal before the law, people, regions and jurisdictions alike. Serikali haina utaratibu maalum au sheria za kipekee za kubembeleza raia na taasisi zilizo maeneo ya watu wakali. Serikali imefunga taasisi isiyotambulika, wanafunzi wameshindwa kuona kwamba Serikali inawalinda wao, wakaamua kutenda jinai ya hali ya juu. Sheria ichukue mkondo.


kama ni uzembe ni wa serikali kwa kutofuatilia mapema kuhakikisha kwamba chuo kinakamilisha taratibu za usajili kabla hakijaanza kudahili wanafunzi.
You got it backwards!

Ni jukumu la chuo, sio la serikali, kuhakikisha kinakamilisha usajili kabla ya kudahili wanafunzi. Wewe ukiamka kesho asubuhi ukaanza kufundisha kozi za uuguzi sebuleni kwako hatuwezi kuilaumu serikali kwamba haijakuwahi wakati unakusanya wanafunzi. Sisi tungejuaje wewe unadahili watu kwa ajili ya kuanzisha shule wakati hatujawaona wanahudhuria masomo?

Ama ni kwanini hakuona umuhimu wa kuupa uongozi/mmiliki wa chuo muda wa kukamilisha usajili kabla hajafikia uamuzi wa kufunga chuo?
Unajuaje hakuupa uongozi wa chuo muda wa kukamilisha usajili?
 
Ipo siku tutasikia DC amefunga ofisi ya mkurugenzi au ataamuru shule ifungwe ili uwe ukumbi wa CCM hii ndio bongo ya rahisi JK
 
Hao wanafunzi watakuwa wanavuta bangi tu. Haiwezekani umpige mawe mtu ambaye ana umri sawa na wazazi wako. Mitoto ya siku hizi haina adabu kabisa kwasababu ya mindumu.

mwenye umri sawa na baba yako ni vizuri pia akawa na akili na busara inayofanana na baba yako aliyejihimu mpaka akakulipia hiyo karo ili usome. Ni upuuzi kumlinganisha DC ZUZU na baba yako, alitakiwa afikirie maslahi ya wengi waliokuwepo hapo, iweje afunge chuo kibabe, halafu vijana waende wapi na ilihali wamelipa karo angalau wapate elimu wajikwamue kimaisha?? kwa nini basi angalau asiache watu wakamalizia japo semester hii, halafu ndo wakarudi home wakiwa prepared?? TAFADHALI USIMLINGANISHE HUYU DC ZUZU NA BABA YAKO MZAZI MWENYE BUSARA, UNAMVUNJIA HESHIMA BABA YAKO.



Tuendeleeni kuwaelimisha wananchi, waelimike ili waling'oe madarakani hili li-serikali la ccm MAONGO/MAFISADI/MAJAMBAZI/WAUAJI
 
Na bado ! Anae fuata sasa atakua ni wasira. Huu ni ujumbe mzuri kwa magamba.
 
VIDEO

Mkuu wa wilaya ya mbarali mkoani Mbeya bwana Gulamu Husein Sekifu amenusulika kupigwa mawe na gari yake kuharibiwa vibaya na wanafunzi wa chuo cha mafunzo ya huduma ya kwanza kilichopo Chimala wilayani Mbarali baada ya mkuu wa wilaya kukifunga rasmi chuo hicho ambacho kilianza kufunza wanafunzi toka mwaka 2008.


source ITV TANZANIA youtube
 
Last edited by a moderator:
Na bado ! Anae fuata sasa atakua ni wasira. Huu ni ujumbe mzuri kwa magamba.

Mkuu Mbozib, Huyu DC alikutana na nguvu ya umma kutoka kwa mabinti wenye kiu ya elimu ambaya Magamba na serikali ya wilaya ya Mbarili wamewanyima lakini masamaria mwema kaanzisha chuo kwa kujinyima ili kuwasaidia wazarendo wenzake. Kama ingekuwa rahisi kwa wao serikali kujenga vyuo vilivyo bora kwanini wameshindwa kuwajenga nga kimoja hao mabinti wasome katika chuo kilicho bora?
 
Na bado ! Anae fuata sasa atakua ni wasira. Huu ni ujumbe mzuri kwa magamba.

Mkuu Mbozib, Kichapo alichopokea kwa mabindi hao kilikuwa cha uhakika ilibidi kucholipoka kutoka kwenye shangingi lake na kutokomea vichakani ndo ponapona yake, la sivyo wangemtoboa macho "Liwalo na Liwe." Hawa walikuwa wakitetea haki yao ya kupata elimu.
 
kweli ndo faida ya kuwa kada wa chama.

Ndugu yangu weee!! wakati wa kutoa amri alijifanya shujaa kweli kweli lakini mabinti walipofanikiwa kutoboa matairi ya shangigngi lake alichanganyikiwa na kukimbilia vichakani, kama kungekuwa na karavati jirani yangemkuta ya Gadafi. Hili ni fundisho kwa ubabe wa ccm.
 
Kwa taarifa nilizopata mabinti wanasema walikosa petroli jirani walitaka kufuta kabisa kizazi,yaan polisi wangekuta jivu.
 
Alichotakiwa kufanya DC (kama ni kazi yake) ni kuagiza mwenye chuo afunguliwe mashtaka ya kuendesha chuo bila usajili. Kesi ingeendelea huku wanafunzi wakisoma.

Ni kukosa busara kwa hali ya juu, na kulewa madaraka, kwa DC kuagiza chuo kifungwe. Au ana shida nyingine?
 
Back
Top Bottom