Sandinistas
JF-Expert Member
- Jul 5, 2013
- 2,616
- 1,778
Mkwaruu umenena; mfano hai ni Kibiti. Miaka michache iliyopita, kabla ya hizi siasa za kugawa watu, haya kibiti yasingepata nafasi.
Not every human being fits the real definition of huma being-Siasa zimetufanya tu-behave kama wanyama.Wapumbavu sana hawa, kazi yao kubwa imebaki kutesa watu wasio na hatia huku majitu yenye hatia tukiambia tuyaache kama yalivyo, inauma sana kuona ukweli unageuzwa uchochezi kwa maslahi tu ya kichama
Hata Halima pia ni binadamu naye pia ana ndugu zake waoumia kwa haya yanayotendeka juu yake!!Wewe nadhani unaweza isaidia polisi kwa matamshi haya. Msifanye utani na maisha ya watu. Angekuwa mwanao ndio anakumbwa na mkasa ule kule kibiti sijui ungesemaje. Sasa kwa sababu ni watu hawakuhusu, unadharau wacha wauwawe tuu au siyo. Dawa yako ipo jikoni
Usicheze na Rais hata simu moja. Yule ni kiongozi wa watu zaidi ya million 45. Ni MTU muhimu sana kuliko unavyofikiria. Ni amiri jeshi mkuu na wanaomshikilia kwa sasa ni jeshi. Hao wote uliowataja hawana cha kufanya.Huyu DC aburuzwe mahakamani haraka sana!! Tundu Lissu, Kibatala, Professor Safari unganeni katika hili! hawa wakutumwa wasiotumia ubongo watatumaliza! Ona sasa polisi wanatupiana mpira ovyo
Akitwaliwa naomba unitagi mkuuPamoja
kweli wewe ni mkwepa kodi duhdah sio fresh lakini,kumfanyia hivyo dada yetu.
nimecheka hapo taarifa iliposema kua ameanza kula,....chadema kwa maigizo; mi nilifikiri yuko 'serious' na suala la kutokula!
Huyu jamaa si alikuwa anapita analia makanisani? Yaani ameshika nguvu mbili kwa Mara moja?Mshauri mkuu wa baba Jesca ni Daud Albert Bashite mshirika wa GSM wafadhili wa miladi binafsi ya kwao ikiwemo kuzilea na kuzitunza nyumba ndogo zao, Wapinzani wakiamua kujihami kwa bidii wakaweza kumdhibiti Bashite wanaweza kumaliza kero nyingi ingawa Bashite anamiliki waganga wa kienyeji zaidi ya 200 lakini hawawezi kuzuia nguvu ya umma pindi ikiamua kuwaandama bila kuchoka.
Hakuna haja ya kwenda mahakamani ya kibiti yawakuteHuyu DC aburuzwe mahakamani haraka sana!! Tundu Lissu, Kibatala, Professor Safari unganeni katika hili! hawa wakutumwa wasiotumia ubongo watatumaliza! Ona sasa polisi wanatupiana mpira ovyo
Halima ni kiongozi jasiri na mwenye uthubutu wa kufanya jambo na kusimamia msimamo wake.BAADA ya Jeshi la Polisi kumshikilia kwa zaidi ya saa 48 Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, ambaye ndiye chanzo cha kukamatwa kwa mwanasiasa huyo, amejivua kwenye sakata hilo.
Jana jeshi hilo lilimuhamisha Mdee kutoka katika mahabusu za Kituo cha Oysterbay alikokaa kwa siku nne na kumpeleka Kituo Kikuu cha Polisi (Central), ambako anaendelea kushikiliwa kwa kosa la uchochezi.
MTANZANIA Jumapili lilipomtafuta Hapi ili kufahamu kama amri ya saa 48 alizozitoa kwa polisi kumshikilia Mdee ina mabadiliko yoyote, alisema kwa sasa suala hilo asiulizwe yeye bali Jeshi la Polisi.
“Muulizeni Kaimu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,” alisema Hapi bila kufafanua.
MTANZANIA Jumapili lilipomtafuta Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya na kumuuliza kuhusu hilo, alijibu kuwa yuko likizo.
“Niko likizo, sijui kama (Mdee) yupo hapo, mtafute Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala,” alisema Mkondya.
Alipotafutwa kwa simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni, alikiri kuwa ni kweli mbunge huyo alipelekwa hapo kwa mahojiano.
“Aliletwa hapa kwa mahojiano, lakini ni suala la Kanda Maalumu,” alisema Kamanda Hamduni.
Alipoulizwa msingi wa mahojiano hayo, Kamanda Hamduni alisema kuwa hilo ni suala la kipelelezi kupitia Kanda Maalumu.
“Mimi si mpelelezi, anayepeleleza ni Kanda Maalumu,” alisema.
Mdee ambaye alihojiwa kwa saa kadhaa jana mara tu baada ya kuhamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi, hakupatiwa dhamana kwa kile kilichoelezwa askari waliopewa jukumu la kumuhoji hawakuwa na maelekezo mengine.
Awali, MTANZANIA Jumapili lilimtafuta Wakili wa Mdee, Hekima Mwasipu ambaye alifafanua kuwa mteja wake alihojiwa kwa kosa la uchochezi.
“Ni kweli alihamishiwa Kanda Maalumu leo (jana),” alisema Mwasipu.
MTANZANIA Jumapili lilitaka kufahamu sababu za Mdee kuhamishwa kutoka Kituo cha Oysterbay na kupelekwa Kanda Maalumu ambako ameendelea kushikiliwa licha ya saa 48 kupita, Mwasipu alisema hata yeye alihoji na kujibiwa kuwa ni suala la polisi kanda hiyo.
“Sababu za kumtoa kule na kumleta Kanda Maalumu sielewi ni nini, lakini ninachoweza kusema ni kwamba Jeshi la Polisi linafanya kazi kwa kushirikiana.
“Ila kwa maelezo yao hata mimi nilipowahoji walijibu kwamba makosa hayo yako chini ya Kanda Maalumu, ni ‘special’ (maalumu), kesi ziko chini ya kanda hiyo,” alisema Mwasipu.
Alipoulizwa kuhusu hali ya mbunge huyo ambaye awali aligoma kula na suala la dhamana, Mwasipu alisema hivi sasa anakula na alihojiwa kwa takribani saa moja, lakini dhamana yake ilishindikana.
“Suala la kufikiswa mahakamani ama kutofikishwa mahakamani hilo ni suala lao polisi, lakini maelezo kaandika na tulifuatilia suala zima la dhamana ikawa ngumu.
“Walisema wao hawana maelekezo yoyote kuhusu dhamana, ni wale ambao walikuwa wanamsimamia Halima kuandika maelezo, hadi jioni hii walinipigia simu, kimsingi leo hatapata dhamana, labda kesho,” alisema Mwasipu.
Awali, waandishi wa MTANZANIA Jumapili walifika kituoni hapo, lakini walizuiwa getini baada ya kujitambulisha kwa madai kuwa Kaimu Kamanda wa Kanda Maalumu hakuwapo ofisini na wala hakukuwa na mtu mwingine aliyekuwapo ili kutoa taarifa kwa waaandishi wa habari na kutakiwa kusubiri nje ya eneo la kituo.
Wakiwa nje ya kituo hicho ambako walikaa kwa saa kadhaa, walishuhudia hali ya utulivu huku ukaguzi ukiendelea, huku baadhi ya watu waliosadikika kuwa wafuasi wa Chadema walizuiwa kuingia na kukaa kando kwa muda kabla ya kuondoka.
Mdee, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), alikamatwa Julai 4, mwaka huu, baada ya Hapi kutoa amri ya kushikiliwa kwa saa 48 kutokana na matamshi aliyodai kuwa ni ya kumkashifu Rais Dk. John Magufuli.
Matamshi hayo anadaiwa kuyatoa katika mkutano aliofanya na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni, Dar es Salaam.
Mdee alidaiwa kumkashifu Rais Magufuli kutokana na kuhoji baadhi ya kauli zake zikiwamo zile alizotumia wakati akitangaza kupiga marufuku wanafunzi wa kike wanaopata mimba kurejea shuleni.
Si hilo tu, Mdee pia alihoji kauli nyingine zinazotolewa na Rais Magufuli ambazo alidai kuwa zinakiuka misingi ya sheria.
Kweli aiseeMungu hawezi chukua watu waonevu hao ni rafiki wa shetani..
Kwani polisi yenyewe haiwezi? Basi waache kupokea mshahara.Wewe nadhani unaweza isaidia polisi kwa matamshi haya. Msifanye utani na maisha ya watu. Angekuwa mwanao ndio anakumbwa na mkasa ule kule kibiti sijui ungesemaje. Sasa kwa sababu ni watu hawakuhusu, unadharau wacha wauwawe tuu au siyo. Dawa yako ipo jikoni
Hata Bokassa Idd Amin Saddam Hussein nao walikuwa watu muhimu katika utesaji na uuaji ndiko anakoelekea huyu wa kwetu. Anacho fanya sasa ni robo tu mpaka 2018 chini ya utawala huu nchi itakuwa Uganda ya Idd AminUsicheze na Rais hata simu moja. Yule ni kiongozi wa watu zaidi ya million 45. Ni MTU muhimu sana kuliko unavyofikiria. Ni amiri jeshi mkuu na wanaomshikilia kwa sasa ni jeshi. Hao wote uliowataja hawana cha kufanya.
Halima Mdee kututukana wote, mwache ashikishwe adabu.
Ila mimi hajanitukanaUsicheze na Rais hata simu moja. Yule ni kiongozi wa watu zaidi ya million 45. Ni MTU muhimu sana kuliko unavyofikiria. Ni amiri jeshi mkuu na wanaomshikilia kwa sasa ni jeshi. Hao wote uliowataja hawana cha kufanya.
Halima Mdee kututukana wote, mwache ashikishwe adabu.