DC Jokate, ametangaza rasmi kuja na kampeni ya TEMEKE GULIO

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,895
940
TEMEKE GULIO KUTOA FURSA ADHIMU KWA WAFANYA BIASHARA WADOGO (WAMACHINGA) WILAYA YA TEMEKE - MHE.JOKATE MWEGELO


Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe.Jokate Mwegelo ,Leo Oktoba 13 ametangaza rasmi kuja na kampeni ya TEMEKE GULIO itakayotoa fursa adhimu kwa wafanyabiashara wadogo maarufu wamachinga kuweza kutangaza biashara zao na kuweka mfumo mzuri wa mahali pa kufanyia biashara zao kwa utaratibu,kampeni ambayo inatarajiwa kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.Amos Makala katika Wilaya ya Temeke.

Katika Kampeni hii ya TEMEKE GULIO Mhe.Jokate amesema kuwa kwa kushirikiana na Viongozi wenzake ngazi ya Wilaya wameweza kuongea na wadau na katika hili watashirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Benki ya NMB,Kampuni ya Vinywaji ya COCACOLA pamoja na Kampuni ya KORIE ya Mafuta na yenye bidhaa za Tambi na Mchele.

Mhe.Jokate ameeleza kuwa Kampeni hiyo ya TEMEKE GULIO imelenga kuwabeba wamachinga kuweza kuzitangaza zaidi biashara zao,kujikwamua zaidi kiuchumi kwa kuwezeshwa kupata mikopo kwa masharti nafuu inayoanzia Tsh laki 5 hadi kufikia Milioni 5,Mikopo ya Bodaboda na Bajaji kutoka Benki ya NMB na kupata Elimu zaidi inayohusiana na Ujasiriamali kutoka pia kwa Kampuni ya Cocacola.

Pia kupitia Kampuni ya KORIE Mhe.Jokate amesema kuwa wanawapatia zawadi akina mama wote waliowahi kuikimbilia fursa ya kufanyia shughuli zao katika maeneo yaliyoainishwa rasmi eneo la Mbagala wa Kilo 400 ambao umeandaliwa kwa pakiti za kilo moja moja ambapo watawapatia akina Mama hao wa Mama lishe wanaondelea kufanya shughuli zao maeneo hayo.

Mhe.Jokate amesema kuwa tayari wameshaainisha maeneo 20 ambayo yanajumuisha na masoko ya DMDP yaliyokuwa hayafanyi vizuri ambayo kwasasa umeshapangwa vema mpango mzuri ikiwa ni pamoja na kuandaa ruti za usafiri wa daladala zitakazoweza kuingia kwenye masoko ili wananchi kufuata bidhaa kwa wamachinga na sio wamachinga kuwafata wateja.

Aidha Mhe.Jokate ametoa Rai kwa wamachinga wafanyao biashara zao pembezoni mwa barabara ya kilwa road kujiandikisha na kuomba mapema maeneo sahihi yaliyoainishwa kufanya biashara zao kwani ifikapo tarehe 19 haitaruhusiwa tena kuendelea kufanya biashara maeneo hayo ya barabarani kwa usalama wao.

Mhe. Jokate Mwegelo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke

z9fIX2Hr_400x400.jpg


FBfPDDkXsAECZD-.jpg


FBfPDDkXEAAbZ3y.jpg
 
Back
Top Bottom