DC Jokate: Wananchi washirikishwe katika hatua zote katika miradi ya maendeleo ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa miradi hiyo

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
DC JOKATE: WANANCHI WASHIRIKISHWE KATIKA HATUA ZOTE KATIKA MIRADI YA MAENDELEO ILI KULETA UFANISI KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mhe Jokate Mwegelo amewataka wanaotekeleza miradi ya serikali na isiyo ya serikali kushirikisha wananchi kwakuwa miradi hiyo ni ya wananchi hivyo Wanayo Haki ya kuifahamu.

Mhe.Jokate ameyasema hayo katika Kijiji Cha Kwatonge kilichopo Kata ya Mashewa Wilayani Korogwe Mkoani Tanga,wakati wa kumkabidhi mradi wa Maji mkandarasi Ili aweze kuanza Ujenzi wa Miundombinu ya Maji katika Kijiji hicho.

Awali akitoa taarifa Kwa mkuu wa Wilaya hiyo meneja wa RUWASA Wilaya ya Korogwe Mhandisi William Tupa amesema mradi huo utagharimu zaidi ya shilingi milioni mia sita na ishirini.

"Mradi huu mheshimiwa mkuu wa Wilaya kwa upande wa mkandarasi utagharimu shilingi milioni mia sita na ishirini.Mradi huu umegawanyika kuna uoande wa mkandarasi na upande wa serikali utanunua Bomba Kutoka kiwandani na hivyo mkandarasi atakupwa zaidi ya shilingi milioni mia nne."alisema Mhandisi Tupa.

Baada ya kukabidhi mradi huo kwa mkandarasi mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe.Jokate amesema kwa kuwa miradi yote inayotekelezwa inawahusu wananchi,hivyo ni muhimu wananchi kushirikishwa kwenye Kila hatua ya utekelezaji wa miradi.

"Mradi huu unapoenda kutekelezwa wananchi washirikiahwe kikamilifu,na ninafurahi kwamba jambo limekuwa jambo,na sio mradi huu tu ni miradi yote uwe wa serikali au usiwe wa serikali Ili hali inawahusu wananchi basi washirikiahwe kikamilifu"

Katika hatua nyingine DC JOKATE Amesema atapenda miradi yote itemeleze kwa viwango vinavyotakiwa na kuongeza kuwa hatavumilia yeyote atakwenda kinyume na makubaliano.

"Ni lazima tutumie pesa inavyotakikana na ni lazima tuone thamani ya fedha kwenye mradi mbalimbali inayotekelezwa,kinyume na hapo utatafuta mgogoro na mkuu wa Wilaya kwa niaba ya wananchi."Alisema DC JOKATE.

IMG-20230326-WA1301(1).jpg
IMG-20230326-WA1299(1).jpg
 
Back
Top Bottom