DC Jerry Muro atishia kuumiza na kupoteza watu wanaodai katiba

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
IKUNGI-SINGIDA,

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida ndugu Jery Muro ametos kauli kali na vitisho kwa wananchi wa wilaya ya hiyo kua yeyote atakayefanya siasa au kudai katiba mpya katika eneo lake atakula kichwa chake na kumpoteza mchana kweupe, ameongeza kua tumezoea kazi hiyo inafanywa na wasiojulikana lakini yeye atafanya mchana kweupe watu wanaangalia. Pia DC Muro amekaririwa akisema kua 2025 hakuna mpinzani atakayetangazwa, ni ccm tu hakuna mwingine.

Kauli hizi amezitoa wakati alipofanya mkutano katika kijiji cha Kinyonga kata ya Mungaa ndani ya Wilaya hiyo baada ya kutembelea eneo ambalo limekua na mgogoro wa ardhi kwa wakulima.

Udhibitisho wa kauli hizi ni wananchi wa eneo husika ambao walikuwepo kwenye mkutano. Mpaka kufikia kuandika maneno hayo hapa jukwaani kuna uhakika wa maneno ya wananchi wa eneo hilo waliofika katika mkutano huo.

Kauli hizi zimezua minong'ono kila mahali na kuwafanya wananchi wa eneo husika kukosa amani kabisa kwa vyama vyote CCM pamoja na upinzani, wanahoji kua Rais Mama Samia aliahidi wakati anaapa kua Rais alisema atawafuta machozi lakini kwanini amewapelekea majonzi tena?

My take
Mimi kama MwanaCCM kindakindaki nimefedheheshwa sana na kauli za kipuuzi za DC Muro kwa kujawa kiburi kiasi hicho, RC wa Dodoma Comrade Athony Mtaka aliwaambia ma-DC wake wakati anawaapisha wasinyanyue mabega wala wasiwe na baleghe ya madaraka lakini DC Muro hii tabia ndio imekolea kwake.

Tumuombe Mhe Rais wetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan, huyu Jerry si mtu wa kuaminika ni mwendelezo wa viongozi wanaofanya kazi kwa kutaka sifa, siku likitokea la kutokea akapoteza mtu katika eneo husika mshukiwa wa kwanza ni Jery Muro. Wananchi wa eneo husika hatutakubali tena mtu mmoja atuchafulie hali ya hewa. Ni wakati mwafaka wa Mama kumuondoa katika eneo husika.

Tulikua na DC Edward Mpogoro ambaye alifanya kazi kwa uadilifu mkubwa lakini hakua na ujinga huu, mbona yeye alipambana na nguvu ya Tundu Lissu na CCM tukashinda majimbo yote? Jery Muro ana kipi cha ziada mpaka kutoa vitisho kiasi hicho?

Yeye anajivunia kutembea na vyombo vya dola lakini akumbuke kua hatototembea navyo maisha yake yote, hii dunia ni eneo la mapito tu. Asijigambe wananchi wakiamua asikae Ikungi hawezi kukaa.

Pia soma: Jerry Muro tulikuambia ubadhirifu wa miradi ya umma Ikungi utakuondoa, pole sana
 
Tupia sauti,maandiko hayo ni mazito sana.Mkuu wa wilaya yupo kwa mikakati ya uchaguzi badala ya maendeleo.Sasa anapingana na nani wakati nchi inaingozwa na ccm
 
Ila anaweza pia kufutika, kabla ya kula kichwa Cha wanadai katiba, mungu Sio wa mchezo, alafu viongozi wa tz mbona wanawazoea Sana wananchi, katiba ya ni wananchi Sio ya familia yake.

Mungu wangu Alie hai naomba ashughulike na viongozi Kama awa kwanza
 
Lakini mkuu au mjomba kwanini hao walio kuambia hayo maneno usingewaaambia wakutumie ka clip au kasauti cha kurekodi ili tuamini maana Serikali hii sio ya majungu kama ile ya mwendazake
 
Ila anaweza pia kufutika, kabla ya kula kichwa Cha wanadai katiba, mungu Sio wa mchezo, alafu viongozi wa tz mbona wanawazoea Sana wananchi, katiba ya ni wananchi Sio ya familia yake ,

Mungu wangu Alie hai naomba ashughulike na viongozi Kama awa kwanza
Eeh Mungu wa Daudi, Mungu wa Isaka na Yakobo Tenda miujiza Bwana
 
Masalia ya Mwendazake ,asidhani huruma na fadhila za Mama kuwapoza wafuasi zitadumu!
 
Back
Top Bottom