DC Igunga amefichua udhaifu wa CHADEMA?

Kwani Raia Mwema nalo pia mwana harakati Generali Ulimwengu kaliuza kama Rai na mengine?????????????

Si unajua njaa ndugu yangu wanaharakati siyo hisia it is a innate trait bwana.Pesa kama hauko makini na hizi njaa unaweza acha ata dini na imani yako.RAI.-YA MWEMA ni ukiwa CCM na siyo vingine bwana.
 
Godfrey Dilunga ni mwandishi anayeandika makala zake kwa mrengo wake anaoufahamu. Yuko baised kwa makala zake nyingi akionyesha dhahiri yupo upande gani hata kwa jambo ambalo hapaswi kuonyesha upendeleo.
Aliandika makala moja ya kuonyesha wazi kwamba haipendi CHADEMA na nilimtumia sms kumwomba anipe E-mail yake ili tuwasiliane vizuri hukufanya hivyo.
Kama mwanajamii mmoja alivyosema katika kuchangia mada hii inaonekana huyu Dilunga ama ana njaa na yupo kwenye pay roll ya sisiem au kaubongo kake kako finyu kidogo. Sasa kesi ipo mahakamani halafu anataka waliohusika waombe radhi kabla hawajaambiwa na mahakama kuwa wametenda kosa, waombe radhi ya nini?
Huu udhaifu wa viongozi wa CHADEMA anaouzungumzia Dilunga ni upi? Udhaifu wa "kutokemea vitendo vya kihuni vilivyofanywa na wafuasi wa CHADEMA" Vitendo gani vya kihuni, hivi Dilunga alikuwepo kwenye tukio au amesoma taarifa kwenye vyombo vya habari? Kwenye makala zake huwa kuna picha yake, ni kijana ambaye anavyoonekana huwezi kufikiri kuwa ana upeo mdogo kiasi hiki wa kuchambua mambo.
Bwana mdogo Dilunga hebu tupatie E mial yako tunaweza kueleweshana baadhi ya mambo kwa gharama ndogo sana.
 
Chenge hajapelekwa mahakamani kwa wizi wa rada,mkapa karudisha kiwira kimyakimya bila kufikishwa mahakamani,mbunge wa kike wa cuf kakamatwa naaskari wa kiume na kudhalilishwa hakuna aliyefunguliwa mashtaka wa kuomba radhi,wabunge wa chadema wamedhalilishwa na vyombo vya dola bila halali.
Mbunge wa ccm kanda ya ziwa alizuiliwa kukamatwa kwa madai anakinga ya kutoshtakiwa.
 
Huyu dc akapimwe kwanza kujua jinsia yake maana sura yake inachanganya sana!
 
Watafiti walisema mapema kabla ya kuanza kampeni kwamba kuna vyombo vya habari na baadhi ya waandishi watanunuliwa na CCM. Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Yametimia!!!. CDM kama wana wa Israeli, Mungu anasema "Endeleeni kusonga mbele kuelekea nchi ya ahadi, nchi ya asali na maziwa Kaanan ya Afrika (Tanzania).
 
Halafu tukisema CHADEMA kimejaa wahuni kuanzia viongozi wake....Wapuuzi wengine humu wanaendelea kubisha. aaakhkhkhkh...puh!
CCM ndo imejaaaa wahuni,wez,wajinga wanaoendelea kuvimbisha mitumbo yao bila kujua kuna wananchi wanalala njaa.Nangushangaa sana kuwa anti-maendeleo
 
Godfrey Dilunga tuambie ni njaa au ushabiki ndio unaokusumbua? Hii ni mara ya pili unatoa uchambuzi hafifu uliojaa ushabiki usiona maana. Nakumbuka ulitoa mada ya kupinga hotuba ya Lema bungeni aliyotoa kama waziri kivuli wa Mambo ya Ndani. Leo bila aibu unarudia upupu mwingine. Mbona unalidharirisha gazeti ambalo linaheshimika sasa hapa nchini!

Hawezi kukuambia kama ni njaa ama ni ushabiki lakini ukiisoma hiyo stori kwa makini na kama ni mfuatiliaji wa gazeti la raia mwema in particular makala za dilunga utagundua kwamba yuko upande wa magamba. Anatumia nafasi yake ya kuwa mwandishi wa habari katika gazeti makini kupitisha agenda yake. Sina shaka kama anadhani waliomkamata dc wa igunga akifanya hujuma dhidi ya chadema ni wahuni basi atambue kwamba yeye dilunga ndiye mhuni kwa kushabikia uhuni unaofanywa na viongozi wa serikali.
 
pole RAIA MWEMA kwa kutumiwa na ccm kama KONDOM mkitumika mtatupwa chooni tena kwa kinyaa kwa sasa hadhi yenu inaporomoka siku hadi siku
 
hah, lakini sheria si zinajulikana, kama eneo ni kwa mkutano wa chama fulan kwa nini wewe wa chama kingine ukaendelee na shughuli za chama chako katika maeneo hayahayo. TUJIFUNZE KUTOKANA NA HILO
 
Pamoja na uhuni huu walio uonesha Igunga inashangaza bado Chadema kinajiita ni Chama Makini! Chadema wanatumia akili za makalio kufikiria!
Wewe ndugu si ulisema ni mtumishi wa Mungu au siyo wewe nakosea? Mbona maneno yako siyo. Wewe kwa simple mind chadema ndo wenye makosa?

Jamani tuache unafiki tuwe wakweli na Mungu ni shahidi katika hili. Mimi sitakaa niamini katika hizi propaganda za CCM kwa sababu ninajua chadema ni watu makini kuliko CCM.
 
DC Igunga amefichua udhaifu wa CHADEMA?

Godfrey Dilunga, Raia Mwema, 21 Sep 2011 Toleo na 204.

JE, kitendo cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutokemea udhalilishaji dhidi ya Mkuu wa Wilaya (DC) ya Igunga, Fatuma Kimario, uliofanywa na ‘wahuni' wanaodaiwa ni wafuasi wa chama hicho, ni udhaifu? Je, ni udhaifu, hata kama hiki ni kipindi cha kampeni za uchaguzi wa ubunge Jimbo la Igunga?
Je, CHADEMA kujidai ‘kutoona' udhalilishaji ule eti tu kwa sababu DC naye anayo makosa yake ni udhaifu? Je, ni udhaifu katika misimamo ya kifalsafa au kimtazamo? Je, ni matukio gani mengine kuhusu CHADEMA yanayothibitisha udhaifu huu? Tujadili.

Kimsingi, CHADEMA kimeonyesha udhaifu. Ni udhaifu wa kujitetea kwa gharama yoyote ikiwamo kufumbia macho makosa yake dhidi ya raia wengine. Kuna hatari au dalili, chama hiki kinaanza kulewa. Ni ulevi wa kuamini wakati fulani kinaweza kuwa juu ya sheria kwa kauli mbiu ya ‘nguvu ya umma' isiyo halisi.
Wahuni wanaodaiwa wafuasi wa CHADEMA wamevamia kikao cha DC, Fatuma Kimario. Wakamkamata, wakampekua na kumdhalilisha (kwa maelezo ya awali). Vitendo hivi vimefanyika baada ya wahuni hao kuhisi hujuma. Eti siku hizi ukihisi tu, basi sheria zinakuruhusu kuvamia, kukamata na kupekua, tena bila kibali cha mamlaka husika? Hisia tu? Vipi, siku wahuni wengine wakihisi, kitu cha ovyo ofisi za CHADEMA na kuvamia?
Hisia ambazo ni chanzo cha uvamivi huo dhidi ya DC kujengewa uhalali au kutetewa kwa sababu tu karatasi ya ajenda za kikao cha DC zimehusisha agenda ya uchaguzi mdogo wa Igunga, ni jambo la kushangaza. Je, mkuu wa wilaya ambayo imo kwenye uchaguzi mdogo, anakatazwa kwa sheria gani kujadili suala hilo katika muktadha wa kiutawala? Sidhani kama hii ni sababu ya msingi.
Lakini ipo sababu ya muda wa mkutano, Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini wa Jeshi la Polisi, Issaya Mungulu, anasema CHADEMA walichelewa ratiba yao iliyokuwa kati ya saa nne hadi saa sita na DC mkutano wake ulikuwa saa nane. Hapa, nakala ya ratiba ndiyo muamuzi bado sijaipata na hivyo, sitajadili.
Hata hivyo, kuna udhaifu ndani ya CHADEMA. Tunaelezwa na Mungulu katika tukio hilo, DC alivuliwa hijabu, viatu, alikatiwa mkufu, achilia mbali simu yake kupotea. Inadaiwa pia DC alidhalilishwa kwa kutukanwa.
Kwa maelezo haya, ambayo ni dhahiri DC alifanyiwa vurugu kama ambavyo baadhi ya picha za magazeti ya zilivyoonesha tukio hilo, CHADEMA walipaswa kuonyesha ujasiri wa kimaadili, nidhamu, mila na desturi za kitanzania, kinyume chake wameonyesha udhaifu.
Walipaswa kueleza makosa ya DC lakini wakati huo huo, nilitaraji waombe radhi kwa vitendo vingine visivyo vya kimaadili wala vya kisheria dhidi ya DC huyo.
Tukumbushane. Wakati Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alipotuhumiwa kudharau Mahakama mkoani Arusha ambako anayo kesi, Mahakama hiyo ilitoa amri akamatwe. CHADEMA kilipinga amri hiyo ya Mahakama kuwa, utekelezaji wake unakiuka sheria, mila na desturi za miaka mingi zinazohusu kinga, haki na madaraka ya Bunge.
Lakini katika taarifa iliyotolewa na Tundu Lissu, kwa upande mwingine,CHADEMA kwa kutumia jina la Kambi ya rasmi ya Upinzani, ililalamika kwa nini Mbunge wa Busega, Dk. Titus Kamani, alikamatwa baada ya taratibu za kisheria kufuatwa na Mbowe akamatwe bila taratibu hizo?
Kwamba, Dk. Kamani ambaye anatuhumiwa kupanga mauaji kwanini kabla ya kukamatwa, polisi walifuata utaratibu kwa kuomba kibali cha Bunge, wakati Mbowe anataka kukamatwa bila kibali cha Bunge?
Mantiki hapa ni kwamba, Lissu alikuwa akisisitiza umuhimu wa kufuata sheria na taratibu. Kwamba, utaratibu wa kumkamata mbunge ni lazima uwe na idhini ya Bunge, ingawa pia uongozi wa Bunge ulifafanua suala hilo kwa maelezo ya kina.
Kwa kuzingatia mantiki hiyo ya Lissu kusisitiza utiifu wa sheria na taratibu tujiulize. Je, hatua ya kuvamia mkutano wa DC, kumkamata, kumpekua (kwa kutumia vijana wa kiume) kumezingatia taratibu kisheria? Je, ni halali kuvunja taratibu za kisheria kwa sababu tu, DC naye amezivunja?
Lakini kama taratibu za kisheria hazikuzingatiwa katika kumvamia DC, kwa nini CHADEMA leo hii inakosa ujasiri wa kuomba radhi kwa makosa yake? Na kama haiombi radhi, kwa nini isiwakane wahusika? Kwa kuzingatia tukio la DC kuvamiwa na hili la Mbowe kutaka kukamatwa bila kibali; Je, uzingatiaji wa sheria na taratibu ni muhimu wakati gani kwa upande wa CHADEMA?
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika


JAMANI MAMBO HAYO NA reserve comment zangu kwa sababu naweza kua bias wenzangu semeni
Mkuu umezungumza mengi sana kuonyesha udhaifu wa Chadema lakini pia umefanya makosa makubwa kuhusisha tukio hilo na chama lakini aliyoyafanya Dc kwa niaba ya chama hayahusiani na CCM isipokuwa unatazama haki ya Dc na sii ile ya wasimamizi wa kura wa Chadema jimbo la Igunga.

Sasa ningekuomba uandike upya Mahala penye mhusika mtaje jina lake iwe anatoka Chadema au CCM na kazi yake au mamlaka alokabidhiwa na kama unataka kutumia majina ya vyama pia ondoa jina la DC weka jina la chama kwa sababu wale waliomvamia walifanya haya kwa niaba ya chama na ndio maana umetumia jina la Chadema badala ya majina ya wahusika na mamlaka waliyokabidhiwa, hali huyu mama Dc alifanya aloyafanya kwa niaba ya CCM hivyo weka jina la CCM na sii jina lake. Kesi iko mahakamani na mshtakiwa sii Chadema!
 
Bosi wako kaona haya makala. nadhani kwa sasa mntaka muishi kwa Ruzuku si biashara. Mwandishi wa habari hutakiwi kuwa shabiki. Sijui kanuni zanu za kiproffession zinasemaje?.
 
Huyu mwandishi anaonekana kabisa anaganga njaa! Sura yenyewe imempauka utafikiri amekula mihogo mibichi. Sijamkawiza nilimtumia sms kumwonyesha alivyo mjinga. Kilaza tu huyu hana lolote.
 
nivi kweli unaweza kutukana watu wote tuliyoipigia chadema kura, ee muumba msamehe huyu mtu, nilitaka kukutukana na nitoweke humu jamvin lakini uwepo wa mungu umezuia hili,,,,,,,, mungu akusamehe
Halafu tukisema CHADEMA kimejaa wahuni kuanzia viongozi wake....Wapuuzi wengine humu wanaendelea kubisha. aaakhkhkhkh...puh!
 
Yule DC amepata bonge la lesson! watu wanang'angana kupigana na wakati!....Ujumbe umefika, kama wezi wa siku za kichina wanachomwa moto tufanyeje kwa wezi wa Haki na Democrasia?....Safari ndo kwanza imeanza, wala si suala la Chadema, ni ishu ya Wananchi tunaoimua, very soon tutaanza kuwashikisha adabu wanaouza chakula cha msaada, tutawaburuta wanaokula pesa sa miradi ya maendeleo na tutawakimbiza mchakamchana wanaozika utu wetu kwa propaganda kavu za "udini wao"....
 
Godfrey Dilunga tuambie ni njaa au ushabiki ndio unaokusumbua? Hii ni mara ya pili unatoa uchambuzi hafifu uliojaa ushabiki usiona maana. Nakumbuka ulitoa mada ya kupinga hotuba ya Lema bungeni aliyotoa kama waziri kivuli wa Mambo ya Ndani. Leo bila aibu unarudia upupu mwingine. Mbona unalidharirisha gazeti ambalo linaheshimika sasa hapa nchini!

Huyu ameshahongwa na magamba kuleta makala za kipuuz. Watu kama hawa ni wasaliti tu.
 
Back
Top Bottom