DC Igunga amefichua udhaifu wa CHADEMA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DC Igunga amefichua udhaifu wa CHADEMA?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BabieWana, Sep 23, 2011.

 1. B

  BabieWana Senior Member

  #1
  Sep 23, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 173
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  DC Igunga amefichua udhaifu wa CHADEMA?

  Godfrey Dilunga, Raia Mwema, 21 Sep 2011 Toleo na 204.

  JE, kitendo cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutokemea udhalilishaji dhidi ya Mkuu wa Wilaya (DC) ya Igunga, Fatuma Kimario, uliofanywa na ‘wahuni’ wanaodaiwa ni wafuasi wa chama hicho, ni udhaifu? Je, ni udhaifu, hata kama hiki ni kipindi cha kampeni za uchaguzi wa ubunge Jimbo la Igunga?
  Je, CHADEMA kujidai ‘kutoona’ udhalilishaji ule eti tu kwa sababu DC naye anayo makosa yake ni udhaifu? Je, ni udhaifu katika misimamo ya kifalsafa au kimtazamo? Je, ni matukio gani mengine kuhusu CHADEMA yanayothibitisha udhaifu huu? Tujadili.

  Kimsingi, CHADEMA kimeonyesha udhaifu. Ni udhaifu wa kujitetea kwa gharama yoyote ikiwamo kufumbia macho makosa yake dhidi ya raia wengine. Kuna hatari au dalili, chama hiki kinaanza kulewa. Ni ulevi wa kuamini wakati fulani kinaweza kuwa juu ya sheria kwa kauli mbiu ya ‘nguvu ya umma’ isiyo halisi.
  Wahuni wanaodaiwa wafuasi wa CHADEMA wamevamia kikao cha DC, Fatuma Kimario. Wakamkamata, wakampekua na kumdhalilisha (kwa maelezo ya awali). Vitendo hivi vimefanyika baada ya wahuni hao kuhisi hujuma. Eti siku hizi ukihisi tu, basi sheria zinakuruhusu kuvamia, kukamata na kupekua, tena bila kibali cha mamlaka husika? Hisia tu? Vipi, siku wahuni wengine wakihisi, kitu cha ovyo ofisi za CHADEMA na kuvamia?
  Hisia ambazo ni chanzo cha uvamivi huo dhidi ya DC kujengewa uhalali au kutetewa kwa sababu tu karatasi ya ajenda za kikao cha DC zimehusisha agenda ya uchaguzi mdogo wa Igunga, ni jambo la kushangaza. Je, mkuu wa wilaya ambayo imo kwenye uchaguzi mdogo, anakatazwa kwa sheria gani kujadili suala hilo katika muktadha wa kiutawala? Sidhani kama hii ni sababu ya msingi.
  Lakini ipo sababu ya muda wa mkutano, Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini wa Jeshi la Polisi, Issaya Mungulu, anasema CHADEMA walichelewa ratiba yao iliyokuwa kati ya saa nne hadi saa sita na DC mkutano wake ulikuwa saa nane. Hapa, nakala ya ratiba ndiyo muamuzi bado sijaipata na hivyo, sitajadili.
  Hata hivyo, kuna udhaifu ndani ya CHADEMA. Tunaelezwa na Mungulu katika tukio hilo, DC alivuliwa hijabu, viatu, alikatiwa mkufu, achilia mbali simu yake kupotea. Inadaiwa pia DC alidhalilishwa kwa kutukanwa.
  Kwa maelezo haya, ambayo ni dhahiri DC alifanyiwa vurugu kama ambavyo baadhi ya picha za magazeti ya zilivyoonesha tukio hilo, CHADEMA walipaswa kuonyesha ujasiri wa kimaadili, nidhamu, mila na desturi za kitanzania, kinyume chake wameonyesha udhaifu.
  Walipaswa kueleza makosa ya DC lakini wakati huo huo, nilitaraji waombe radhi kwa vitendo vingine visivyo vya kimaadili wala vya kisheria dhidi ya DC huyo.
  Tukumbushane. Wakati Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alipotuhumiwa kudharau Mahakama mkoani Arusha ambako anayo kesi, Mahakama hiyo ilitoa amri akamatwe. CHADEMA kilipinga amri hiyo ya Mahakama kuwa, utekelezaji wake unakiuka sheria, mila na desturi za miaka mingi zinazohusu kinga, haki na madaraka ya Bunge.
  Lakini katika taarifa iliyotolewa na Tundu Lissu, kwa upande mwingine,CHADEMA kwa kutumia jina la Kambi ya rasmi ya Upinzani, ililalamika kwa nini Mbunge wa Busega, Dk. Titus Kamani, alikamatwa baada ya taratibu za kisheria kufuatwa na Mbowe akamatwe bila taratibu hizo?
  Kwamba, Dk. Kamani ambaye anatuhumiwa kupanga mauaji kwanini kabla ya kukamatwa, polisi walifuata utaratibu kwa kuomba kibali cha Bunge, wakati Mbowe anataka kukamatwa bila kibali cha Bunge?
  Mantiki hapa ni kwamba, Lissu alikuwa akisisitiza umuhimu wa kufuata sheria na taratibu. Kwamba, utaratibu wa kumkamata mbunge ni lazima uwe na idhini ya Bunge, ingawa pia uongozi wa Bunge ulifafanua suala hilo kwa maelezo ya kina.
  Kwa kuzingatia mantiki hiyo ya Lissu kusisitiza utiifu wa sheria na taratibu tujiulize. Je, hatua ya kuvamia mkutano wa DC, kumkamata, kumpekua (kwa kutumia vijana wa kiume) kumezingatia taratibu kisheria? Je, ni halali kuvunja taratibu za kisheria kwa sababu tu, DC naye amezivunja?
  Lakini kama taratibu za kisheria hazikuzingatiwa katika kumvamia DC, kwa nini CHADEMA leo hii inakosa ujasiri wa kuomba radhi kwa makosa yake? Na kama haiombi radhi, kwa nini isiwakane wahusika? Kwa kuzingatia tukio la DC kuvamiwa na hili la Mbowe kutaka kukamatwa bila kibali; Je, uzingatiaji wa sheria na taratibu ni muhimu wakati gani kwa upande wa CHADEMA?
  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika


  JAMANI MAMBO HAYO NA reserve comment zangu kwa sababu naweza kua bias wenzangu semeni
   
 2. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chadema wataomba radhi kwa kosa lipi! Kwani kesi ilishaisha mahakamani na kuwatia hatiani watu wanaodaiwa kumdhalilisha! Na kama ikija hukumu ikaonekana kwamba wale watu hawana hatia kwa hiyo Chadema wawaombe nao msamaha kwa kuwachafulia majina! Tumia akili acha kutumia masaburi kufikiri. Chadema ni chama makini hakikurupuki kama serikali ya JK, mara hatuwatambui waasi wa Libya mara aibu.
   
 3. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Raia Mwema kumbe nao wako kwenye mgao wa 35M.
   
 4. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Godfrey Dilunga tuambie ni njaa au ushabiki ndio unaokusumbua? Hii ni mara ya pili unatoa uchambuzi hafifu uliojaa ushabiki usiona maana. Nakumbuka ulitoa mada ya kupinga hotuba ya Lema bungeni aliyotoa kama waziri kivuli wa Mambo ya Ndani. Leo bila aibu unarudia upupu mwingine. Mbona unalidharirisha gazeti ambalo linaheshimika sasa hapa nchini!
   
 5. J

  John Marwa JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pamoja na uhuni huu walio uonesha Igunga inashangaza bado Chadema kinajiita ni Chama Makini! Chadema wanatumia akili za makalio kufikiria!
   
 6. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Wewe ndiye Wilson Mkama haswa.Umechoma banda la yule mjinga mjinga kisha ukaenda kubandika kikaratasi chako ujinga uliovuka mipaka
   
 7. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Dilunga kaandika akiwa so biased,inashangaza mwandishi kushindwa kubaini exagerations of the story iliyofanywa kwa maslahi ya kikundi/ccm kikampeni nae kuibuka nayo kama ilivo,raise doubt kwamba pengine nae analinda/tumikia kitumbua flani
   
 8. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Halafu tukisema CHADEMA kimejaa wahuni kuanzia viongozi wake....Wapuuzi wengine humu wanaendelea kubisha. aaakhkhkhkh...puh!
   
 9. PPM

  PPM JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Rubish!!!!
   
 10. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  acha porojo...
   
 11. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mwandishi uyu aende akavalishwa kanga na apande kwenye jukwaa la CCM ahubiri yale aliyoyaandika katika gazeti
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hilo ndilo raia mwema ambalo limetiwa mkononi na magamba.
   
 13. M

  Molemo JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  ni sera mpya ya gazeti la Raia mwema kuiandama chadema.
   
 14. M

  Molemo JF-Expert Member

  #14
  Sep 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  mmelinunua hili gazeti kwa bei gani?
   
 15. M

  Molemo JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  zamani habari kama hii huiwezi kuikuta kwenye Raia Mwema.
   
 16. M

  Molemo JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  gazeti la RAI ni makini kuliko Raia mwema sasa hivi.
   
 17. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #17
  Sep 23, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Wewe umebadili jina Mwita25 au ni ndg yake, wote mpo kwenye PayRoll ya maghamba's pole!!!!!!!!!!
   
 18. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #18
  Sep 23, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Kwani Raia Mwema nalo pia mwana harakati Generali Ulimwengu kaliuza kama Rai na mengine?????????????
   
 19. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #19
  Sep 23, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  du.... sikumbuki siku ile ya arusha josehine alivyo nyanyasika na mimba yake waliandika nini ?wabunge wa chadema kuwekwa ndani kwa jambo linaloruhisiwa dhamana huo sio uthalilishaji ? mbona huandiki serikali kutumia pesa vibaya kuwapeleka wabune wabunge cdm tabora? hayo ni machache ukitaka manyanyaso dhidi ya cdm mbona ni mengi...umekomaan mkuu wa wilaya mchokozi sijui hana mume eti kavuliwa hijabu ..hata mashuleni zimepigwa marufuku kwanza sio fazi rasmi za kazi...hatu upepo mkali hijabu itapeperushwa tu
   
 20. ngorope

  ngorope JF-Expert Member

  #20
  Sep 23, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,113
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuki mtamu....... mara nyingi tumeona viongozi wa upinzani wakitendewa udhalilishaji mkubwa kuliko huo wa kupika lakini hamkukemea nyie mliopewa dhamana ya kuuelimisha umma, mkiwa na jina zuri Raia Mwema. Hayo ni matokeo ya upotoshaji mnaoufanya waandishi wa habari mnaotumikia matumbo badala ya umma subiri siku yaja sio DC hata Rais atapambana na nguvu ya umma kama ilivyompata Hosn Mbarak kule Egypt.
   
Loading...