Hivi si mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya wilaya? Si trafick ya wilaya yote iko chini yake? Kwanini akaongoze magari yeye? Je anajua sheria za kuongoza magari? Hii serekali ya awamu ya tano ni serekali ambayo haina mwelekeo kabisa, baba akishapoteza mwelekeo na Watoto nao huwa hohe hahe! Nadhani anachofanya slow slow ni sawa kabisa
Nimesoma majibu mengi ya watu wanaopinga kitendo hiki cha Mkuu wa wilaya Mhe Pole pole kuongoza magari katika msongamano, tena baadhi yao wana ushawishi mkubwa kuwa kakosea sana. Ila nimegundua kuwa wengi wao ni vijana wenye umri mdogo ambao hawafahamua vyema wajibu wa raia.
Hivi inapotokea ajali katika barabara kuu na raia akaamua kuchukua majani kuweka alama barabarani kuwataarifu madereva kupunguza mwendo inahitaji awe amesomea sheria za usalama barabarani kufanya hivyo? kwa taarifa yenu kazi hizo tumekuwa tukizifanya sana ili kuwasaida watanzania wanaonasa katika foleni katika barabara ya Morogoro.
Ni vyema tukatambua kuwa ulinzi na usalama ni wajibu wa kila raia mwema. Na hapo zamani ilikuwepo mipango ya kuhakikisha kila raia anapata mafunzo "basi"c ya ulinzi na usalama.
Wakati huo likitokea tukio lolote hata kwa kutazamana tu raia waliweza kupeana ishara ya nini kifanyike kupunguza makali "mitigation of impact" wakati vikisubiriwa vyombo vya dola
Kwa upande wangu nimefurahishwa zaidi kugundua kuwa DC Pole pole anaweza kufikia hatua hiyo. Hivyo kama dereva nichukue fursa hii kumpatia ushauri ufuatao:-
1. Chanzo kikubwa cha foleni pale Kimara mwisho ni madereva wa daladala kuamua kuegesha magari yao mwisho wa kituo badala ya kuingiza magari ndani ya kituo hata kama nafasi ipo. Baada ya daladala moja kuegesha hapo mwishoni, hufuata nyingine na nyingine na nyingine sasa zikiegesha katika upande mmoja wa barabara huku zote zikipiga debe kutafuta abiria kwa kipindi kirefu sana. Hivyo kufanya pale Kimara mwisho kutumika barabara moja badala ya mbili na msongamano wa magari huanzia hapo nyakati za jioni na kukua kadri muda unavyoendelea.
Nilifanya utafiti kidogo kutaka kugundua ni kwanini madereva wa daladala huegesha mwisho wa kituo badala ya kuingiza magari ndani ya kituo hata kama nafasi ipo? Niligundua kuwa hata sisi abiria ambao ndio waathirika wakubwa wa hizi foleni tunachangia sana kwa kusimama mwisho wa kituo badala ya kuingia ndani ya kituo na kusimama kusubiri usafiri.
Nilifanya pia utafiti katika vituo vingi vya daladala katika barabara ya Morogoro nikagundua abiria na daladala wote husimama mwisho wa kituo badala ya mwanzo au katikati ya kituo, hivyo utakuta daladala inashusha au kupakia abiria ikiwa mwisho kabisa wa kituo huku sehemu ya gari ikiwa iko barabarani au kuzuia njia ya watembea kwa miguu ambayo mara nyingia magari hutumia kwa dharura. Jambo hili ni hatari sana kwa barabara kama ya Morogoro ambayo magari hutembea kwa mwendo wa kasi kubwa.
Hivyo pande zote mbili yaani abiria na madereva wa daladala wanahitaji kupatiwa elimu kuhusu namna abiria wanavyopaswa kusimama kusubiri mabasi na madereva wanavyotakiwa kuegesha magari yao.