DC Ally Hapi aingilia kati Mandojo kuvunjiwa nyumba

Lee Swagger

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
1,070
Reaction score
1,816
Mkuu Wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ametoa saa 48 kwa watu wote walioshiriki kumuuzia kiwanja mwanamuziki wa Bongo Fleva, Joseph Francis (Mandojo) kujisalimisha kwake.

Pia amelitaka Jeshi la Polisi kuwakamata endapo hawatajisalimisha ndani ya muda huo.
FB_IMG_1522495007038.jpg
 
Kwani mandojo pekee ndiyo mwenye shida

Ova
 
"Nitamlipia kodi ya miezi sita Man Dojo ili ajisitiri kwa muda baada ya nyumba yake hii aliyokuwa anaishi awali kubomolewa hivi karibuni wakati suala lake linapatiwa ufumbuzi,"- Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,
 
hayo ndio malupulupu ya umaalufu wale wengine Mungu awaangalie katika hili
 
Mkuu Wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ametoa saa 48 kwa watu wote walioshiriki kumuuzia kiwanja mwanamuziki wa Bongo Fleva, Joseph Francis (Mandojo) kujisalimisha kwake.

Pia amelitaka Jeshi la Polisi kuwakamata endapo hawatajisalimisha ndani ya muda huo.View attachment 730298
haka nako ni kapuuzi kengine haka. zilivunjwa nyumba kimara hakajapanua midomo yake .juzi kanaongea kama vile ukiwa mkuu wa wilaya unakuwa gavana kwamba unaweza kutunga sheria zako... ati ukija kinondoni unafanyiwa mitihani upya! we na ka degree kako kamoja kakudesa utaweza kumfanyia mtihani PhD holder wewe? au unadhani wote waliopo kwenye utumishi ni mbumbumbu kama bashite?
 
Kuna watu wanalala njee mpaka leo. Ila amemwona huyo tu.
Sijui ni nyotaa hahahhaaha
 
*TAARIFA YA DC HAPI KUMTEMBELEA MSANII MAN DOJO ALIYEBOMOLEWA NYUMBA YAKE*

Leo asubuhi nimefika alipokua akiishi msanii Man Dojo.Taarifa ya awali inaonesha kuwa eneo alilojenga kuna viwanja vitatu ambavyo vina hati na kuna watu walipewa mwaka 2003.Mwaka 2013 viwanja hivyo vikiwa havijaendelezwa,Man Dojo aliuziwa na mtu aliyedai ni mmiliki wa eneo hilo kwa Tsh milioni 3 wakimuaminisha kuwa ni mali yao.

Wenye hati wameeleza kuwa walifungua kesi na kushinda katika Baraza la ardhi la wilaya, hivyo kupata amri ya kubomoa.
Baada ya yake kubomolewa, kwa sasa Man Dojo na familia yake wanalala nje.

Baada ya kuona na kusikiliza mechukua hatua zifuatazo kwa awali:-

1. Nimeelekeza Man Dojo atafute nyumba ya kujistiri yeye na mkewe eneo la Mbweni kwa kipindi cha mpito ambayo nitamlipia kwa miezi sita.

2. Nimeagiza wote waalioshiriki kumtapeli Man Dojo kwa kumuuzia kiwanja huku wakijua si mali yao wakamatwe na jeshi la Polisi haraka iwezekanavyo.Kitendo walichofanya ni jinai na lazima washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.

3. Nimemuita Man Dojo ofisini kwangu siku ya jumanne saa 4 asubuhi na wenzie ambako tutafanya kikao na mashauriano na wataalam wa ardhi wa manispaa na uongozi wa kata ya Mbweni ili kujiridhisha kiini cha jambo hili, kupitia nyaraka zote na kuona namna tutakavyomsaidia kwa kutumia HEKIMA, BUSARA NA UBINADAMU.

4. Nimeagiza, Mkurugenzi kupitia idara ya ardhi na Mipangomiji Kinondoni kuniletea taarifa ya watu wote waliopewa viwanja kwa kuanzia na Mbweni ambao hawajaendeleza viwanja vyao hadi sasa (kama masharti ya hati yanavyowataka).

Kutoendeleza viwanja kunatoa mwanya kwa matapeli kuwatapeli wananchi wenye shida ya dhati ya ardhi ya kujenga makazi kama ilivyokua kwa ndugu yetu.

Wako watu walipewa viwanja mwaka 2003 lakini hadi leo wameshindwa kusafisha na kuendeleza viwanja vyao.Badala yake viwanja hivyo vimekua vichaka na maficho ya wahalifu.

5. Siku ya jumatano wiki ijayo nitazungumza na umma juu ya nini kimejiri katika kikao changu cha jumanne na namna gani tutamsaidia na kumshauri Man Dojo.

Nafahamu jinsi ilivyo taabu kujenga, nafahamu jinsi kazi ya sanaa ilivyo ngumu hadi kudunduliza na kujenga.
Lakini nawaasa wananchi wote wa Kinondoni kuchukua tahadhari na kujiridhisha kabla ya kufanya manunuzi yoyote ya kiwanja.
Ni vyema kupata ushauri kwa wataalam wetu wa ardhi kabla ya kununua kiwanja na kuanza ujenzi.
*DC HAPI*
 
Siku hizi bwana kila kiongozi anatafuta kiki kama ukipatwa janga una ka umaarufu kidogo katakapompa kiongozi kiki basi atapita mle mle.
Amefanya vizuri kumsaidia sema angemsaidia kimya kimya sasa kuzungumza na umma juu ya kubomolewa mandojo sioni mantiki hapo unless lingekuwa janga la wengi
 
Badala ya kuagiza upimaji wa viwanja vya kutosheleza mahitaji ya wananchi katika halmashauri yako ili wahitai wavipate kwa urahisi na haraka ili wasitapeliwe umeagiza orodha ya viwanja vilivyopimwa........

Haya

Acha nipite hivi=====>>>>>>
 
Kupima ni gharama juu sana.
 
Back
Top Bottom