DC adai talaka mbili kwa mpigo mahakamani

DC adai talaka mbili kwa mpigo mahakamani

Balaa tupu
Huyo mwanamke namshangaa,akubali hiyo talaka.Huyo mkuu wa wilaya nae si akafunge ya serikali ? Maana baada ya hiyo ana ndoa nyingine ya serikali ambayo pia anatoa talaka. Ila hii kesi itafundisha wengi. Ngoja tuone mwisho wake.
 
Hakuna,labda kwenye urithi mme akifa. Ila masuala ya kifo huwezi jua nani atatangulia. Maana kama hakuna mapenzi tena,hakuna tendo la ndoa. Hiyo ndoa ya nini sasa?
Huyo mwanamke ni gold digger.
Ana mshefa ana mfadhili na bado anataka hela ya Odunga.
 
DC aeleza sababu ya kuomba talaka
Thursday August 15 2019

Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga amedai kuwa huwa anatoa matunzo ya mtoto wao wa kike ambaye kwa sasa anasoma kidato cha sita aliyezaa na Medelina Mbuwuli aliyefunga naye ndoa ya Kikristo mwaka 2001.

Mkuu wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, Simon Odunga (aliyevaa suti) akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Mwazo iliyopo Ukonga Jijini Dar es salaam jana. Picha na Omar Fungo
BY Tausi Ally, Mwananchi tally@ mwananchi.co.tz

Advertisement
Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga amedai kuwa huwa anatoa matunzo ya mtoto wao wa kike ambaye kwa sasa anasoma kidato cha sita aliyezaa na Medelina Mbuwuli aliyefunga naye ndoa ya Kikristo mwaka 2001.

Alidai hayo jana katika Mahakama ya Mwanzo Ukonga alipokuwa akitoa ushahidi katika kesi ya madai ya talaka namba 181 ya mwaka huu aliyoifungua katika Mahakama ya Mwanzo Ukonga, Dar es Salaam.

Odunga, akitoa ushahidi huo mbele ya Hakimu, Christina Luguru alisema anaomba talaka kwa sababu ametengana na mkewe huyo tangu mwaka 2003 na kwamba katika maisha yao ya ndoa, walikuwa wakigombana mara kwa mara kiasi cha kutengana na kipindi chote hicho alikuwa hana kazi. Alidai kuwa ilipofika mwaka 2002 alipata kazi akapanga nyumba eneo la Makuburi akamfuata mkewe wakasuluhishwa na wakarudiana kuishi pamoja.

“Baada ya kusuluhishwa tuliishi hadi mwaka 2003 pamoja, lakini hatukuwa na maelewano, siku moja nilipokuwa kazini mke wangu aliamua kuhama nyumba bila kunitaarifu.”

Alidai kuwa baada ya mama huyo kuondoka, alikaa na familia yake wakashauriana kuwa amtafute kwa ajili ya kumtunza mtoto na wakati huo alikuwa anasoma shule ya awali.


Alidai kuwa aliwahi kwenda katika shule ya awali aliyokuwa akisoma mtoto wao na kukuta ameandikishwa kuwa ana mzazi mmoja na kwamba baba yake alishakufa hivyo alikataliwa.

“Nilirudi kwa familia za pande zote mbili tukafanya kikao na mke wangu aligoma kuishi na mimi akidai niendelee kumtunza mtoto, kikao kiliamua nimpatie talaka, hatua ambayo sikuitekeleza hadi sasa ninapoiomba hapa mahakamani,” alieleza Odunga.

“Ila nimekuwa nikipeleka matunzo ya mtoto nyumbani kwake, lakini kuna siku nilishambuliwa, nikazuiliwa kwenda.”

Alidai kuwa amekuwa akimlea mtoto wake kwa tabu kwa sababu mdaiwa hataki aende nyumbani kwake, lakini ameendelea kutoa huduma kama ada kwa kumpatia mama yake. Alidai pia kwamba mtoto huyo alifaulu lakini mama yake alimpeleka shule binafsi, “hivyo nilikuwa nikitoa huduma kulingana na uwezo wangu.”

Kutokana na maelezo hayo, aliomba mahakama iivunje ndo hiyo kwa kuwa ilishindikana kusuluhishwa ngazi ya familia ambayo ilimpatia baraka ya kutoa talaka.

Baada ya Odunga kutoa ushahidi huo, Medelina alimuuliza kama alishawahi kwenda kanisani kabla ya kufika mahakamani na alijibu kuwa alienda mwaka 2001 na 2003.

Medelina alimuuliza tena Odunga kama alikuwa akitoa ada ya shule ya mtoto tangu mwanzo, anaweza kukumbuka jina la shule aliyokuwa akisoma mtoto wao na kujibu kuwa hakumbuki ila anajua mahali ilipo na sasa hajui anasoma wapi.

Alimuuliza tena kama anaweza kuithibitishia mahakama hata kwa risiti za ada na Odunga alidai kuwa alikuwa akimpa fedha taslimu.

Shahidi wa Odunga, Godol Odunga (61) maarufu Ogonda alidai kuwa mdai na mdaiwa walifunga ndoa ya Kikristo lakini hakumbuki ilikuwa lini na mwaka 2003 walitengana na kila mmoja aliishi peke yake.

Alidai kuwa kati ya mwaka 2012 na 2013 kikao cha ukoo kilikaa na Odunga alidai kuwa anataka kuoa mke mwingine na akaagizwa kama anataka hiyo atoe talaka kwanza.

Baada ya kutoa ushahidi huo, Medelina alimuuliza wewe ni mtumishi wa Mungu ulishawahi kuona ndoa ya kanisani inavunjwa mahakamani? Shahidi huyo akajibu, “mimi nasema ninachojua.”

Odunga alifunga ushahidi wake na kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa Medilina na mashahidi wake watano Agosti 19.

Kesi nyingine ya madai ya talaka iliyofunguliwa na Odunga mahakamani hapo dhidi ya ndoa aliyoifunga serikalini na Ruth Osoro itaendelea kusikilizwa siku hiyohiyo.
Makonda yukowapi anadili nawengine akati wateule wababa yake waharibifu,dilinao kwanza hao ndipo urudi kwa majority
 
Kisheria kama wanandoa wametengana kwa miaka mitatu mfululizo kwa uamuzi wao wenyewe, basi ndoa haipo tena. Hata hivyo, huyo mke anang'ang'ania ndoa na kusema haivunjiki wakati haishi na mumewe maana yake nini? Hivi hajui mumewe anaweza kusema amekubali warudiane halafu akanunua magunia mawili ya mkaa akafanya kile yule jamaa alichofanya kwa mke wake akamchomelea mbali?
 
Haya mambo ya ndoa magumu sana. Huyu mwanamke nadhani anataka afaidi mafao ya mumewe hapo baadae kama mapenzi hamna unamgandia nn mwenzio na mtoto kashakua?
 
Kuna mambo mawili hapa inabidi DC uyatazame kwa makini
1. Mwajiri wako hapendezwi na kitendo cha kutumia muda mwingi mahakamani wakati watu wake wakikosa mtatuzi wa kero zao.
2. Haya ni maisha tu, kuendelea kuishi na huyo mama hakukugharimu chochote, ni kweli inawezekana ana mapungufu yote hayo, fikiria kwanini mwanzoni ulishauriwa utoe talaka ukakataa na leo wewe uliyekataa kutoa talaka ndiye unaomba talaka, tafakari kwa kina Mungu anaongea nawe jipe nafasi ya kutafakari jambo hilo
 
Haya mambo ya ndoa magumu sana. Huyu mwanamke nadhani anataka afaidi mafao ya mumewe hapo baadae kama mapenzi hamna unamgandia nn mwenzio na mtoto kashakua?


Huenda tunapoteza muda wetu bure kuchangia hii mada, huyo bibi ana asili ya kanda gani
 
Huyo mke anaeng'ang'ania ndoa kisa ya kanisani hajielewi. Ndoa sio makaratasi. Kama hawaishi wote,hakuna mapenzi. Hapo hakuna ndoa tena. Ila wajaluo nao wa kuoa wake wengi hawajambo.
Anamkomoa tu hamna jingine.
 
Huyo mwanamke mpenda hela,anataka afaidi za u-DC
 
Huyo mwanamke namshangaa,akubali hiyo talaka.Huyo mkuu wa wilaya nae si akafunge ya serikali ? Maana baada ya hiyo ana ndoa nyingine ya serikali ambayo pia anatoa talaka. Ila hii kesi itafundisha wengi. Ngoja tuone mwisho wake.
Huyu DC nae anahangaika tu nyama ni ileile tu japo mapishi tofauti,lakini nyama inabaki nyama tu. Watu wa Mara wanapenda sana kuoa kila akipata vipesa basi anaoa,halafu Israel akimchukua anaacha kadhia za mambo ya mirathi mahakamani.
 
Huyo mke anaeng'ang'ania ndoa kisa ya kanisani hajielewi. Ndoa sio makaratasi. Kama hawaishi wote,hakuna mapenzi. Hapo hakuna ndoa tena. Ila wajaluo nao wa kuoa wake wengi hawajambo.
Mkuu kwa mantiki ya maelezo ni kwamba, baada ya kushindwana ndiyo akaoa mke mwingine bomani ambaye naye wameshindwana pia.

Kwa maelezo ya mdai talaka na maswali ya mdaiwa, yananivuta kuwa upande wa dc.
 
Kuna mambo mawili hapa inabidi DC uyatazame kwa makini
1. Mwajiri wako hapendezwi na kitendo cha kutumia muda mwingi mahakamani wakati watu wake wakikosa mtatuzi wa kero zao.
2. Haya ni maisha tu, kuendelea kuishi na huyo mama hakukugharimu chochote, ni kweli inawezekana ana mapungufu yote hayo, fikiria kwanini mwanzoni ulishauriwa utoe talaka ukakataa na leo wewe uliyekataa kutoa talaka ndiye unaomba talaka, tafakari kwa kina Mungu anaongea nawe jipe nafasi ya kutafakari jambo hilo
Hayo mengine tusimuhusishe sana Mungu, kwa sababu inaonesha kwa maelezo ya hapo mahakamani, huyo mwanamke ni maruhuni na kuna mtu kamkochi ujinga.

Point hapo ni kwamba, hawa viongozi wanatakiwa kuwa kioo cha jamii.

Hatakiwi kuonesha missbehave ya aina yoyote ile ama dalili, ama kuhisiwa tu.

Hii kesi inatafsiri mbovu sana kwa huyo dc, tafsiri ya kushindwa kuicontrol familia yake.

Mtu anayeshindwa kuongoza vizuri familia yake ambayo ni kikundi kidogo cha watu, je kundi kubwa la kijamii kama wilaya?

Huyo moja kwa moja kajinyang'anya sifa mwenyewe na hastahili kupewa uongozi hata wa kitongoji.

Watu wa maadali ama mwajiri wake, waliangalie hili, ili hatua madhubuti za kimaadili zichukuliwe mapema dhidi yake,hata kabla kesi hii haijafikia ukomo.

Kwenye kada ya uongozi hafai hata kulumangila, aondolewe akafanye kazi nyingine.
 
Back
Top Bottom