DC adai talaka mbili kwa mpigo mahakamani

BIGURUBE

BIGURUBE

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2014
Messages
6,699
Points
2,000
BIGURUBE

BIGURUBE

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2014
6,699 2,000
DC aeleza sababu ya kuomba talaka
Thursday August 15 2019

Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga amedai kuwa huwa anatoa matunzo ya mtoto wao wa kike ambaye kwa sasa anasoma kidato cha sita aliyezaa na Medelina Mbuwuli aliyefunga naye ndoa ya Kikristo mwaka 2001.

Mkuu wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, Simon Odunga (aliyevaa suti) akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Mwazo iliyopo Ukonga Jijini Dar es salaam jana. Picha na Omar Fungo
BY Tausi Ally, Mwananchi tally@ mwananchi.co.tz

Advertisement
Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga amedai kuwa huwa anatoa matunzo ya mtoto wao wa kike ambaye kwa sasa anasoma kidato cha sita aliyezaa na Medelina Mbuwuli aliyefunga naye ndoa ya Kikristo mwaka 2001.

Alidai hayo jana katika Mahakama ya Mwanzo Ukonga alipokuwa akitoa ushahidi katika kesi ya madai ya talaka namba 181 ya mwaka huu aliyoifungua katika Mahakama ya Mwanzo Ukonga, Dar es Salaam.

Odunga, akitoa ushahidi huo mbele ya Hakimu, Christina Luguru alisema anaomba talaka kwa sababu ametengana na mkewe huyo tangu mwaka 2003 na kwamba katika maisha yao ya ndoa, walikuwa wakigombana mara kwa mara kiasi cha kutengana na kipindi chote hicho alikuwa hana kazi. Alidai kuwa ilipofika mwaka 2002 alipata kazi akapanga nyumba eneo la Makuburi akamfuata mkewe wakasuluhishwa na wakarudiana kuishi pamoja.

“Baada ya kusuluhishwa tuliishi hadi mwaka 2003 pamoja, lakini hatukuwa na maelewano, siku moja nilipokuwa kazini mke wangu aliamua kuhama nyumba bila kunitaarifu.”

Alidai kuwa baada ya mama huyo kuondoka, alikaa na familia yake wakashauriana kuwa amtafute kwa ajili ya kumtunza mtoto na wakati huo alikuwa anasoma shule ya awali.


Alidai kuwa aliwahi kwenda katika shule ya awali aliyokuwa akisoma mtoto wao na kukuta ameandikishwa kuwa ana mzazi mmoja na kwamba baba yake alishakufa hivyo alikataliwa.

“Nilirudi kwa familia za pande zote mbili tukafanya kikao na mke wangu aligoma kuishi na mimi akidai niendelee kumtunza mtoto, kikao kiliamua nimpatie talaka, hatua ambayo sikuitekeleza hadi sasa ninapoiomba hapa mahakamani,” alieleza Odunga.

“Ila nimekuwa nikipeleka matunzo ya mtoto nyumbani kwake, lakini kuna siku nilishambuliwa, nikazuiliwa kwenda.”

Alidai kuwa amekuwa akimlea mtoto wake kwa tabu kwa sababu mdaiwa hataki aende nyumbani kwake, lakini ameendelea kutoa huduma kama ada kwa kumpatia mama yake. Alidai pia kwamba mtoto huyo alifaulu lakini mama yake alimpeleka shule binafsi, “hivyo nilikuwa nikitoa huduma kulingana na uwezo wangu.”

Kutokana na maelezo hayo, aliomba mahakama iivunje ndo hiyo kwa kuwa ilishindikana kusuluhishwa ngazi ya familia ambayo ilimpatia baraka ya kutoa talaka.

Baada ya Odunga kutoa ushahidi huo, Medelina alimuuliza kama alishawahi kwenda kanisani kabla ya kufika mahakamani na alijibu kuwa alienda mwaka 2001 na 2003.

Medelina alimuuliza tena Odunga kama alikuwa akitoa ada ya shule ya mtoto tangu mwanzo, anaweza kukumbuka jina la shule aliyokuwa akisoma mtoto wao na kujibu kuwa hakumbuki ila anajua mahali ilipo na sasa hajui anasoma wapi.

Alimuuliza tena kama anaweza kuithibitishia mahakama hata kwa risiti za ada na Odunga alidai kuwa alikuwa akimpa fedha taslimu.

Shahidi wa Odunga, Godol Odunga (61) maarufu Ogonda alidai kuwa mdai na mdaiwa walifunga ndoa ya Kikristo lakini hakumbuki ilikuwa lini na mwaka 2003 walitengana na kila mmoja aliishi peke yake.

Alidai kuwa kati ya mwaka 2012 na 2013 kikao cha ukoo kilikaa na Odunga alidai kuwa anataka kuoa mke mwingine na akaagizwa kama anataka hiyo atoe talaka kwanza.

Baada ya kutoa ushahidi huo, Medelina alimuuliza wewe ni mtumishi wa Mungu ulishawahi kuona ndoa ya kanisani inavunjwa mahakamani? Shahidi huyo akajibu, “mimi nasema ninachojua.”

Odunga alifunga ushahidi wake na kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa Medilina na mashahidi wake watano Agosti 19.

Kesi nyingine ya madai ya talaka iliyofunguliwa na Odunga mahakamani hapo dhidi ya ndoa aliyoifunga serikalini na Ruth Osoro itaendelea kusikilizwa siku hiyohiyo.
 
Victoire

Victoire

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2008
Messages
13,837
Points
2,000
Victoire

Victoire

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2008
13,837 2,000
Huyo mke anaeng'ang'ania ndoa kisa ya kanisani hajielewi. Ndoa sio makaratasi. Kama hawaishi wote,hakuna mapenzi. Hapo hakuna ndoa tena. Ila wajaluo nao wa kuoa wake wengi hawajambo.
 
leroy

leroy

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2010
Messages
1,103
Points
2,000
leroy

leroy

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2010
1,103 2,000
Kama hakumbuki alifunga lini ndoa basi akumbuke tu alifungia kanisa gani na la wapi. Maana makanisa yana database kubwa sana.
 
Root

Root

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Messages
31,459
Points
2,000
Root

Root

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2012
31,459 2,000
Kumbe talaka ni ngumu kuipata
 
Daby

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Messages
30,195
Points
2,000
Daby

Daby

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2014
30,195 2,000
Hakuna,labda kwenye urithi mme akifa. Ila masuala ya kifo huwezi jua nani atatangulia. Maana kama hakuna mapenzi tena,hakuna tendo la ndoa. Hiyo ndoa ya nini sasa?
Analisha ego.

Nayo ni faida kwake....siunaona mme alitaka kuoa akaambiwa kavunje ile ya mwanzo ndiyo tufunge ya sasa. Na pia anaogopa madhara ya kuoa mwingine ilihali ile haijafutika.

Ni wachache huombea ma ex wao wayafurahie maisha baada ya kuacha.
 
Victoire

Victoire

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2008
Messages
13,837
Points
2,000
Victoire

Victoire

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2008
13,837 2,000
Analisha ego.

Nayo ni faida kwake....siunaona mme alitaka kuoa akaambiwa kavunje ile ya mwanzo ndiyo tufunge ya sasa. Na pia anaogopa madhara ya kuoa mwingine ilihali ile haijafutika.

Ni wachache huombea ma ex wao wayafurahie maisha baada ya kuacha.
Huyo mwanamke namshangaa,akubali hiyo talaka.Huyo mkuu wa wilaya nae si akafunge ya serikali ? Maana baada ya hiyo ana ndoa nyingine ya serikali ambayo pia anatoa talaka. Ila hii kesi itafundisha wengi. Ngoja tuone mwisho wake.
 
kijana wa leo

kijana wa leo

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2011
Messages
2,668
Points
2,000
kijana wa leo

kijana wa leo

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2011
2,668 2,000
Kiufupi huyu ndo kavurugwa na mapenzi, yani talaka kwa wake wawili kwa mpigo!!!
 
Sumve 2015

Sumve 2015

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Messages
2,638
Points
2,000
Sumve 2015

Sumve 2015

JF-Expert Member
Joined Jun 16, 2013
2,638 2,000
Mmnh...isije ikawa DC kajisevia kile ki katibu tawala cha Nchemba Zahra Muhidin binti wa Michuzi maana nakaona nowadays kanavaa miguo mipanamipana kana kwamba kanategemea na hakajawahi kuolewa.
 
radicals

radicals

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Messages
3,470
Points
2,000
radicals

radicals

JF-Expert Member
Joined Nov 7, 2016
3,470 2,000
mh, jamaa ni hodari, anataka kutoa talaka mbili kwa mpigo
 
lazalaza

lazalaza

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2012
Messages
2,405
Points
2,000
lazalaza

lazalaza

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2012
2,405 2,000
Ndoa bwana kabla hujaingia unaona wenzako wanafaidi sana ukiingia Ndiyo mziki wake unaanza upya.
 
Saguda47

Saguda47

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Messages
6,906
Points
2,000
Saguda47

Saguda47

JF-Expert Member
Joined May 1, 2016
6,906 2,000
Mmnh...isije ikawa DC kajisevia kile ki katibu tawala cha Nchemba Zahra Muhidin binti wa Michuzi maana nakaona nowadays kanavaa miguo mipanamipana kana kwamba kanategemea na hakajawahi kuolewa.
Unaujua mnada wa soya?
 
tusipotoshane

tusipotoshane

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2018
Messages
359
Points
500
tusipotoshane

tusipotoshane

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2018
359 500
Ndoa bwana kabla hujaingia unaona wenzako wanafaidi sana ukiingia Ndiyo mziki wake unaanza upya.
Mkiwa wote mnajielewa inakuwa murua tu,ila kama wote micharuko,ni chungu kama k-vant.
 

Forum statistics

Threads 1,326,674
Members 509,566
Posts 32,230,516
Top